Uchaguzi 2020 Mapingamizi halali kisheria dhidi ya mgombea nafasi ya Urais

MAPINGAMIZI HALALI KISHERIA DHIDI YA MGOMBEA NAFASI YA URAIS.

Wiki ijayo tarehe 26 August, 2020 itakuwa ni siku ya wagombea kuwasilisha mapingamizi dhidi ya wagombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mapingamizi halali kisheria anayoweza kuwekewa mgombea wa nafasi ya Urais kwa mujibu wa masharti ya ya Kifungu cha 35 D na 40 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 yakisomeka kwa pamoja na (read in tendem with) masharti ya Kanuni ya 39 (4) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 (Tangazo la Serikali Na. 402 la 2020) ni haya yafuatayo;

(1) Mgombea Urais sio raia wa Tanzania.

(2) Mgombea Urais hajafikisha umri wa miaka 40.

(3) Mgombea Urais hajui kusoma na kuandika Kiswahili au Kiingereza.

(4) Mgombea Urais sio mwanachama wa chama cha siasa.

(5) Mgombea Urais hajadhaminiwa na chama cha siasa kugombea.

(6) Mgombea Urais amekutwa na hatia ya kosa la jinai la kukwepa kodi katika kipindi cha miaka 5 kabla ya siku ya Uchaguzi.

(7) Mgombea Urais hajadhaminiwa na wapiga kura 200 kutoka mikoa 10 ya Tanzania ikiwemo mikoa 2 kutoka Zanzibar.

(8) Mgombea Urais hajadhaminiwa na idadi ya kutosha ya wapiga kura.

(9) Mgombea Urais hakulipa dhamana ya Tshs 1, 000, 000/=

(10) Mgombea Urais hakuwasilisha au hakuambatinisha picha kwenye Fomu ya Uteuzi.

(11) Mgombea Urais ameshindwa kuambatanisha Tangazo la Kisheria (statutory declaration) kwenye Fomu ya uteuzi ambalo limesainiwa na mgombea na limefanywa mbele ya Jaji kudhibitisha kuwa mgombea anayo nia na anazo sifa za kugombea Urais.

(12) Mgombea Urais ameshindwa kuweka wazi pesa ambazo atazitumia katika uchaguzi.

(13) Mgombea Urais hakusaini kukubali kutii Maadili ya Uchaguzi.

(14) Mgombea Urais hakujaza au hakurudisha Fomu ya Uteuzi kwa Tume ya Taifa Uchaguzi kwa mujibu wa matakwa ya sheria.

(15) Mgombea Urais amefanya makosa ambayo yamezuhiwa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi, 2010.

(16) Kutokana na taarifa ambazo ziko kwenye Fomu yake ya Uteuzi, mgombea hana sifa za kuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge au mjumbe wa baraza la wawakilishi la Zanzibar zilizoainishwa na Katiba husika.

(17) Taarifa ambazo mgombea Urais amewasilisha kwa Tume ya Taifa uchaguzi hazijitoshelezi kumtambua mgombea.

(18) Kutokana na taarifa ambazo ziko kwenye Fomu yake ya Uteuzi, hana sifa za kuwa mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizoainishwa na Katiba.

Haya ndo mapingamizi 18 pekee ambayo anaweza kuwekewa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sio vinginevyo.
Asant sana kwa post
 
Hapo namba 15 inaondoka na lisu.
Jiwe asijaribu kutuvuruga kupitia hiyo TUME YAKE YA MFUKONI, aache demokrasia ichukue mkondo wake ili tuchague Mgombea tumtakaye.

Wachumia tumbo kama wewe inabidi mkubaliane na hali halisi, Utawala wa Mkono wa Chuma sasa basi..
 
Mkuu jaribu Basi kuheshimu haki yangu ya kutoa maoni Kama ninavyoheshimu yako.
 
MATAGA,Lissu anaingia wapi hapo kwa hoja ya kufanya kampeni kabla ya wakati?

Umefanya jambo la maana sana kuleta hii habari.

Hapa pia anajiuliza,mtu huyu ambae hajapitishwa na Tume, anaitwaje mgombea uraisi?

Sasa kuna maana gani ya kumuwekea pingamizi mtu asigombea na hapo hapo tayari anatambulika/anatajwa kama mgombea?

