Uchaguzi 2020 Mapingamizi halali kisheria dhidi ya mgombea nafasi ya Urais

Uchaguzi 2020 Mapingamizi halali kisheria dhidi ya mgombea nafasi ya Urais

Yaani CCM nawahurumia sana

Na mwaka huu tume haitakubali kuwabeba upepo ukiwa mbaya yaani mtapata tabu Sana

Lissu atapitishwa tena mapema Sana hakuna mtu ambaye haipendi Tanzania ambaye atakubali ujinga kuchafua nchi.

Sio tume sio watu wa usalama mwaka huu watu wanasimama na umma.
Dawa ya msaliti ni tarehe 28/10/2020!
 
Tanzania itaingia kwenye machafuko ambayo hayajawahi toke tangu dunia imeumbwa
Usichukulie machafuko kama kitu kidogo, waulize Lyibia wanatamani enzi za Gaddafi zirude, halafu vijana mnashabikia, hata hiyo mitandao ya kijamii ambayo mnachat nayo mtaisikia kwenye radio.
 
Kuanza Kampeini mapema (pre-mature election campaign) sio kosa chini ya sheria za uchaguzi za Tanzania. Kuanza Kampeini mapema hakumuondolei mtu sifa za kugombea Urais katika Sheria za Uchaguzi za Tanzania.

Kuanza Kampeini mapema ni kosa chini ya sheria za ndani za CCM lakini sio kwenye sheria za nchi.

Hivi mbona mnatapatapa sana, nani kasema kuwa kuna mgombea atakatwa?
 
MAPINGAMIZI HALALI KISHERIA DHIDI YA MGOMBEA NAFASI YA URAIS.

Wiki ijayo tarehe 26 August, 2020 itakuwa ni siku ya wagombea kuwasilisha mapingamizi dhidi ya wagombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mapingamizi halali kisheria anayoweza kuwekewa mgombea wa nafasi ya Urais kwa mujibu wa masharti ya ya Kifungu cha 35 D na 40 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 yakisomeka kwa pamoja na (read in tendem with) masharti ya Kanuni ya 39 (4) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 (Tangazo la Serikali Na. 402 la 2020) ni haya yafuatayo;

(1) Mgombea Urais sio raia wa Tanzania.

(2) Mgombea Urais hajafikisha umri wa miaka 40.

(3) Mgombea Urais hajui kusoma na kuandika Kiswahili au Kiingereza.

(4) Mgombea Urais sio mwanachama wa chama cha siasa.

(5) Mgombea Urais hajadhaminiwa na chama cha siasa kugombea.

(6) Mgombea Urais amekutwa na hatia ya kosa la jinai la kukwepa kodi katika kipindi cha miaka 5 kabla ya siku ya Uchaguzi.

(7) Mgombea Urais hajadhaminiwa na wapiga kura 200 kutoka mikoa 10 ya Tanzania ikiwemo mikoa 2 kutoka Zanzibar.

(8) Mgombea Urais hajadhaminiwa na idadi ya kutosha ya wapiga kura.

(9) Mgombea Urais hakulipa dhamana ya Tshs 1, 000, 000/=

(10) Mgombea Urais hakuwasilisha au hakuambatinisha picha kwenye Fomu ya Uteuzi.

(11) Mgombea Urais ameshindwa kuambatanisha Tangazo la Kisheria (statutory declaration) kwenye Fomu ya uteuzi ambalo limesainiwa na mgombea na limefanywa mbele ya Jaji kudhibitisha kuwa mgombea anayo nia na anazo sifa za kugombea Urais.

(12) Mgombea Urais ameshindwa kuweka wazi pesa ambazo atazitumia katika uchaguzi.

(13) Mgombea Urais hakusaini kukubali kutii Maadili ya Uchaguzi.

(14) Mgombea Urais hakujaza au hakurudisha Fomu ya Uteuzi kwa Tume ya Taifa Uchaguzi kwa mujibu wa matakwa ya sheria.

