Mapokezi ya Mwenge Dodoma: Wilaya ya Bahi yafanya Kufuru

Mapokezi ya Mwenge Dodoma: Wilaya ya Bahi yafanya Kufuru

Nitawashauri Chadema endapo watachukua nchi 2015 kutokana na makosa ya CCM kutomsimamisha yule mgombea, then serikali ya Chadema iwajibike kuendelea kumuenzi Baba wa Taifa kwa kuendeleza mbio za mwenge ila wauzungushe kwa helcopter!.
P.
Huu ushauri bado ni muhimu nyakati hizi ?
 
Msimamo wa CHADEMA kuhusu Mwenge wa Uhuru uko very clear, si leo, wala si jana. Siku nyingi. Mwenge unastahili kuwekwa Makumhusho ya Taifa.

Mwenge huu wa uhuru, ambao ni moja ya nembo za taifa, kwa miaka ya karibuni, chini ya uongozi wa CCM, umepoteza kabisa maana nzuri au nia njema iliyokuwepo wakati wa Mwalimu Nyerere na serikali ya awamu ya kwanza.

Pasco, with all due respect, kwa heshima na hadhi yako unapaswa kusema ukweli au kuandika vitu ulivyo na uhakika navyo mkuu. Katika ratiba ya Mabaraza Huru ya Katiba Mpya yanayoendeshwa na CHADEMA, leo hakuna ratiba ya Dodoma mjini.

CHADEMA si zote imeendelea kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kwa vitendo. Si kwa kukimbiza Mwenge unaotumika kuibia na kunyanyasa wananchi. Wanamuenzi kwa kupigania haki, matumaini ya wananchi, kupiga vita ufisadi na ubadhirifu wa CCM na kutimiza 'ndoto' zake za kuona nchi hii inapata mabadiliko ya mfumo na utawala, nje ya CCM, kupitia chama alichowahi kukiri mwenyewe kuwa ndiyo chama makini, chenye sera, dira na mwelekeo sahihi kwa ajili ya Watanzania.

Hayo ya mgombea, ni kama vile hujaeleweka hasa ulitaka kumaanisha nini mkuu!
Leo humu jf kuna bandiko kuhusu Mwenge wa uhuru limepandishwa, hivyo nikajikumbusha enzi zangu za kukimbiza mwenge ndipo nikakutana na hii post ya Mkuu Tumaini Makene, nikaona nimsalimie tuu, na kumuulizia yuko wapi siku hizi amekuwa kimya sana na jee bado anaamini na kusimama na haya aliyo yaandika humu?.
P
 
Back
Top Bottom