Mapishi ya nazi ni overrated sana kwa vyakula vingi

Mkuu wali nazi 25 ,kisamvu nazi tatu ,pilau nazi+nyanya ni hatari mkuu.

Maharage mabichi +nazi ni hatari mkuu.
 
Nadhani imekaa kiurithi wa kitamaduni zaidi..
1. Mimi mawese mekundu nasikia harufu muda wote! Kigoma na makabila ya huko kwao ni murua
2. Mimi chakula kilichopikiwa tui ya karanga siwezi gusa kabisa!
3. Olive oil sijawahi ielewa!
4. Cheese and butter ni uchafu
5. Kuunga maziwa kwenye chakula chochote ni wendawazimu!
6. Nazi naikubali kwenye mboga za majani na ubwabwa tu!
 
Utakuwa hujaonja Chai nazi wewe
 
utamu wa pishi la nazi inategemeana na aina ya mpishi maana kila mtu ana ufundi wake hasa wakati wa kufanya mixing.. tatizo ni la mkeo anakutolea boko alimradi tu kapika kiasi huoni maajabu ww mkoromee huyo mkeo anaekuingiza chaka ila acha kabisa kukashifu pishi la nazi
 
Unaonekana una kanyalo na wanaume kama wewe inataka uvumilivu kuishi nanyi mna vimasharti vingi vingi mpaka mnaboa
 
Huyo hana masharti mbona, mimi Mwanamke akipika chakula huku amevaa nguo atakula peke yake nakuambia
Hee ndo mizimu ya kwenu inataka hivyo? Huko kagera miaka hiyo ilikuwa mwanamke huruhusiwi kumenya ndizi ukiwa umekaa kuchuchumaa(kutandama) mume akikufuma chakula hali inabidi zitafutwe ndizi nyingine, ni ukae ufunge miguu ndipo umenye na hairuhusiwi kuongea utatemea chakula, mara kufunga nguo kichwani wakati wa kumenya au kupika hairuhusiwi saiv hotel zote ni sharti kufunga kichwa nywele zisidondokee kwenye chakula,,, kusalimia na kitambaa kichwani haitakiwi visheria ushuzi tu sasa ndiye wewe
 
Ndio hivyo, yaani Mke umuoe kabisa kwa mahari halafu eti anavaa sijui kanga sijui kitenge wakati wa kupika...Dharau gani hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…