(15) Mgombea Urais amefanya makosa ambayo yamezuhiwa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi, 2010.

(16) Kutokana na taarifa ambazo ziko kwenye Fomu yake ya Uteuzi, mgombea hana sifa za kuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge au mjumbe wa baraza la wawakilishi la Zanzibar zilizoainishwa na Katiba husika.

(17) Taarifa ambazo mgombea Urais amewasilisha kwa Tume ya Taifa uchaguzi hazijitoshelezi kumtambua mgombea.

(18) Kutokana na taarifa ambazo ziko kwenye Fomu yake ya Uteuzi, hana sifa za kuwa mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizoainishwa na Katiba.

Haya ndo mapingamizi 18 pekee ambayo anaweza kuwekewa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sio vinginevyo.

Mnaanzisha mada kisha mnajijibu wenyewe. Hii dhana ya mgombea fulani kukatwa mmeanzisha wenyewe na mnajijibu wenyewe. Siyo tume wala chama hawajawahi kusoma lolote. Hakika kuna tatizo kubwa kiongozi/ katikati yenu.
 
Usichukulie machafuko kama kitu kidogo, waulize Lyibia wanatamani enzi za Gaddafi zirude, halafu vijana mnashabikia, hata hiyo mitandao ya kijamii ambayo mnachat nayo mtaisikia kwenye radio.

Yote inafungwa hata simu pia. Juzi Ethiopia wamemaliza wiki tatu bila internet wala simu kisa kuuawa kwa mwanamziki maarufu.
 
Mnaanzisha mada kisha mnajijibu wenyewe. Hii dhana ya mgombea fulani kukatwa mmeanzisha wenyewe na mnajijibu wenyewe. Siyo tume wala chama hawajawahi kusoma lolote. Hakika kuna tatizo kubwa kiongozi/ katikati yenu.
Aisee!!!
 
namtania tu kuwa list ya mapingamizi hakuna linalomgusa Lisu!

Hakuna pingamizi lolote ambalo kisheria linamgusa Lissu labda lile linalohusu kukosea kujaza fomu ambapo ni vigumu sana Lissu kukosea kujaza fomu za uteuzi.
 
Hakuna pingamizi lolote ambalo kisheria linamgusa Lissu labda lile linalohusu kukosea kujaza fomu ambapo ni vigumu sana Lissu kukosea kujaza fomu za uteuzi.
Nasikia wamemuweka katika chumba akisubiria. Let us wait and see itakuwaje. Lkn niko convinced kuwa watamwekea mapingamizi ya kijinga kumzuia asigombee
 
Wanamchomesha mahindi huko[emoji2][emoji2][emoji119][emoji119], CHADEMA mjiandae kisaikolojia[emoji2][emoji2].
 
Leo ndo leo, tunasubili mapingamizi kutoka all sides of political divides.
 
MATAGA,Lissu anaingia wapi hapo kwa hoja ya kufanya kampeni kabla ya wakati?

Umefanya jambo la maana sana kuleta hii habari.

Hapa pia anajiuliza,mtu huyu ambae hajapitishwa na Tume, anaitwaje mgombea uraisi?

Sasa kuna maana gani ya kumuwekea pingamizi mtu asigombea na hapo hapo tayari anatambulika/anatajwa kama mgombea?

Je,tumekosa msamiati wa kiswahili katika hili au mimi ndio sielewi?
Uwe unasoma unaelewa kilichoandikwa-
Pingamizi linwekwa kwa mtu aliyechukua na kuwakilisha fomu zake Tume baada ya KUDHANI amekidhi vigezo vyote na kuteuliwa na Tume;
Mmoja ya walioteuliwa na Tume akiwa na taarifa za kukiuka matakwa ya sheria ambazo ndizo mtoa mada ameyataja- NDO inaitwa pingamizi.
 
Back
Top Bottom