Je,tumekosa msamiati wa kiswahili katika hili au mimi ndio sielewi?
Nenda kaisome hiyo sheria acha kusubiri lutafuniwa
 
Wiki ijayo tarehe 26 August, 2020 itakuwa ni siku ya wagombea kuwasilisha mapingamizi dhidi ya wagombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Shukrani mwanaJF hapa wana CCM Mpya watajifanya hawaelewi bandiko lako lililo sheheni facts kuliko zile za kufikirika za wanaLumumba kuombea kitu kisicho kuwapo.
 
MAPINGAMIZI HALALI KISHERIA DHIDI YA MGOMBEA NAFASI YA URAIS.

Wiki ijayo tarehe 26 August, 2020 itakuwa ni siku ya wagombea kuwasilisha mapingamizi dhidi ya wagombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mapingamizi halali kisheria anayoweza kuwekewa mgombea wa nafasi ya Urais kwa mujibu wa masharti ya ya Kifungu cha 35 D na 40 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 yakisomeka kwa pamoja na (read in tendem with) masharti ya Kanuni ya 39 (4) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 (Tangazo la Serikali Na. 402 la 2020) ni haya yafuatayo;

(1) Mgombea Urais sio raia wa Tanzania.

(2) Mgombea Urais hajafikisha umri wa miaka 40.

(3) Mgombea Urais hajui kusoma na kuandika Kiswahili au Kiingereza.

(4) Mgombea Urais sio mwanachama wa chama cha siasa.

(5) Mgombea Urais hajadhaminiwa na chama cha siasa kugombea.

(6) Mgombea Urais amekutwa na hatia ya kosa la jinai la kukwepa kodi katika kipindi cha miaka 5 kabla ya siku ya Uchaguzi.

(7) Mgombea Urais hajadhaminiwa na wapiga kura 200 kutoka mikoa 10 ya Tanzania ikiwemo mikoa 2 kutoka Zanzibar.

(8) Mgombea Urais hajadhaminiwa na idadi ya kutosha ya wapiga kura.

(9) Mgombea Urais hakulipa dhamana ya Tshs 1, 000, 000/=

(10) Mgombea Urais hakuwasilisha au hakuambatinisha picha kwenye Fomu ya Uteuzi.

(11) Mgombea Urais ameshindwa kuambatanisha Tangazo la Kisheria (statutory declaration) kwenye Fomu ya uteuzi ambalo limesainiwa na mgombea na limefanywa mbele ya Jaji kudhibitisha kuwa mgombea anayo nia na anazo sifa za kugombea Urais.

(12) Mgombea Urais ameshindwa kuweka wazi pesa ambazo atazitumia katika uchaguzi.

(13) Mgombea Urais hakusaini kukubali kutii Maadili ya Uchaguzi.

(14) Mgombea Urais hakujaza au hakurudisha Fomu ya Uteuzi kwa Tume ya Taifa Uchaguzi kwa mujibu wa matakwa ya sheria.

(15) Mgombea Urais amefanya makosa ambayo yamezuhiwa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi, 2010.

(16) Kutokana na taarifa ambazo ziko kwenye Fomu yake ya Uteuzi, mgombea hana sifa za kuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge au mjumbe wa baraza la wawakilishi la Zanzibar zilizoainishwa na Katiba husika.

(17) Taarifa ambazo mgombea Urais amewasilisha kwa Tume ya Taifa uchaguzi hazijitoshelezi kumtambua mgombea.

(18) Kutokana na taarifa ambazo ziko kwenye Fomu yake ya Uteuzi, hana sifa za kuwa mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizoainishwa na Katiba.

Haya ndo mapingamizi 18 pekee ambayo anaweza kuwekewa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sio vinginevyo.
Hivi kwanini anahofiwa sana mtu huyu? Najiuliza sipati majibu, unajua team nzima kuwa na hofu iliyopitiliza juu ya mtu fulani si jambo dogo
 
Kwenu Wana Lumumba,

Hakuna kitu kama hicho cha kuenguliwa, Tundu Lissu lazima agombee.

Mlisema hatakuja, kaja toka Belgium.

Mlisema msaliti hana mvuto wa kisiasa, imebainika siyo kweli.

