Mapokezi ya Mwenge Dodoma: Wilaya ya Bahi yafanya Kufuru

Kuhusu mwenge wa uhuru, kuna maeneo watu huwaambii kitu!. Saa hizi hapa bush Dom jua ni kali ajabu na tena la utosi!. mote tunapopita watu wamejazana barabarani tangu asubuhi wakisubiri kuushangilia mwenge huku wengine wakishangilia kwa matawi ya mimea kama alivyokuwa akishangiliwa Mwana wa Adamu ile siku anaingia Yerusalemu!.
Wengine wanashangilia kwa kupunga mikono tuu!.

Ila pia naomba kukiri, sura za walio wengi ni destitute!, living in less than a $ a day!, yaani wanaishi katika umasikini uliotopea!.

Na kuna wachache unawaona na sura za usongo na hasira sijui kama ni dhidi ya zoezi au aliyewatia umasikini huu walio nao.
 
Msafara wa Mwenge sasa umeingia kijiji cha Zenjele kuweka jiwe la msingi zahanati ya Zenjele uliogharimu milioni 74.
 
Pasco bana , hiki kipindi ndio kitaitwaje? Maana nanenane spesho kimeisha .......Betty kukupatia Bonge la shavu kama una kama M 6 hivi kibindoni au nimepunguza sana ?

Endelea na promo , huyu Betty anataka eti naye kuwa RC haridhiki na Udc , ambao aliupata baada ya kurusha kipindi cha kumtusi sana mzee Salim .....2005 , Muulize alikoenda DARUSO aliowahoji walimpa majibu gani ambayo yalifanyika kesho yake kuwa na kipindi maalum na watu waliojitokeza na kupewa cheo cha DARUSO .......IT'S Pathetic !
 
Kutoka Zenjele nikajikuta nina mahitaji ya kibinaadamu. hivyo nikachepuka kidogo na kutafuta hifadhi Zahanati ya Chipanga!.

Kwanza nilishangaa kukuta zahanati inafanya upasuaji kwa kutumia vifaa vya kisasa kabisa vinavyotumia solar!.

Yute tisa, kumi nikashuhudia nesi mmoja sii mchezo!. Utadhani hakuzaliwa bali aliumbwa na kushushwa moja kwa moja!.
Kusema ukweli sisi wengine tuna nadhaifu yetu!. Almanusura nighairi kuendelea na mbio za mwenge niwaambie wenzangu wakimaliza wanikute pale huwezi jua naweza kupata hifadhi ya zaidi na zaidi!.
Yaani !...
Hawa wazungu wametuharibia sana asili yetu ya kiafrika!.
 
Wanawekaje jiwe la msingi wakati mradi ushakamilika na gharama kufahamika?!
Au mi ndo sielewi maana ya kuweka jiwe la msingi na neno msingi lenyewe?!
 
Mkuu Deshmo, Dr. Anatua leo saa 8 mchana na chopa ya Ndesa Pesa ambapo bado inaendelea kuitwa Helcopter ya Mbowe hata kama Mbowe hajatua nayo!.
Nitawashauri Chadema endapo watachukua nchi 2015 kutokana na makosa ya CCM kutomsimamisha yule mgombea, then serikali ya Chadema iwajibike kuendelea kumuenzi Baba wa Taifa kwa kuendeleza mbio za mwenge ila wauzungushe kwa helcopter!.
P.

Huo Mwenge una bahasha.?
kama hauna Nenda katuletee update kwa Dr.Slaa
 
Tumechoka na upuuzi wa Mwenge maana Watu wazima wanainishwa kuwa unamurika mipaka ya TZ. Ni U-Pinda mtupu haaaaaa haaaa haaaa
 
Msafara umewasili Ngulugano. na kuweka jiwe la msingi maabara ya shule ya sekondari ya Chikola iliyogharimu Sh. milioni 70.
 
Yute tisa, kumi nikashuhudia nesi mmoja sii mchezo!. Utadhani hakuzaliwa bali aliumbwa na kushushwa moja kwa moja!.
Kusema ukweli sisi wengine tuna nadhaifu yetu!. Almanusura nighairi kuendelea na mbio za mwenge niwaambie wenzangu wakimaliza wanikute.

Tabia ya Pasco na swahiba wake Mwigulu ni sawa sawa
 
Last edited by a moderator:
Wanawekaje jiwe la msingi wakati mradi ushakamilika na gharama kufahamika?!
Au mi ndo sielewi maana ya kuweka jiwe la msingi na neno msingi lenyewe?!
Mkuu K'Jambazi, ni kweli baadhi ya miradi imekamilika kabisa na inafanya kazi hivyo haikustahili kuwekewa jiwe la msingi bali ilipaswa ndio izinduliwe!.

Ila pia mradi ni project hivyo cost inajulikana wazi kabla mfano bomba la gesi ni dola biloni 1.2.

Hata hivyo hili la kuweka jiwe la msingi miradi iliyokamilika kwa maoni yangu ikizinduliwa sasa kufikia 2015 watu watakuwa wamesahau!. Hivyo zinduzi nyingi zitafanyika 2015 ili october, mtimize wajibu wa kutoa asante kwenye..
Hata Daraja la Kigamboni, mabasi yaendayo kasi, katiba mpya, barabara za juu kwa juu etc!, kuna atakaye sema hapana?!.
 
mimi nitasema hapana kwenye sanduku la kura
 
Pasco bana , hiki kipindi ndio kitaitwaje? Maana nanenane spesho kimeisha .......Betty kukupatia Bonge la shavu kama una kama M 6 hivi kibindoni au nimepunguza sana ?

