Pre GE2025 Mapokezi makubwa ya Rais Samia Mkoani Songwe

Pre GE2025 Mapokezi makubwa ya Rais Samia Mkoani Songwe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa mapokezi makubwa ,mazito na ya heshima aliyoyapata na kupewa Rais Samia alipokanyaga ardhi ya Mkoa wa Songwe ,kwa hakika nawashauri CHADEMA wasijaribu wala kusubutu kusimamisha Mgombea Urais uchaguzi ujao.maana wakijaribu na kupuuzia ushauri huu watakwenda kuvuna aibu ambayo haijawahi kutokea katika Taifa letu Tangia mfumo wa vyama vingi uanze na kuasisiwa hapa Nchini.

Nimeshuhudia kwa macho yangu Mwenyewe maelfu kwa maelfu ya wananchi wakimiminika kwa bashasha, matumaini, tabasamu na furaha kubwa katika nyuso zao,kwenda kumlaki Rais Samia wilayani Mbozi eneo la mji mdogo wa Mlowo .mapokezi ambayo hayajawahi kutokea wala kufanyika.

Yalikuwa ni mapokezi ya aina yake,palikuwa hakuna mahali pa kukanyaga wala kuweka mguu wako endapo utatoa mguu wako ulipokuwa umeweka Awali. Ilikuwa mkiachana na mwenzako hatua moja basi humuoni tena mpaka upige labda simu tena simu iwe na sauti kubwa na vibration,maana ilikuwa ni shangwe ,nderemo na vifijo muda wote kutoka kwa wananchi waliofurika kwa maelfu.

Rais Samia anakubalika zaidi ya pesa halali ya Mtanzania au Dollar ya Mmarekani .anapendwa na kuungwa mkono utafikiri ametoka kuipatia nchi uhuru,.Muda wote watu walikuwa wanasema huyu ni Mama wa Taifa letu. Nimeshuhudia wale wanaojiitaga wapinzani wakitamani wapewe nafasi ili wajiunge na CCM leo leo na kuungana na Rais Samia katika ujenzi wa Taifa letu.

Wana Mlowo ,wana Mbozi na wana Songwe ambao asilimia kubwa ni wakulima mioyo yao imejaa furaha baada ya Rais Samia kutangaza uamuzi mzito wa kupandisha bei ya mahindi kwa kilo kufikia shilingi Mia 7.jambo ambalo limeinua Matumaini na morali kubwa sana kwa wakulima ambao wanaona neema imewashukia.

CHADEMA jikiteni na kuelekeza nguvu zenu katika kuokoteza Wabunge ,ambako mnaweza kubahatisha kupata hata Wabunge watatu,lakini huku kwenye Urais futeni na ondoeni kabisa ndoto hizo.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.View attachment 3045598View attachment 3045600View attachment 3045601View attachment 3045602
Nchi yetu Ina wajinga wengi pia. Wewe ni mfano wa wajinga tulionao. Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kukesha kuandika vitu kama hivi. Mungu chukua hili lishetani haraka Sana lichome moto liteketee
 
Sasa mbona huyo Mama anataka kutoroka na Maboksi ya Kura.
 
Ushauri uliowapa ni mzuri. Watajiingiza tu hasara kuweka mgombea urais. Ila Mbowe mjanja yeye atagombea ubunge huku akiweka mgombea urais wa kukodi kutoka CCM.
 
Msafara wa gari 152 ,kila gari lina watu wasiopungua watano ,hapo tu UJUMBE una watu zaidi ya 750...Ukijumlisha na wanafunzi primary na secondary lazima mapokezi yaonekane makubwa.
 
Msafara wa gari 152 ,kila gari lina watu wasiopungua watano ,hapo tu UJUMBE una watu zaidi ya 750...Ukijumlisha na wanafunzi primary na secondary lazima mapokezi yaonekane makubwa.
Acha wivu wako wewe .Naona mmekosa hoja .kwa kuwa awali mlikuwaga mnasema watu ni wachache kwenye mikutano yake .sasa mmeanza kuweweseka baada ya kuona mafuriko ya wananchi kila anapotua Rais wetu mpendwa
 
Nchi yetu Ina wajinga wengi pia. Wewe ni mfano wa wajinga tulionao. Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kukesha kuandika vitu kama hivi. Mungu chukua hili lishetani haraka Sana lichome moto liteketee
Wewe hunaga akili kabisa .
 
Halafu siku ya uchaguzi mnazima internet na kuengua wagombea wa CHADEMA
CHADEMA na wagombea wake Wakifanya uzembe wa kujaza Fomu wataenguliwa tu bila huruma.maana tume haiwezi Lea na kuvumilia ujinga na uzembe.
 
Mimi siyo chawa ndugu yangu mtanzania uliyejaa msongo wa mawazo na wivu .
Huyu mtanzania anahitaji kupewa elimu ili kujua mazuri yanayotendeka nchini ili aungane nasi tuliojaa bashasha na kububujikwa machozi ya furaha kila tunapokumbuka kazi nzuri za Mama.
 
Back
Top Bottom