Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

Kutoka kwenye vyanzo mbali mbali nilivyosoma, nilikuja kugundua Okelo pamoja mambo mazuri yote aliyokuwa nayo lakini still alikuja kuwa mroho wa madaraka maana baada ya kuondoka Zanzibar alienda Congo Kinshasa na baadae Uganda ambako Idd Amin aliamin anaweza kufanya nae kazi na kumteua baadae okelo akamkejeli Idd Amin kwa kumwambia "Nafurahi sasa Nchi ya Uganda inakwenda kuwa na Field Marshal wawili" hapo Idd Amin ndipo alipoanza kuarrange mipango ya kifo chake.
 
Kwa nini tusiwaenzi kina Chief Mkwawa, Mangi Sina, Mangi Mandara, Wakina Chief Songea Mbano na Chief Chabruma wa kule Ruvuma, au Saidi Milambo wa tabora, wakina Isike, Kinjekitile, au Chief Masanja, Chief Mataka wa kule kwa wayao? Who's Okello?
Kwan Songea Mbano alikua ni Chief au Nduna maana Chief najua alikua Mputa Gama
 

Ule ulikuwa uhuru bandia , huu tulionao ni uhuru wa Tamthilia😭😭😭😭😭😭😭😭
 
Ninasoma Historia
 

Kumbe Afro Shirazi iliingia kwenye uchaguzi kutafuta uhuru bandia ? Walipoukosa wakaja kwa Nyerere kuomba askari wa kuuchukuwa kwa nguvu ule uhuru bandia?
 
Kumbe Afro Shirazi iliingia kwenye uchaguzi kutafuta uhuru bandia ? Walipoukosa wakaja kwa Nyerere kuomba askari wa kuuchukuwa kwa nguvu ule uhuru bandia?
Hakuna kitu kama hicho. Hawo ni mabaki wa Watumws waliovhotwa Tanganyika wana hasira zao. Wewe ungewekwa utumwa ungefurahi?
 
Hakuna kitu kama hicho. Hawo ni mabaki wa Watumws waliovhotwa Tanganyika wana hasira zao. Wewe ungewekwa utumwa ungefurahi?
Nani mtumwa .,hizo ni propaganda za kanisa , labda wewe ndiye ulikuwa mtumwa
 
Tarehe kama ya leo 11/01/1964 miaka 60 iliyopita, ndio Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalifanyika!. Alfajiri ya Tarehe 12 Januari, 1964 ilikuwa ni kutangazwa tuu!.

Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Paskali
 
Tarehe kama ya leo 11/01/1964 miaka 60 iliyopita, ndio Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalifanyika!. Alfajiri ya Tarehe 12 Januari, 1964 ilikuwa ni kutangazwa tuu!.

Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Paskali

AZAM TV: MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUTOKA KUMBUKUMBU ZILIZOZIKWA​

Mohamed Said Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania January 11, 2016

Utangulizi

Makala haya nimeandika katika Kumbukumbu ya Mapinduzi mwaka wa 2016 kutokana na mahojiano na AZAM TV.

Kpindi hiki kilisababisha matatizo kutokana na yale ambayo nilizungumza kuhusu mapinduzi.

AZAM hawakunialika tena kwa miaka minane baada ya kipindi hiki hadi mwaka huu.

Ikiwa ulisikiliza kipindi tulichofanya mwaka huu katika kumbukumbu ya mapinduzi miaka 60 utaona kuwa nilikataa kujibu mswali kadhaa.

Baadhi ya watu hapa wamenilaumu kwa kukataa kujibu mswali kuhusu mapinduzi kama inavyostahili.


Leo asubuhi nilifanyiwa mahojiano na mtangazaji Faraja Sindegea wa Azam TV kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar. Mtangazaji alifungua kipindi kwa utangulizi kuhusu historia ya mapinduzi na umuhimu wa kuyaenzi mapinduzi. Nilimtaka radhi kwa kumwambia kuwa itafaa kama tutayazungumza mapinduzi kutoka kumbukumbu ya mashujaa waliopigania uhuru wa Zanzibar lakini michango yao haitambuliwa na nchi yetu.