Mlisema siku ya Sikukuu ya Nane Nane Ofisi ya Tume ya Uchaguzi Dodoma itakuwa imefungwa, Tundu Lissu alikuta ipo wazi.

Mlisema hati yake ya Kiapo haitasainiwa na Jaji wa Mahakama Kuu Dar es Salaam , jana fomu zake za kiapo zimesainiwa.

Mmepanga kumuita Kisutu tarehe 26 August 2020, Tundu Lissu hawezi kutokea kwa udhuru wa jambo muhimu ktk mchakato wa kuelekea uchaguzi 2020.

Mnasema tarehe 26 August 2020 hatatambuliwa kama mgombea rasmi wa Urais kupitia CHADEMA 2020, Tundu Lissu atatambuliwa na Tume ya Uchaguzi ya Taifa na ndiyo itakuwa siku ya kusitisha tuhuma zote za mahakamani mpaka baada ya uchaguzi tarehe 28 Oktoba kumalizika.

Wagombea wanaotambuliwa na Tume ya Uchaguzi 26 Agosti tuhuma za mashtaka yao yatasitishwa kwa kinga maalum ili sisi waTanzania tuweze kushiriki kumpigia kura maana tuhuma ya kesi siyo kigezo cha kumuondolea haki yake kuchaguliwa kwani tuhuma siyo ukweli mpaka pale tu atakapo hukumiwa ndiyo sifa inakosekana
 
Ni kazi ya Bunge kupitia constituent assembly wafanyie marekebisho katiba na kufuta ibara inayotoa hilo sharti.
Mbona tulishamaliza kote huko na Tume ya Katiba ya Jaji Warioba. Matokeo yakazimwa.

Tume ya Jaji Nyalali ilipofanya mjadala na mchakato kuhusu vyama vingi ikieleza hili kwa bayana. Mgombea huru aruhusiwe. Nyerere akasema hivyo hivyo.

CCM ndio hawataki.
 
Bahati mbaya hata rasimu ya katiba mpya haikuondoa hicho kigezo!

Hivyo, hata katiba mpya, kama ingepita, huenda ingekuwa tu sawa sawa na ya sasa.

Mahakama ya Afrika, katika shauri lililofunguliwa kuhusu mgombea binafsi, ilisema wazi wazi kwamba ni swala lililo kinyume na Katiba!

Ubaya ni kwamba, katiba haiwezi kuwa kinyume na katiba yenyewe kwa yenyewe!

Tulishafungua mashauri mengi mahakama kuu kuhusu hili ikashindikana! Mahakama ilisema wazi kwamba, "THE CONSTITUTION CAN NOT BE UNCONSTITUTIONAL". (na ni kweli wako sahihi)

Hata Mahakama ya Afrika nayo ilitoa ruling ambayo haitekelezeki.

Tunahitaji katiba mpya, itakayorekebisha rasimu ya katiba mpya.
Can the constitution contradict itself?

Umenikumbusha historia moja.

Siku Albert Einstein alivyokuwa anaapishwa kuwa raia wa Marekani, alimchukua rafiki yake kipanga wa logic Kurt Godel. Aende kuwa shahidi wa kiapo cha Einstein kuwa raia wa Marekani.

Basi wakatoka zao Princeton University mpaka makao makuu ya serikali ya New Jersey hapo Trenton kwa jaji iki E8nstein aapishwe.

Einstein akawa anataka kuapishwa kwa kutumia katiba ya Marekani.

Basi hapo hapo Kurt Godel akaanza kichaa chake kuanza kuchambua logic ya katiba ya Marekani.

Godel akamwambia Einstein, unajua hiyo katiba unayoitumia kuapa haifai na ina ma contradictions haya na haya na haya.

Einstein akamwambia Godel hebu acha uchizi wako. Mimi leo kazi yangu mija tu. Kula kiapo niwe raia wa Marekani. Ukianza kuleta stories za contradictions kwenye katiba mbele ya Jaji naweza kunyimwa uraia buree.

So. This shows. The constitution can be self contradicting.

And when this happens, the contradictions need to be resolved.
 
Bahati mbaya hata rasimu ya katiba mpya haikuondoa hicho kigezo!

Hivyo, hata katiba mpya, kama ingepita, huenda ingekuwa tu sawa sawa na ya sasa.

