Mapishi ya nazi ni overrated sana kwa vyakula vingi

Mapishi ya nazi ni overrated sana kwa vyakula vingi

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Samaki, dagaa na maharage vikiwekwa nazi huwa vyakula vizuri vinavyovyutia kula na ladha ya kueleweka. Nazi kwenye vyakula vingine vingi huwa naona overrated sana.

Sijui ni nini hasa huwa kinawafanya watu watokwe na udenda au kusifia sana wali nazi, nyama nazi, bamia nazi, kisamvu nazi, tambi nazi, pilau nazi, n.k
 
zamani tuliwaonya wake zetu kwa moja ya kibao cha supu ikitia nazi umeharibu ladhaaa

hii ilikua kuwaonya si kila pishi wao ni nazi tuh
 
Umezaliwa mkoa wa mara nini? Wale jamaa hawana mbwembwe kwenye mapishi hata samaki huwa hawaoshi vizuri wanachemsha na nyanya nzima na maganda yake ukimaliza kula unanuka shombo ya samaki hata wiki 3
 
Mi nazi kiujumla siielewi kwenye chochote
 
Umezaliwa mkoa wa mara nini? Wale jamaa hawana mbwembwe kwenye mapishi hata samaki huwa hawaoshi vizuri wanachemsha na nyanya nzima na maganda yake ukimaliza kula unanuka shombo ya samaki hata wiki 3
Kumenya nyanya ni ujuha mwingine tu.
 
Kuna wanawake wanajua kuitumia NAZI..

PIA kuna SIRI ktk upishi wa kutumia NAZI kuanzia inavyokunwa ktk kibao.. mpk kupikwa kwake..

Wajuvi wataongezea..
 
Back
Top Bottom