Nilikwenda moja kwa moja kwenye kumbukumbu za Aman Thani kueleza yale ambayo si wengi wanayafahamu. Watazamaji nadhani kwa mara ya kwanza waliona picha ya Aman Thani kwenye televiseheni zao na picha ndiyo hiyo hapo juu. Nilieleza kuwa nimezisoma kumbukumbu za Aman Thani na niligusia umuhimu wa nyaraka zake kwa mwanafunzi yoyote yule anaejifunza historia ya siasa za Afrika hususan historia ya Zanzibar na mapinduzi yaliyokuja kutokea mwaka wa 1964.

Nimesema kuwa kumbukumbu za Aman Thani zinakuja na picha nyingine kabisa ya mapinduzi ambayo si wengi wanaijua. Nilieleza kuwa ni Aman Thani peke yake katika wafungwa wa siasa wa Zanzibar aliyeweza kueleza kwa kirefu kuhusu Jela za Mateso zilizoundwa baada ya mapinduzi na jinsi alivokabiliana na Mtesaji Mkuu Hassan Mandera.

Niliwaonyesha watazamaji baadhi ya vitabu muhimu vya historia ya Zanzibar pamoja na kitabu, ''Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha,'' kitabu ambacho nilisema mwandishi Minael- Hosanna O. Mdundo amepotosha mambo mengi.

Mtangazaji Faraja alitaka kujua John Okello ni nani. Nilimweleza kuwa John Okello hakuwa chochote katika mapinduzi ila alitumiwa kutoa matangazo ya kuwatisha wananchi. Kwa lugha ya wenye mapinduzi yao ni kuwa, ''Walimvisha blanketi la U-Field Marshall na likamwenea na yeye mwenyewe akaamini khasa kuwa hakika ni ''Field Marshall,'' Hapa kuhusu, ''Blanketi la Okello,'' niliwapeleka watazamaji wangu kwenye rejea ya kitabu cha Dr. Harith Ghassany, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru.''

Nilimtaja Abdallah Kassim Hanga kuwa ndiye aliyepanga mapinduzi akishirikiana na serikali ya Tanganyika chini ya Julius Nyerere. Katika muktadha huu niliwarejesha tena watazamaji kwenya kumbukumbu za Aman Thani aliposema kuwa hayakuwa ''mapinduzi,'' bali mavamizi.

Aman Thani nikaeleza kuwa ametoa changamoto katika picha maarufu ya Okello hapo juu kuwa atokee mtu awaonyeshe Wazanzibari khalis katika picha ile.

Baadhi ya mawaziri wa serikali iliyopinduliwa
Kushoto: Ibun Saleh, Juma Aley, Mohamed Shamte, Dr, Baalawy na Ali Muhsin Barwani​




Niliendelea kusema kusema kuwa hatujapatapo kusheherekea Mapinduzi ya Zanzibar katika hali ya majonzi kama mwaka huu. Moja kwa moja nikawafahamisha watazamaji kuwa tunasheherekea mapinduzi tukiwa katika hali ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar wamepanda jahazi la ubaguzi wa rangi kwa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kuonyesha bango la kibaguzi wakiwabagua Wazanzibari ambao hawakuzaliwa na ngozi nyeusi habari ambazo zimezagaa katika mitandao ya kijamii kama moto wa makumbi. Nilimweleza mtangazaji kuwa sitaki kuamini kuwa CCM Zanzibar imefilisika kiasi hiki. Nilieleza maana ya ''Hizbu,'' kuwa ni neno la Kiarabu lenye maana ya ''Chama'' na ''Watan,'' maana yake ni ''Taifa.''