Mahakama ya Afrika, katika shauri lililofunguliwa kuhusu mgombea binafsi, ilisema wazi wazi kwamba ni swala lililo kinyume na Katiba!

Ubaya ni kwamba, katiba haiwezi kuwa kinyume na katiba yenyewe kwa yenyewe!

Tulishafungua mashauri mengi mahakama kuu kuhusu hili ikashindikana! Mahakama ilisema wazi kwamba, "THE CONSTITUTION CAN NOT BE UNCONSTITUTIONAL". (na ni kweli wako sahihi)

Hata Mahakama ya Afrika nayo ilitoa ruling ambayo haitekelezeki.

Tunahitaji katiba mpya, itakayorekebisha rasimu ya katiba mpya.
Can the constitution contradict itself?

Umenikumbusha historia moja.

Siku Albert Einstein alivyokuwa anaapishwa kuwa raia wa Marekani, alimchukua rafiki yake kipanga wa logic Kurt Godel. Aende kuwa shahidi wa kiapo cha Einstein kuwa raia wa Marekani.

Basi wakatoka zao Princeton University mpaka makao makuu ya serikali ya New Jersey hapo Trenton kwa jaji ili Einstein aapishwe.

Einstein akawa anataka kuapishwa kwa kutumia katiba ya Marekani.

Basi hapo hapo Kurt Godel akaanza kichaa chake kuanza kuchambua logic ya katiba ya Marekani.

Godel akamwambia Einstein, unajua hiyo katiba unayoitumia kuapa haifai na ina ma contradictions haya na haya na haya.

Einstein akamwambia Godel hebu acha uchizi wako. Mimi leo kazi yangu moja tu. Kula kiapo niwe raia wa Marekani. Ukianza kuleta stories za contradictions kwenye katiba mbele ya Jaji naweza kunyimwa uraia buree.

Mtikila alijaribu mara 3 kupigania haki ya Mgombea binafsi mahakamani lakini mwishowe alishindwa kesi . Mtikala alishinda kesi katika Mahakama Kuu mara 2 yaani mwaka 1993 kwa Jaji Lugakingira na 2006 kwa majaji watatu (3) wakina Mihayo na wenzake, hatahivyo, alishindwa Mahakama ya Rufaa katika kesi ya Attorney General Vs Mtikila, Civil Appeal No. 45 of 2019.

Ni kwa sababu wale wazee ni wanasiasa wanaoamua mambo ya kisheria, hivyo wao ndio the last line of defence ya watawala kimakakama.
 
The constitution can be self contradicting.

And when this happens, the contradictions need to be resolved.
 
Mtikila alijaribu mara 3 kupigania haki ya Mgombea binafsi mahakamani lakini mwishowe alishindwa kesi . Mtikala alishinda kesi katika Mahakama Kuu mara 2 yaani mwaka 1993 kwa Jaji Lugakingira na 2006 kwa majaji watatu (3) wakina Mihayo na wenzake, hatahivyo, alishindwa Mahakama ya Rufaa katika kesi ya Attorney General Vs Mtikila, Civil Appeal No. 45 of 2019.
Hii ni issue ya common sense tu.

Hatutakiwi kusema Watanzania wote wa majority age na sane mind wana haki ya kupiga na kupigiwa kura, halafu tulaweka vizingiti zaidi vinavyoondoa haki hiyo, kama sharti la mgombea kuwa na chama.

Sasa kama mtu haoni chama kinachomfaa na hataki habari za vyama, haki yake ya kikatiba ya kugombea uongozi qnyimwe kwa sababu hana/ hataki chama?
 
Sikiliza, kiazi! Kifungu tajwa kinahusiana na “gharama”. Kuna jambo gani linalohusu gharama ambalo litambana Lissu??
Hapo hakijatajwa kifungu Bali Sheria ,

Ifahamu kwanza hiyo Sheria ndio urudi kunikosoa tena.
 
Mahakama ya Kikatiba ya Afrika Kusini mwezi Juni mwaka huu ilibatilisha sheria inayozuhia wagombea binafsi katika kesi New Nation Movement NPC and Others v President of the Republic of South Africa and Others[ 2020] ZACC 11, hivyo, wagombea binafsi wanaruhusiwa kushiriki uchaguzi nchini Afrika Kusini.
Sisi tunaendeshwa na CCM. Hatufuatilii haki.
 