Endelea na promo , huyu Betty anataka eti naye kuwa RC haridhiki na Udc , ambao aliupata baada ya kurusha kipindi cha kumtusi sana mzee Salim .....2005 , Muulize alikoenda DARUSO aliowahoji walimpa majibu gani ambayo yalifanyika kesho yake kuwa na kipindi maalum na watu waliojitokeza na kupewa cheo cha DARUSO .......IT'S Pathetic !
Mpaka Kiele', hapa nafanya tuu kazi ya kanisa!. Betty Mkwasa ndie Mtanzania wa kwanza kutangaza FM akiwa RTD na kuna shavu alinipa hapa nalipa tuu fadhila.

Hata hivyo Pasco wa jf ni mwandishi wa kujitegemea kwa kujitolea. I don't make a single cent kwa uandishi!.
P.
 
Wajameni saa hizi ni saa 10:00!. Hatujaouna mchana!. Ingekuwa ni mwezi mtukufu tungeelewa!.
 
Mkuu Deshmo, Dr. Anatua leo saa 8 mchana na chopa ya Ndesa Pesa ambapo bado inaendelea kuitwa Helcopter ya Mbowe hata kama Mbowe hajatua nayo!.
Nitawashauri Chadema endapo watachukua nchi 2015 kutokana na makosa ya CCM kutomsimamisha yule mgombea, then serikali ya Chadema iwajibike kuendelea kumuenzi Baba wa Taifa kwa kuendeleza mbio za mwenge ila wauzungushe kwa helcopter!.
P.

Hahahaha mwenge uzungushwe kwa chopa?! Pasco una utani mbaya ujue!!
 
Anatua leo saa 8 mchana na chopa ya Ndesa Pesa ambapo bado inaendelea kuitwa Helcopter ya Mbowe hata kama Mbowe hajatua nayo!.
Nitawashauri Chadema endapo watachukua nchi 2015 kutokana na makosa ya CCM kutomsimamisha yule mgombea, then serikali ya Chadema iwajibike kuendelea kumuenzi Baba wa Taifa kwa kuendeleza mbio za mwenge ila wauzungushe kwa helcopter!.
P.

Msimamo wa CHADEMA kuhusu Mwenge wa Uhuru uko very clear, si leo, wala si jana. Siku nyingi. Mwenge unastahili kuwekwa Makumhusho ya Taifa.

Mwenge huu wa uhuru, ambao ni moja ya nembo za taifa, kwa miaka ya karibuni, chini ya uongozi wa CCM, umepoteza kabisa maana nzuri au nia njema iliyokuwepo wakati wa Mwalimu Nyerere na serikali ya awamu ya kwanza.

Pasco, with all due respect, kwa heshima na hadhi yako unapaswa kusema ukweli au kuandika vitu ulivyo na uhakika navyo mkuu. Katika ratiba ya Mabaraza Huru ya Katiba Mpya yanayoendeshwa na CHADEMA, leo hakuna ratiba ya Dodoma mjini.

CHADEMA si zote imeendelea kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kwa vitendo. Si kwa kukimbiza Mwenge unaotumika kuibia na kunyanyasa wananchi. Wanamuenzi kwa kupigania haki, matumaini ya wananchi, kupiga vita ufisadi na ubadhirifu wa CCM na kutimiza 'ndoto' zake za kuona nchi hii inapata mabadiliko ya mfumo na utawala, nje ya CCM, kupitia chama alichowahi kukiri mwenyewe kuwa ndiyo chama makini, chenye sera, dira na mwelekeo sahihi kwa ajili ya Watanzania.

Hayo ya mgombea, ni kama vile hujaeleweka hasa ulitaka kumaanisha nini mkuu!
 
Mwenge umeingia Kijiji cha Uhelela, hapa wamezindua mradi wa uvunaji mifugo na kumpongeza mfugaji tajiri Nduyuyaluha Lusendamila ana ng'ombe 370, mbuzi 76 na kondoo 57, ana wake 5 na wote wakiishi nyumba za tope zilizoezekwa kwa nyasi!.

Sasa amevuna mifugo yake, amejenga nyumba 6 za kisasa ya kwake na kila mke!. Amewanunulia kila mmoja gari la kutembelea na sasa ni mfanya biashara mkubwa anafikiria hadi kupunguza wake!.
 
Kutoka Zenjele nikajikuta nina mahitaji ya kibinaadamu. hivyo nikachepuka kidogo na kutafuta hifadhi Zahanati ya Chipanga!.

Kwanza nilishangaa kukuta zahanati inafanya upasuaji kwa kutumia vifaa vya kisasa kabisa vinavyotumia solar!.

Yute tisa, kumi nikashuhudia nesi mmoja sii mchezo!. Utadhani hakuzaliwa bali aliumbwa na kushushwa moja kwa moja!.
Kusema ukweli sisi wengine tuna nadhaifu yetu!. Almanusura nighairi kuendelea na mbio za mwenge niwaambie wenzangu wakimaliza wanikute pale huwezi jua naweza kupata hifadhi ya zaidi na zaidi!.
Yaani !...
Hawa wazungu wametuharibia sana asili yetu ya kiafrika!.

Hahahaha Pasco!! Nimecheka sana!

Kuhusu huyo nesi wengine kwa calibre yao wangekufa kijerumani! Wewe umeona uweke jukwaani wote tujue! Na madhaifu hayo wengi wanayo kimya kimya wewe umekiri kabisa!
Nimekuhamishia kundi jingine leo! Kwa heshima niliyokupa!
 
Back
Top Bottom