Mapishi ya Ndizi Utumbo

Mapishi ya Ndizi Utumbo

farkhina

Platinum Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
14,568
Reaction score
16,917
Mahitaji

  • Utumbo wa ng'ombe kg 1

  • Ndizi mbichi chana 2 ukubwa kiasi (ndizi 16-20)
  • Nyanya 3 kubwa
  • Kitunguu 1 kikubwa
  • Ndimu 2
  • Pilipili manga 1/2 kijiko cha chai
  • Tangawizi iliosagwa na saumu kijiko kimoja cha chakula
  • Bizari ya pulau kijiko kimoja cha chai
  • Binzari ya manjano nusu kijiko cha chai
  • Tui la nazi
  • Namna ya kutayarisha

Maandalizi

1. Katika sufuria weka utumbo, saumu, chumvi, pilipilili manga na tangawizi, Chemsha moto mdogo mdogo (usiweke maji kwanza). Kamulia ndimu na uache ichemke

2. Ukiona inakaribia kukauka weka maji na uchemshe huku ukiongeza maji hadi kuwiva, Mimina ndizi zako ulizokatakata katika supu ya utumbo uliochemsha

3. Weka nyanya na kitunguu, Weka bizari ya pilau na bizari ya njano na chumvi kidogo kama utahitaji

4. Achia ichemke kidogo ili soup ipungue, Weka tui lako na upike hadi ndizi kuiva

Chakula chetu kipo tayari kwa kuliwa

attachment.php
 

Attachments

  • IMG-20141011-WA0004.jpg
    IMG-20141011-WA0004.jpg
    89.3 KB · Views: 3,617
Na hata ukiwiva hao vidudu hawajafa tu?

Kuna hadith ya Mtume (s.a.w) niliisikia anasema hata nyama zina maradhi...ila akafundishe itibiwe kwa thomu na tangawazi (You can prove me wrong guys)

Labda MziziMkavu atufafanulie
 
ahhhh we mchokozi :wacko: this is my favorite food ever.....hii kitu naweza kula dailyyy....umenitamanisha na utumbo siupati mpaka niende nchi ya jirani....
 
ahhhh we mchokozi :wacko: this is my favorite food ever.....hii kitu naweza kula dailyyy....umenitamanisha na utumbo siupati mpaka niende nchi ya jirani....


Pole habibty leo zamu yako si umeninyima bokoboko wewe?
 
Back
Top Bottom