Mapishi ya Chapati: Jikoni kwa Evelyn Salt & Mentor

Mapishi ya Chapati: Jikoni kwa Evelyn Salt & Mentor

Chapati zangu za maji ya baridi hizo
4e9e9567c2a01a0132a377d2d6c5b7ff.jpg
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] bravo bibi, bora umekuja ww maana kila nikimwambia mimi naona haelewi Mentor Njoo uchukue mawaidha kwa mkongwe

Nnampa darsa anasema eti "wivu".

Hahaha wivu kwa hivyo vifunga tumbo alivyovitengeneza.

Kwetu chapati nene kama hizo za Mentor huwapikia wenye tumbo la kuhara, zinasaidia sana tena sana.
 
Jifunze um-surprise my-husband-wako.

Mhh! Walisema kipimo cha mke bora basi ni mapishi yake ya chapati, sasa kama hujui kupika kabisa...sijuiiii!!!
Khaaah jamani hicho kipimo kiliwekwa na nani??
 
Nnampa darsa anasema eti "wivu".

Hahaha wivu kwa hivyo vifunga tumbo alivyovitengeneza.

Kwetu chapati nene kama hizo za Mentor huwapikia wenye tumbo la kuhara, zinasaidia sana tena sana.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji121] [emoji121] [emoji121] Basi muache bibi ameshakiri ndo mara yake ya kwanza kupika kidogo mwanzo si mbaya ni makosa madogo madogo tu hajayaweka sawa
 
nit
Salaam!

Tangu kuzaliwa kwangu nimeshapika vyakula vingi. Hata hivyo (nadhani kwa kutokana na kuzaliwa wa kiume) sikuwahi kupika chapati. Niliaminishwa mapishi ya chapati yana utaalamu ambao ni binti wa kike, tena waliofundwa vyema, wenye kuuweza.

Na ninakiri, ukimpata binti anayejua kupika chapati laini zenye layers zinazoonekana, basi huyo muoe hahah.

Anyway, leo nilimuomba mke wangu Evelyn Salt anifundishe mapishi ya chapati. Na huu ni mrejesho wa mapishi yenyewe. Nathibitisha kuwa hajagusa chochote, nimepika kila kitu kutoka mwanzo hadi mwisho, ila maelekezo yote niliyapata kwake. Muda wote alikuwa pembeni akinywa wine...

View attachment 455408

1. Kama kawaida yetu tunaandaa mahitaji yote na kuyaweka mezani kabla ya kuanza mapishi. Hii inakuhakikishia kuwa una kila unachokihitaji kabla hujaanza. Isijetokea ukahitaji mafuta kumbe huna na ulishaanza kupika/kuandaa.

Mahitaji:
Unga wa ngano (au kwa nchi za wenzetu wanatumia all-purpose flour), mafuta ya kupikia, chumvi, sukari, maji, bakuli, frying pan (kiswahili?), kikombe na kijiko cha kupimia, brush ya kupakia mafuta, mikono misafi, kibao/meza safi ya kukandia na kile kimbao cha kukandia (sifahamu jinale sanifu).

View attachment 455409

JINSI YA KUANDAA:

2 (a). Anza kwa kutia vijiko vinne vya mafuta ya kupikia kwenye sufuria na kuyapasha moto

2 (b). Kisha pasha maji yako kuwa ya vuguvugu

3. Pima vikombe viwili vya unga kwenye bakuli.

4. Ongeza kijiko kimoja cha chai cha chumvi

5. Ongeza 'pinch' (yaani chukua kwa vidole viwili) ya sukari

6. koroga pamoja mchanganyiko wako kuhakikisha chumvi na sukari vimechanyangika vyema na unga wako.

View attachment 455412

7. Ongeza mafuta yako (vijiko vinne vya mafuta ya kupikia ulivyokwisha kuvichemsha 2 (a)) Kisha uendelee kuuchanganya mchanganyiko wako. Sasa unaweza kutumia mikono kuchanganya mchanganyiko wako. Fanya hivyo kwa dakika mbili hadi tatu. Jitahidi kuhakikisha sehemu kubwa ya unga imeshika mafuta. (mchanganyiko wako utakuwa na vibonge bonge, usihofu)

View attachment 455411

8. Ongeza robo tatu ya kikombe cha maji yale ya vuguvugu (hatua 2 (b)) na kisha uanze kuukanda unga wako. Dakika moja ya mwanzo unaweza kukata tamaa maana unga wako utashikana sana na mikono na chombo chako, usihofu.