MATAGA,Lissu anaingia wapi hapo kwa hoja ya kufanya kampeni kabla ya wakati?

Umefanya jambo la maana sana kuleta hii habari.

Hapa pia anajiuliza,mtu huyu ambae hajapitishwa na Tume, anaitwaje mgombea uraisi?

Sasa kuna maana gani ya kumuwekea pingamizi mtu asigombea na hapo hapo tayari anatambulika/anatajwa kama mgombea?

Je,tumekosa msamiati wa kiswahili katika hili au mimi ndio sielewi?
Kutokukaa miaka 3 mfululizo nchini Tz!
 
Kweli ka
Na hii inasababisha wagombea wenye vipaji vya uongozi ktk jamii husika kukoswa nafasi ya kugombea kwa sbb ya ukilitimba uliomo ndani ya vyama vya siasa vyote.
Rasimu ya katiba ya jaji Warioba inapendekeza kuwe na mgombea binafsi pia.

Kweli kabisa.
 
MAPINGAMIZI HALALI KISHERIA DHIDI YA MGOMBEA NAFASI YA URAIS.

Wiki ijayo tarehe 26 August, 2020 itakuwa ni siku ya wagombea kuwasilisha mapingamizi dhidi ya wagombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mapingamizi halali kisheria anayoweza kuwekewa mgombea wa nafasi ya Urais kwa mujibu wa masharti ya ya Kifungu cha 35 D na 40 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 yakisomeka kwa pamoja na (read in tendem with) masharti ya Kanuni ya 39 (4) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 (Tangazo la Serikali Na. 402 la 2020) ni haya yafuatayo;

(1) Mgombea Urais sio raia wa Tanzania.

(2) Mgombea Urais hajafikisha umri wa miaka 40.

(3) Mgombea Urais hajui kusoma na kuandika Kiswahili au Kiingereza.

(4) Mgombea Urais sio mwanachama wa chama cha siasa.

(5) Mgombea Urais hajadhaminiwa na chama cha siasa kugombea.

(6) Mgombea Urais amekutwa na hatia ya kosa la jinai la kukwepa kodi katika kipindi cha miaka 5 kabla ya siku ya Uchaguzi.

(7) Mgombea Urais hajadhaminiwa na wapiga kura 200 kutoka mikoa 10 ya Tanzania ikiwemo mikoa 2 kutoka Zanzibar.

(8) Mgombea Urais hajadhaminiwa na idadi ya kutosha ya wapiga kura.

(9) Mgombea Urais hakulipa dhamana ya Tshs 1, 000, 000/=

(10) Mgombea Urais hakuwasilisha au hakuambatinisha picha kwenye Fomu ya Uteuzi.

(11) Mgombea Urais ameshindwa kuambatanisha Tangazo la Kisheria (statutory declaration) kwenye Fomu ya uteuzi ambalo limesainiwa na mgombea na limefanywa mbele ya Jaji kudhibitisha kuwa mgombea anayo nia na anazo sifa za kugombea Urais.

(12) Mgombea Urais ameshindwa kuweka wazi pesa ambazo atazitumia katika uchaguzi.

(13) Mgombea Urais hakusaini kukubali kutii Maadili ya Uchaguzi.

(14) Mgombea Urais hakujaza au hakurudisha Fomu ya Uteuzi kwa Tume ya Taifa Uchaguzi kwa mujibu wa matakwa ya sheria.

(15) Mgombea Urais amefanya makosa ambayo yamezuhiwa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi, 2010.

(16) Kutokana na taarifa ambazo ziko kwenye Fomu yake ya Uteuzi, mgombea hana sifa za kuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge au mjumbe wa baraza la wawakilishi la Zanzibar zilizoainishwa na Katiba husika.

(17) Taarifa ambazo mgombea Urais amewasilisha kwa Tume ya Taifa uchaguzi hazijitoshelezi kumtambua mgombea.

(18) Kutokana na taarifa ambazo ziko kwenye Fomu yake ya Uteuzi, hana sifa za kuwa mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizoainishwa na Katiba.

Haya ndo mapingamizi 18 pekee ambayo anaweza kuwekewa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sio vinginevyo.

Great post Matojo Cosatta
 
Back
Top Bottom