Hapa nikaeleza historia ya Tanzania kuwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika kulikuwa na Wazungu na Wahindi waliokuwa viongozi wa TANU na wakisimama kugombea nafasi za uongozi na wakishinda bila ubaguzi. Nilimtaja Sophia Mustafa, Ratansey, Amir Jamal, Dereck Bryceson na nikaeleza kuwa katika Bunge la Tanzania kuna kila aina ya wabunge mpaka Makalasinga.

Nikaeleza kuwa huko Zanzibar tumekuwa na rais Amani Abeid Karume ambae baba yake asili yake ni Mnyasa na mama yake ana asili ya Kihindi. Nikawauliza hawa wabaguzi kuwa hivi ndugu zetu kama Mansour Yusuf Himid na Mahamoud Thabit Kombo na wengi wao Amani Karume mwenyewe na binti yake Fatma watajisikiaje kwa kauli kama hizi za ugozi? Nilifanya rejea za Ton Ton Macout wa Papa Doc wa Haiti ambae alitumia mbinu za vitisho kwa wananchi wake mfano wa Mazombie wa Zanzibar halikadhalika nilitahadharisha hatari ya kuwatumia vijana kama walivyotumiwa na Adolf Hitler kwa kutengeneza ''Stormtroopers,'' au ''Brown Shirts,'' kuwatisha wananchi. Nikawaeleza viongozi waisome historia ili wapate mafunzo nini ilikuwa hatima ya mambo haya.

Nilieleza kuwa historia nyingi ya mapinduzi ya Zanzibar imo katika vifua vya watu wengi wao wameshatangulia mbele ya haki. Wengi katika hao kwa njia moja au nyingine walishiriki wakiwa Bara katika kuiangusha serikali ya Zanzibar. Lakini kutokana na mauaji yaliyotokea katika mapinduzi na baadae wengi wao walifunga midomo yao na hawakutaka watu wajue kuwa walihusika. Mfano mmoja niliouleza ni wa Ali Mwinyi Tambwe.

Nilieleza kwa uchache kuwa Ally Sykes alimgusia Dr. Harith Ghassany kuwa wao ndiyo walimjulisha Nyerere kwa Karume.

Mtangazaji alitaka tuhitimishe mahojiano yetu kwa mimi kueleza hali ya baadae ya Zanzibar. Nilimueleza kuwa Wazanzibari wamefanya uchaguzi na CCM Zanzibar imeshindwa kwa ufupi ni kuwa, ''The people of Zanzibar have spoken,'' hakuna njia yeyote nyingine ila kwa walioshindwa kukubali kushindwa na maneno ya Ali Mohamed Shein kuwa kesi yake ipelekwe mahakamani ni jambo linalotufedhehesha.

Itakuwa kichekesho cha mwaka mtu ashindwe uchaguzi dhahiri na anapoelezwa hivyo aseme, ''Nenda mahakamani mimi ni rais halali.''​
 

AZAM TV: MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUTOKA KUMBUKUMBU ZILIZOZIKWA​

Mohamed Said Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania January 11, 2016
Nimesema kuwa kumbukumbu za Aman Thani zinakuja na picha nyingine kabisa ya mapinduzi ambayo si wengi wanaijua.
Mkuu Maalim Mohamed Said, asante sana kwa simulizi hii, Channel Ten wamenipa fursa kuzungumzia Katiba, Sheria na Haki, kila siku za Jumapili Saa 3:00 usiku. Nitakuja kutafuta wasaa ni fanye mahojiano na wewe kuhusu harakati za uhuru wa Tanganyika na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa siku za usoni.
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=7qgFBAnYXa2dRzFB Hapa nimemshauri Dada na mdogo, Zanzibar iundwe tume ya Truth and Reconciliation waliopo hai walioteswa wateme nyongo zao na watesi waombe msamaha na kuridhiana, tena nikashauri hata jina la Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, neno Matukufu lisiendelee kutumika, hivyo nimeshauri kwanza kusameheana Voices From Within: Sultan Jamshid bin Abdullah Al Said Atafurahi Zaidi, Kama Ata... Zanzibar!, Rais Samia, Rais Mwinyi, Sameheni, Mtabarikiwa Sana!.
Kisha nikashauri Zanzibar itendewe haki Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Tuyaenzi kwa 4R za Rais Samia?, JMT Tuitendee Haki Zanzibar?, Tuwatendee Haki Wazanzibari? Mshindi Halali Apewe?
P


 
Issues za Mapinduzi ya Zanzibar ni very sensitive topic, hivyo ulichofanya mwaka huu ni vema kujifanyia self censorship maana hao wenye TV zao huwa wanaitwa mahali kuhojiwa.