9. Ongeza unga kidogo kidogo huku ukiendelea kuukanda unga wako. (kipimo cha kidogo kidogo ni kuchukua unga kwa vidole vyako vyote vitano - vidole, sio mkono). Kwa njia hii hutajikuta umepitiliza kuweka unga mwingi. Endelea kufanya hivi kwa dakika si chini ya tano. Baada ya hapa, unga wako utakuwa umeachana na sufuria na mkono wako.

10. Toa unga wako kutoka kwenye bakuli na uuweke juu ya meza yako safi au tumia kibao cha kukandia (hakikisha usafi wa eneo utakalofanyia kazi). Nyunyiza unga juu ya eneo hilo kisha endelea kuukanda unga wako. Endelea kukanda huku ukinyunyiza unga kila wakati. Fanya hivi kwa dakika zisizopungua 15. Kuwa mwaminifu kwako mwenyewe wakati wa kukanda usifanye tu ili kumaliza dakika 15, ila hakikisha unaukanda vyema.

11. unda mpira/tufe wa mchanganyiko wako na kisha utie ndani ya bakuli lako uliloanzia nalo kuchanganyia.

12. Kwa kutumia brashi yako, paka sehemu ya juu ya tufe lako mafuta kiasi, kisha funika bakuli lako kwa kitu chochote ambacho hakitaruhusu kupitisha hewa. Acha kwa dakika zisizopungua 30.

View attachment 455415

View attachment 455416

13. Baada ya dakika thelathini, toa tufe lako na uligawe katika vitufe vidogo vinne (kutokana na vipimo tulivyotumia).

14. tengeneza mduara kama unataka kupika chapati tayari. kisha upake mafuta kwa kutumia brashi yako. Mafuta kiasi tu.

View attachment 455419

15. Kisha zungurusha kama unatengeneza kijiti (pipe). Baada ya hapo zungurusha tena 'pipe' yako katika mduara kisha kile kisehemu cha mwisho kichomeke chini ya mduara wako kama inavyoonekana kwenye picha ya chini.

View attachment 455420

16. Funika tena na uviache kwa dakika zisizozidi 15.

17. Baada ya hapo tengeneza vitufe vyako kama chapati tayari kwa kupika. (muda wote unapotengeneza chapati zako hakikisha unanyunyizia unga kwenye meza/ubao wako).

18. Tengeneza chapati zako (hakikisha ile iliyokuwa ya kwanza kutengenezwa kwenye namba 15 ndiyo inaanza kutengenezwa/kupikwa) tayari kwa kupika. Jitahidi kutengeneza kuwa mduara.

View attachment 455421

19. Tia frying pan yako kwenye jiko na hakikisha moto wako sio mkubwa (uwe wa wastani, sawa na namba tano kwenye jiko la umeme). Hakikisha pan yako ni kavu na haina mafuta wala majimaji.

View attachment 455422
20. Acha kwa dakika moja kisha geuza chapati yako, ichome kwa dakika moja kisha kwa kutumia brashi yako paka mafuta kwenye sehemu ya juu. Geuza chapat yako na upake tena mafuta sehemu iliyopo juu. Subiri kwa dakika moja kisha geuza tena kwa dakika moja na utoe chapati yako tayari kwa kuliwa.

View attachment 455423

21. Hakikisha unasafisha jiko lako baada ya kupika.

View attachment 455417

Wasalaam wapendwa,
Mentor & Evelyn Salt.
nitajaribu na mimi nione.
 
Mkuu matayarisho mpaka kula si itakuchukua masaa kadhaa chapati zenyewe nne tu c bora nipike za maji
 
Huyo bwana simwamini naweza jitahidi akanisema cjazipika vzr ntaita jirani aonje

Basi nitakuja mwenyewe kuonja...ukipika niite mimi shemeji!

Mimi nimejaa tele hata sijafichwa mpendwa. Amen na kwako pia

Sikubaliani na hili!

Ila nafurahi kuona u mzima wa afya...barakaz kwako!!

