Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

Nakushauri tenga muda wa kutosha kusoma historia ya mapinduzi ya Zanzibar.
 
Tulifundishwa darasani kuwa ni Karume aliyeongoza mapinduzi na hatukutajiwa huyo John. Kwani vipi?
 

Ni kama nyie mlivokuwa mkitumwa na wakiristo tu waislam wakawasaidia kutoka utumwani mwa wakiristo kisha shujaa mkamuoma Nyerere peke ake
 
Baraghash,
John Okello hakupatapo kuwa ''kiongozi mkuu,'' wa Mapinduzi ya Zanzibar.
Ukiwa huu ndiyo ukweli hiyo heshima ya jina lake lipewe mnara itakuwa haipo pia.

Ikiwa Okello ndiye ''kiongozi mkuu,'' Abdallah Kassim Hanga atachukua nafasi gani?
Oscar Kambona atapewa heshima gani?

Victor Mkello je?
Au Mohamed Omar Mkwawa nini nafasi zao katika mapinduzi ya Zanzibar?

Vipi kuhusu Ali Mwinyi Tambwe na Jumanne Abdallah.
Vipi kuhusu Wayahudi waliokuwa wakiisaidia Afro-Shirazi Party?

Vipi kuhusu meli ya silaha kutoka Algeria?
Historia ya Mapinduzi ina mengi ambayo wengi hawayajui.

Ukitaka kuijua historia ya Mapinduzi ya Zanzibar soma kitabu cha Dr. Harith Ghassany,
''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru (2010).

Hiki kitabu kipo ''online.''
Kisome uelimike.

Ndani ya kitabu hiki utakutana uso kwa uso na waliopanga mapinduzi na kila
mmoja nini ulikuwa mchango wake.

Okello hayumo katika hiyo orodha.

Inafurahisha sana na kwa hakika nimecheka kidogo ulipomfananisha Che Guevara
na Okello.

Che alikuwa Siera Maestra na Fidel Castro.

Okello hakuweko hata Kipumbwi na Mohamed Omari Mkwawa lilipotokea jeshi la
Wamakonde wakata mkonge kutoka shamba la Sakura walioingia Zanzibar na mapanga
kupindua serikali ya ZNP/ZPPP ya Mohamed Shamte.
 
Sasa kama hicho kitabu kinataja waliopigana vita ya maneno halafu hakimtaji yeye aliyeingia vitani physically kuna haja gani ya kukiamini... Kiko biased
 

Soma hapa kidogo
John Okello - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Okello ndiye aliyetoa silaha kwa vijana wa Kizanzibar wakati huo ili wafanikishe mapinduzi. Bila zile silaha na mafunzo ya namna ya kuzitumia mapinduzi yasingefanyika or perhaps yangechelewa kufanyika. Kusema mtu kama huyu hana mchango kwenye mapinduzi ni ukilaza wa kiwango cha juu sana.

Note: Okello alipeleka Zanzibar bunduki maelfu kwa maelfu kwa vijana wa kiafrika wa Zanzibar ili wampindue sultan.
 
 
Ahsante nimesoma Wikipedia na rejea zake ambamo wamo wasomi maarufu.

Kitu kimoja ambacho nitakufahamisha ni kuwa hao wote hakuna aliyepata bahati
ya kupata nyaraka na kauli ya watendaji wenyewe katika sakata zima la mapinduzi
kama Dr. Harith Ghassany.

Msome Dr. Ghassany utaelewa nini nakueleza.

Ikutoshe tu ni yeye peke yake katika watafiti baada ya zaidi ya miaka 40 ndiye aliyeleta
habari kuwa kulikuwa na askari mamluki kutoka mashamba ya mkonge waliovamia
Zanzibar kuja kupigana upande wa ASP.

Msome Ghassany yapo mengi utajifunza.
 
It is in the mark...nobody can erase it....John Okello. Just a question of time
 

HAMY -D,

Soma tena historia ya Mapinduzi na jielekeze katika mlango wa silaha zilizotumika.
Okello hakuwa na bunduki zozote.

Silaha zilizokuja kwa ajili ya mapinduzi alizileta Ben Bella wa Algeria na hazikutumika.
Silaha hizi zilipokelewa Dar es Salaam.

Dr. Ghassany kaeleza kwa kirefu sana ushiriki wa Ben Bella katika mapinduzi ya Zanzibar.
Mafunzo hakufanya Okello.

Kambi ya mafunzo ilikuwa Kipumbwi, Tanga na wasimamizi wake walikuwaa Ali Mwinyi
Tambwe
na Jumanne Abdallah.

Mamluki walikuwa chini ya uongozi wa Mohamed Omari Mkwawa na Victor Mkello.

Kubwa zaidi Dr. Ghassany aliongea na Ben Bella mwenyewe.
Picha zao zipo kwenye kitabu.

Msomeni Dr. Ghassany mtapata mengi.
Kitabu kipo bure online.
 
Kunaonekana kuwa kuna umakusudi fulani hivi wa kuficha historia ya mapinduzi ya Zanzibar kwa nini hali hiyo inatokea? Bahati nzuri bado wapo wengi ambao walikuwepo siku zile lakini kila mmoja anasema lake na kuvutia upande aupendao, sababu hasa ni nini?
 
Mkuu unachanganya sana, ama kwakujua au kwakutokujua.

Mapinduzi ya Znb haya tunayoyaona leo hayahusiani na hao uliowataja, si nyerere si karume si babu wala nani,

Kulikuwa na makundi matatu yote yakipanga mapinduzi, kundi la kwanza ni la Umma Party chini ya Abdulahman Babu, kundi la pili ni la ASP chini ya Karume akisaidiwa na Julius Nyerere kupitia Kipumbwi kule Tanga, na kundi la tatu ni la Okello na vijana wake (askari wa staafu wa kikoloni)

Kundi lililofanikiwa kufanya mapinduzi ni la Okello, na halikuwa na chama kabisa.

Karume na Nyerere na Babu wakapora mapinduzi hayo yani wakafanya mapinduzi ndani ya mapinduzi lakini bila umwagaji damu.

Ghasany ameandika mengi, lakini ameshindwa kung'amua kwamba kulikuwa na makundi matatu yakifanya mipango ya mapinduzi, na kundi la okello ndilo likafanikiwa.
 
Unadanganya, silaha toka Algeria kwa Ben Bela alizokwenda kuomba Abdulhman Babu zilichelewa Bandari ya Dar, zikafika Znb washamaliza kazi kwakutumia silaha zilezile za Sultan walizoziteka Okello na jeshi lake. Kwaujumla msaada wa ben bela haukuingia Zanzibar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…