Mimi nilipoteza kazi TBC kwa issue ya Zanzibar!, ule uchaguzi wa 2000, nilikuwa naendesha kipindi cha Ulingo wa Siasa, kwenye uchaguzi wa Zanzibar, kila nikimuomba Amani interview, CCM wanakataa, kila nikimuita Maalim Seif, anakuja, uchaguzi ulipokaribia nikamwalika tena Amani na Seif, Amani hakurespond, Seif akakubali kuja, siku ya kipindi ni kesho, leo naitwa kuelezwa kesho Amani anakuja, nikawaeleza niliisha mualika Maalim na leo amelala Starlight hotel kusubiria kuja kesho, nikaambia m cancel Seif, anakuja Amani. Kweli nikam cancel Maalim, kesho yake Amani akaja, it's very unfortunately yeye sio muongeaji mzuri lakini tukafanya kipindi. Kikaruka, kipindi kilichofuata ndio cha mwisho, hivyo nikamuita Maalim Seif, kumbe Maalim aliangalia kipindi cha Amani, hivyo kwenye kipindi chake, Ali m counter Amani mwanzo mwisho!.

Kwenye uchaguzi wanaijua wenyewe kilichotokea, ila baada ya uchaguzi, nikapigwa zengwe kuwa it was my plan kumtanguliza Amani, kisha nikamleta Seif ili aamalize Amani!. Kwa TVT, that was like treason!. Nilipigwa summary dismissal kwa kosa la insubordination!. That was the end of me TBC.
P
 
Haya mambo ya Chaguzi za Zanzibar, ni mimi ndie niliyetangaza matokeo halisi ya kweli ile 1995 nikiwa Channel Ten.

Kabla ya uchaguzi wa 2015 nikawashauri Kumuepushia aibu ya Kushindwa, CCM isimsimamishe Dr. Shein hawakusikia!, ni kweli uchaguzi ule alishindwa ndipo Jecha akapindua meza na kufunika kombe! Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda
Tumemuomba sana Mama, Uchaguzi wa 2025 ni haki bin haki na mshindi wa haki, atatangwa!.
P
 
Issues za Mapinduzi ya Zanzibar ni very sensitive topic,
Ni kweli, nilimuuliza Sheikh Said ikiwa Mapinduzi ni halali au ni haramu. Sijawahi kupata jibu zaidi ya ku'dance'

Kuna ''Mwarabu wa London'' Bw Rajab, yeye alijaribu lakini pia hakuwa na jibu la moja kwa moja.
Katika gazeti la Raia mwema, alisema ' kwamba ni halali au haramu inatagemea mtu yupo upande gani''

Ni nadra kumsikia Jussa akitamka neno Mapinduzi lakini ni kawaida sana kumsikia Mansour Himid akitamka.
Mifano hiyo inaonyesha sensitivity ya jambo zima na linavyowagawa Wazanzibar hasa kwa rangi na nywele

Niliwahi kumuuliza Mo ikiwa Mapinduzi ni haramu na yalifanywa na Watu kutoka Tanganyika kambi ya Kipumbwi, je, Wazanzibar wanaosherehekea wanafanya makosa kutukuza haramu?
Hakuna jibu hadi kesho, ana 'dance' tu

Kwa bahati mbaya katika wale 12 wa Baraza la Mapinduzi wengi wametangulia mbele ya haki, waliobaki wachache ni A.H.Mwinyi sina habari za Kanali S.Bakar. JokaKuu kama una taarifa zaidi tafadhali