[emoji23] [emoji23] [emoji23] bravo bibi, bora umekuja ww maana kila nikimwambia mimi naona haelewi Mentor Njoo uchukue mawaidha kwa mkongwe

Huyo bibi ana wivu tu!

Muulize yeye siku ya kwanza kupika chapati zilikuwaje.

Na sijasema nina maksi 100 ila kwa kila category aliyotaja nina maksi (siyo 0).
 
Chapati zangu za maji ya baridi hizo
bc09dccf068b0c6f7d314ce7be928e7b.jpg
972dd08051e60ef0507afec2bd3733dd.jpg
83983450320ebd9b11e28fda394937e9.jpg
65356a065ee58b93c7f382ac8e8c624a.jpg

Wow! ipyax hizo zimekaa poa..especially ulivobalance kuiva kwake.

Sema sasa wakija hapa FaizaFoxy na johnson godfrey watasema ooh mduara sio 360, mara haina layer mara sijui ni kifunga tumbo...

Khaaah jamani hicho kipimo kiliwekwa na nani??

Wahenga!

nit

nitajaribu na mimi nione.

Way to go brother...utupe mrejesho!

Mkuu matayarisho mpaka kula si itakuchukua masaa kadhaa chapati zenyewe nne tu c bora nipike za maji

Maximum masaa mawili na izo nne ni kwa sababu familia yangu bado ndogo mkuu ila ni around the same time labda kama wapikia sherehe.
 
Wow! ipyax hizo zimekaa poa..especially ulivobalance kuiva kwake.

Sema sasa wakija hapa FaizaFoxy na johnson godfrey watasema ooh mduara sio 360, mara haina layer mara sijui ni kifunga tumbo...

Wahenga!

Way to go brother...utupe mrejesho!

Maximum masaa mawili na izo nne ni kwa sababu familia yangu bado ndogo mkuu ila ni around the same time labda kama wapikia sherehe.

Yaani hao wahenga wako inabidi watumbuliwe.
 
Basi nitakuja mwenyewe kuonja...ukipika niite mimi shemeji!

Sikubaliani na hili!

Ila nafurahi kuona u mzima wa afya...barakaz kwako!!

Huyo bibi ana wivu tu!

Muulize yeye siku ya kwanza kupika chapati zilikuwaje.

Na sijasema nina maksi 100 ila kwa kila category aliyotaja nina maksi (siyo 0).

Kwakweli mdogo wangu umejitahidi, japo ulininyima kuonja.
 
Nimegundua mapishi ya chapati ni mengi. Ila hii niliyoweka ni niliyoifanyia kazi mwenyewe, kwa mikono yangu, inatoa chapati nne na ukitaka ziwe nyembamba basi zitatoka sita.

Ni laini, na inakunjika vyema ingawa si laini kama chapati za kumimina.
Uko vizuri sana hongera kwa jitihada na usafi pia nimekupa credit. Next time jaribu kukandia maji baridi pia ukichekecha unga kabla ni vizuri zaidi. Cheers
 
Nnampa darsa anasema eti "wivu".

Hahaha wivu kwa hivyo vifunga tumbo alivyovitengeneza.

Kwetu chapati nene kama hizo za Mentor huwapikia wenye tumbo la kuhara, zinasaidia sana tena sana.
Hahahahaha lakini amejitahidi jamani pishi lake la kwanza na ni mwanaume.
 
Uko vizuri sana hongera kwa jitihada na usafi pia nimekupa credit. Next time jaribu kukandia maji baridi pia ukichekecha unga kabla ni vizuri zaidi. Cheers

Popote ulipo my dear agiza kinywaji ukipendacho nitumie bill...nitalipa! Thank you for appreciating...

Hahahahaha lakini amejitahidi jamani pishi lake la kwanza na ni mwanaume.
 
Chapati zimenipitia kushoto kwanzia kula mpaka uandaaji.... Nikila naishia nusu tu

Hongera kwa hatua hiyo Mentor
 
Umejitahidi sana mentor...

Naamini next time utafanya vizuri zaidi.

Pia samli ni nzuri kwa kukandia chapati,unaipasha vizuri unakandia na kuviringishia badala ya mafuta ya kawaida. Pia wakati wa kuichoma uwe unaikandamiza kwenye frying pan na kijiko ili hiyo iwe brownish ienee zaidi.

Hongera.
 
Pika basi chapati nije kula.
 
Back
Top Bottom