Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi, kama kawaida yangu, nipatapo nafasi, huzungukia maeneo mbalimbali ya nchi yetu kushuhudia haya na yale.
Leo nimepata fursa kushuhudia shamra shamra za mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Mkoani Dodoma.
Jana Mwenge ulilala Kijiji cha Mwitikira Wilaya ya Bahi. Mambo niliyoyaona usiku wakati wa mkesha wa mwenge, naomba nisiyateje yasije kuniharibia flow ya thread yangu hii.
Leo asubuhi Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Chalamila Mkwasa (Mama Master) amemtambulisha kiongozi wa Chadema wa eneo hilo na kusisitiza Wakuu wa wilaya ni watumishi wa wote, kazi yao ni kuhimiza maendeleo kwa kushirikiana na wote bila kujali itikadi za vyama ndio maana hata kiongozi wa Chadema amekaribishwa!.
Mwenge umeanza mbio zake wikayani Bahi saa 4:00 asubuhi hii kwa kuwekwa jiwe la msingi ukumbi wa kisasa wa mikutano uliogharimu shilingi Milioni 65 zilizochangwa na wananchi kwa asilimia 100%.
Kiukweli wilaya ya Bahi imefanya kufuru kwa jinsi walivyojipanga kuanzia sare maalum kwa watumishi wote wa umma wilaya ya Bahi.
Ule mtindo wa kuwatumia watoto wa shule kwenye shughuli za kitaifa unaendelea!. Japo leo ni siku ya Jumapili, wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wametinga uniform na kujitokeza kwa wingi (inaonyesha wamelazimishwa maana ni hadi watoto wa darasa la kwanza!
Japo significance ya mwenge wa uhuru ni issue debatable, mada hii sio subject matter ya thread yangu hii. Mimi najikita kwenye Kufuru za Bahi.
Fuatana nami kwa siku nzima ya leo nikiwaletea kila kinachojiri katika mapokezi ya Mwenge wilayani Bahi.
Karibu
Pasco