Wanamapinduzi 12 hawakuacha nyaraka kwa kimaandishi kama vitabu vya kueleza nini kilijiri, sijui kama walikatazwa au la. Tunabaki na simulizi za upande mmoja kutoka Oman au mrengo wa Kiimani.
Kinachosikitisha ni chombo kama TBC kinachoendeshwa kwa kodi zetu kinatumiwa 'kiharamia'

Tido alilipa gharama pia kwa kutaka kuiweka TBC huru. Aliahidi kuonyesha chaguzi mubashara. CCM hawakubaliani na mambo ya kwenye mwanga, wanapenda mambo kizani, Tido akalipia gharama.

Lakini pia kuna kauli nimeisikia na hapa Mohamed atanisahihisha kwamba ' kuna nyakati heri inafichwa ndani ya shari'' kule Buckingham palace wanasema '' a blessing in disguise' , Tido is better off today.
 
Nguruvi...
Bahati mbaya unaandika kwa kukejeli.
Umemkejeli Ahmed Rajab na umenikejeli mimi pia.

Laiti ungeandika kwa ustaarabu ningeweza kushawishika kuchangia.
Nimejifunza mengi kutoka kwa Ahmed Rajab katika historia ya Zanzibar.

Si mtu wa kuvunjiwa heshima yake hapa.


Mwandishi na Ahmed Rajab, Mhariri wa Africa Analysis, Barbican London 1991
 
Wewe mbuzi huwezi kuja kwenye mijadala huru ambapo unaweza kula za uso, unajificha kwenye jukwaa lako la kujijibu mwenyewe kule
Maandiko yako mengi ya kushindana na historia au maelezo yanahusina na jamii ya dini ya kiislamu au Zanzibar
Huna cha maana humu zaidi ya kushindana na muda, badala ya kushindana na umbali kati ya sebule na mlango wa choo kama utaweza kufika on time
 
Wewe mbuzi huwezi kuja kwenye mijadala huru ambapo unaweza kula za uso, unajificha kwenye jukwaa lako la kujijibu mwenyewe kule
Nipo kila mahali wala sina tatizo. Huu mjadala tulikuwa nao ndio maana ninaweza kumnukuu Mohamed Said , twafahamiana vema tu.

Kumbe unatembelea lile jukwaa, nashukuru kuwa msomaji wangu! Allah akujaze neeghma zake
Maandiko yako mengi ya kushindana na historia au maelezo yanahusina na jamii ya dini ya kiislamu au Zanzibar
Huwezi kutenga Uislama na Historia ya Zanzibar. Leo 99% ya Wazanzibar ni Waislam, kuna kosa gani kuwa mwislam na Mzanzibar?
Huna cha maana humu zaidi ya kushindana na muda, badala ya kushindana na umbali kati ya sebule na mlango wa choo kama utaweza kufika on time
Kipi cha maana ulichoandika? Katika aya tatu nilizo nukuu kipi cha maana msomaji amepata kutoka kwako.

Mzee wangu Mmoja akiishi Ubwari hapa Tanga, aliwahi niambia hakuna mtu asiye na hoja.
Yule unayedhani hana hoja ana hoja hata kama ni tusi, tofauti ni thamani ya hoja.

Ningefurahi ungepitia mstari mmoja hadi mwingine uonyeshe upotofu wangu. Tunahitaji hoja , matusi si pake

Ninakueleza ninachotaka kukueleza si kile unachotaka kusikia.

Mimi si miongoni mwa wanaokaa kitako kusikiliza simulizi kisha kuondoka nazo na kuzifanya mwenge!
Wale wa Zanzibar nchi ya kwanza kuwa na TV ya rangi wakati alikuwa nayo Sultani peke yake.

Ukitaka kujua sensitivity ya jambo la Mapinduzi nimekupa mifano.
Jussa hutamasikia akitamka neno 'Mapinduzi' Mansour Himid anatamka Mapinduzi kwa ufahari. Jiulize

Ajira zinatolewa kwa kuangalia vyeti na sifa ya mhusika zikiwemo nywele.

