Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

This could be the deepest information about the okello guy that I ve ever came across
 
Alikuwa kiongozi wa ASP na mwanaharakati wa kuleta utawala wa Waafrika dhidi ya udhalimu wa waarabu na wazungu walio wachache
Udhalimu wa waafrika kwa waafrika wenzao umevuka mipaka mpaka hii leo
 
Nawasalimu katika jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuwatumia salaam zangu za kuadhimisha kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, tutayalinda kwa gharama yoyote.

Nawatakia maadhimisho mema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Japo sasa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yanaelekea miaka 60, Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Maswali Bila Majibu -1

Kazi Iendelee!.

Paskali
 
Reference please!!
 
Unaifahamu historia ya karume? (I see it's just utopian)
 
Kwa nini tusiwaenzi kina Chief Mkwawa, Mangi Sina, Mangi Mandara, Wakina Chief Songea Mbano na Chief Chabruma wa kule Ruvuma, au Saidi Milambo wa tabora, wakina Isike, Kinjekitile, au Chief Masanja, Chief Mataka wa kule kwa wayao? Who's Okello?
Fafanuwa michango Yao Ili wapewe iyo heshima, michango wa okelo unafahamika
 

 
Fafanuwa michango Yao Ili wapewe iyo heshima, michango wa okelo unafahamika
Remedius...
Okello ana mchango gani katika historia ya mapinduzi ya Zanzibar?

Tatizo ninaloliona katika mjadala huu ni watu kuzidiwa na hisia ambazo hazima ithibati.

Waliohusika na mapinduzi ya Zanzibar wote wanafahamika.

Kwanza ni serikali ya Tanganyika baadhi ya viongozi wake na vyombo vyake vyote vya usalama.

Historia ya mapinduzi imeandikwa yote katika kitabu cha Dr. Harith Ghassany ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' na kuna mtu kaweka hapa kipande chote cha Okello lakini inaelekea wengi wenu hampendezewi na historia ya kweli mnapenda historia za kutunga.

Mara kadhaa hapa nimemweleza Okello na nafasi yake katika mapinduzi.

Mimi nilikuwa Mtafiti Msaidizi wa Dr. Ghassany kwa miaka saba wakati anatafiti historia hii.

Najua mengi sana.

Nashangaa ninaposoma historia zinazoletwa hapa kumtukuza Okello hatajwi Ali Mwinyi Tambwe, Jumanne Abdallah, Victor Mkello na Mohamed Omari Mkwawa.

Hawa ndiyo waliokuwa wasimamizi wa Kambi ya Kipumbwi, Tanga ambako ndiko walikowekwa mamluki wa Kimakonde waliovushwa kuingizwa Zanzibar kuipigia kura ASP katika uchaguzi wa Zanzibar wa mwaka wa 1961 na kusaidia katika mapinduzi mwaka 1964.

Upi mchango wa Oscar Kambona na Abdullah Kassim Hanga?

Upi mchango wa Wayahudi, Algeria na Waingereza wenyewe na washirika wake?

Upi mchango wa Makomredi?

Katika ''dramatis personae,'' yaani wahusika wa tamthlia hapa mliyemuona wa kujengewa sanamu ni Okello.

Hajajengewa mnara Hanga atajengewa Okello?

Okello hata kama asingekuwapo mapinduzi yangewezekana.

Lakini bila msaada wa Tanganyika mapinduzi yasingewezekana.

Tujifunze kusoma tunachotaka kujadiili kabla hatujaingia katika mijadala.

Kuna mengi hamyafahamu katika historia ya mapinduzi.


Kushoto Ali Mwinyi Tambwe amembeba Karume​
 

Bila okello mapinduzi yasingewezekana kumbuka wakati okello anaomgoza mapambano karume na wenzake walikua wamejificha lodge huku tanganyika,au mzee sideboy umesahau kuwa okello ndiye aliewatisha wazenji na sauti yake kali ya kiuongozi hadi sultani na wafuasi wake wakakimbia zenji?Shida Okello sio mfuasi wa dini ya waarabu ndio mana huwezi kumkubali,Nyerere tu humkubali iweje okello. ?
 
Jiwe...
Kama kuongoza tumchukue mtu mmoja tu katika mapinduzi.

Aboud Mmasai
Unaujua mchango wake?

Karume hakujificha.

Karume kuja Dar-es-Salaam ulikuwa uamuzi wa ASP na akija mara nyingi na Special Branch wakijua hata nyumba aliyokuwa akifikia.

Karume na Abbas Sykes walikuwa na uhusiono maalum.

Kwanza Karume alijulishwa kwa Nyerere na Abdul Sykes kaka yake Abbas na ilikuwa safari maalum aliyofanya Abdul na Dossa Aziz kumpeleka Nyerere Zanzibar kumjulisha kwa Karume.

Abbas ndiye aliyekuwa akimpelekea Karume fedha Zanzibar kwa ajili ya harakati za ASP.

Ndiyo ikawa Karume akija Dar-es-Salaam Alikuwa anafikia nyumbani kwa Regional Commissioner wa Eastern Province Abbas Sykes Shaaban Robert Street.

Haya ndiyo msiyoyajua na hamna ujasiri wa kujifunza yale msiyoyafahamu.

Kilichompa umaarufu Okello ni kule kupewa kazi ya kutoa matangazo radioni na akawa anaropoka maneno ya ovyo.
 
Upo sahihi okello John anamchango mkubwa kwenye mapinduzi ya Zanzibar but historia imemtupa nnje na kumpa mwingne sifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…