Mapinduzi daima wanabeba mabango... halafu kuna mamlaka kamili turudishe hadhi... Tuachie hapo
 
Nipo kila mahali wala sina tatizo. Huu mjadala tulikuwa nao ndio maana ninaweza kumnukuu @Mohamed Said , twafahamiana vema tu.

Kumbe unatembelea lile jukwaa, nashukuru kuwa msomaji wangu! Allah akujaze neeghma zake
Na uendelee kuwepo tu kama upo upo
Ya kumnukuu mzee said hayanihusu
Na sina muda huo wa kupoteza kusoma pumba za hilo jukwaa maana huwa zinaonekana katika main page huku zikionyesha mchangiaji wa mwisho ni miezi mitatu iliyopita
Kipi cha maana ulichoandika? Katika aya tatu nilizo nukuu kipi cha maana msomaji amepata kutoka kwako.
Ni vizuri kuelewa hapa ni kijiweni, na ndio maana ya forums, hapa sio ScienceDirect, wala Elsevier au ResearchHub ambapo kila unachoandika kitatakiwa kuhakikiwa na kwa manufaa ya tafiti
Hapa ni kijiweni, kwa hiyo, hayo maandiko yako ni pumba zako ulizobumba kichwani, kwahiyo zinaweza kuwa ni pumba za uchochezi, chuki na unyanyapaa na zinazokubalika na kikundi kinachoendano na mrengo wako wa maoni, kwa hiyo usishangae unapokutana na na mtu mwenye mtazamo kama wangu wa kukuona ni mbuzi fulani unatapatapa


Ajira zinatolewa kwa kuangalia vyeti na sifa ya mhusika zikiwemo nywele.
Hapa nadhani tunajua, ni jinsi gani mnavyojitahidi kuhamisha magoli , wakati ukweli unaanzia kwenye mtaala mzima wa jinsi elimu inavyotolewa kwa upendeleo kwa jamii fulani, ambapo haya madai yemeshawahi kufika mpaka bungeni.
Lakini katika uajiri, ni kama Saidi anafanya mtihani wa form 4 kwenda elimu ya juu, ni sawa na Michael anatuma maombi ya kazi Azam TV
 
Na sina muda huo wa kupoteza kusoma pumba za hilo jukwaa maana huwa zinaonekana katika main page huku zikionyesha mchangiaji wa mwisho ni miezi mitatu iliyopita
Wewe unapoteza nini yakiwemo hata ya miezi 6! Lakini unapitia jambo zuri ndio maana unaghadhabika.
Nafahamu kinachokukera! lakini ukweli unabaki kuwa ukweli. Endelea kupitia kule ukiwa na fursa kama ulivyofanya na pole kwa kukereka.
OK! ni kijiweni. Ikiwa ni pumba zangu kipi kinakukera? Kwanini usiayaache kama Pumba ! ukaendelea na yako.
Hebu eleza chuki ipi au uchochezi upi ambao wewe huwezi kuujibu lakini unaweza kuutukana! ha ha.
Ni hivi kule Zanzibar tunakoongelea suala la Mapinduzi kuna tatizo. Kwamba, watu wanatambuana kwa rangi na nywele, hilo si geni. Kwani hukuwahi kusoma mabango yanayohusu machotara! Kwani hujawasikia Wanaopinga Mapinduzi! Hoja hapa ipo Zanzibar ndio maana nilikuwa najadiliana na Pasco kuhusu 'sensitivity' ya suala la Mapinduzi.

Ukileta hoja utasaidia wasomaji wa 'kijiweni' , lakini pia usisahau yule mzee aliniambia kila mtu ana hoja hata mwenye tusi, tofauti ni thamani ya hoja.
 
Kinaitwaje hiko kitabu kaka
 
Mapinduzi yalikuwa halala au haramu? Swali limekuwa gumu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…