Mapokezi ya Mwenge Dodoma: Wilaya ya Bahi yafanya Kufuru

Mapokezi ya Mwenge Dodoma: Wilaya ya Bahi yafanya Kufuru

Mwenge umeingia Kijiji cha Uhelela, hapa wamezindua mradi wa uvunaji mifugo na kumpongeza mfugaji tajiri Nduyuyaluha Lusendamila ana ng'ombe 370, mbuzi 76 na kondoo 57, ana wake 5 na wote wakiishi nyumba za tope zilizoezekwa kwa nyasi!.

Sasa amevuna mifugo yake, amejenga nyumba 6 za kisasa ya kwake na kila mke!. Amewanunulia kila mmoja gari la kutembelea na sasa ni mfanya biashara mkubwa anafikiria hadi kupunguza wake!.

Hivi unaposema kupunguza wake unaelewa analomaanisha?!

Je anamaanisha atataliki alionao?! atafukuza tu (nani ataendelea kuwahudumia watoto na wake hao) au hataendelea kuoa wengine?

Sababu aliyotoa ya kupunguza wake ni nini?! Isijekuwa anataka kubadili tu?! Ondoa hao wazee kisha alete vijana sasa?! Si unajua wazee wetu wanavyopenda vijana siku hizi?!
 
Hahahaha Pasco!! Nimecheka sana!

Kuhusu huyo nesi wengine kwa calibre yao wangekufa kijerumani! Wewe umeona uweke jukwaani wote tujue! Na madhaifu hayo wengi wanayo kimya kimya wewe umekiri kabisa!
Nimekuhamishia kundi jingine leo! Kwa heshima niliyokupa!
Bob, ukiwa mkweli ni unakuwa mkweli tuu. Sisi watu wa Kanda ya Ziwa ni dhaifu kwenye type flani!, tena sio tuu tunahonga sana!, pia tunapenda sana!, hatuna roho mbaya, tuna utamaduni wa wake wengi!, watoto wetu wote wanaozaliwa na hao wake zetu, wote ni watoto wetu!, hatuhitaji DNA etc. Kwa kukuongezea tuu habari zangu, mimi ni father of 6 na one of then ni .5 anaishi na 1st wife US!. Nina wife pia Toronto na hapa Bongo na kote kuna watoto!.
Nesi amekaribishwa rasmi!.
P.
 
Msimamo wa CHADEMA kuhusu Mwenge wa Uhuru uko very clear, si leo, wala si jana. Siku nyingi. Mwenge unastahili kuwekwa Makumhusho ya Taifa.

Mwenge huu wa uhuru, ambao ni moja ya nembo za taifa, kwa miaka ya karibuni, chini ya uongozi wa CCM, umepoteza kabisa maana nzuri au nia njema iliyokuwepo wakati wa Mwalimu Nyerere na serikali ya awamu ya kwanza.

Pasco, with all due respect, kwa heshima na hadhi yako unapaswa kusema ukweli au kuandika vitu ulivyo na uhakika navyo mkuu. Katika ratiba ya Mabaraza Huru ya Katiba Mpya yanayoendeshwa na CHADEMA, leo hakuna ratiba ya Dodoma mjini.

CHADEMA si zote imeendelea kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kwa vitendo. Si kwa kukimbiza Mwenge unaotumika kuibia na kunyanyasa wananchi. Wanamuenzi kwa kupigania haki, matumaini ya wananchi, kupiga vita ufisadi na ubadhirifu wa CCM na kutimiza 'ndoto' zake za kuona nchi hii inapata mabadiliko ya mfumo na utawala, nje ya CCM, kupitia chama alichowahi kukiri mwenyewe kuwa ndiyo chama makini, chenye sera, dira na mwelekeo sahihi kwa ajili ya Watanzania.

Hayo ya mgombea, ni kama vile hujaeleweka hasa ulitaka kumaanisha nini mkuu!
Mkuu Tumaini Makene, kwanza heshima mbele. Pili nikupongeze na kuwapongeza Chadema kwa remakable improvements kwenye idara ya public information!. Hongereni sana!. Ni mwanzo mzuri ila bado!.

Nikirudi kwenye hoja ya Chadema hapa Dodoma, mimi ndio niko hapa Dodoma nani kakuambia niko mjini?.

Naamini hata nikukuuliza gari lenu la PA huku Bahi jana limelala wapi wewe utakuwa hujui!. Find out linatangaza nini urudi kuniambia you are sorry!. Wewe kama mtu wa Public Information program hapo Chadema kama hujui ni nini kinachotangazwa na Chadema PA huku Bahi then you still have a problem.

La Chadema na Mwenge, find out kiongozi wenu Bahi, ametambulishwa, amepanda jukwaani, amesakimia!. Find out alikuja kufanya nini?!.

Sina chama kuna issues za Chadema is fighting for nazikubali na kuna issues za unafiki nazipinga!.

Mfano mzuri mlipijifanya hamumtambui dhaifu!. Niliwaambia humu mnamtambua kimya kimya mkapinga!. Hivi mliwahi kutangaza rasmi kumtambua rasmi?!. Ikulu mlikwenda kunywa tuu chai kama mgahawani?!.

Nawashauri mkiingia, mwenge ni kwa chopa!.
Pasco.
 
Mbio zimeingia Bahi mjini. Mji mzima umezizima kwa nderemo na vifijo!.
Bahi Sokoni wamezindua mradi wa mashine za kuvunia mpunga wenye thamani ya Milioni 14!. Vijana wa boda boda hawakuachwa nyuma, wameshushiwa milioni 2!. Funga kazi ni mradi wa nyumba za watumishi wa umma zenye thamani ya Shilingi milioni 540.

Jumla ya miradi yote zaidi ya Bilioni 1.2 kama bomba la gesi!. Tofauti ni kwenye bomba la gesi ni $ Bilioni 1.2 miradi ya Bahi ni Bilioni 1.2!. Hii sio kufuru?!.

Tukiioatia tena CCM another 5 years term!, itaigeuza Tanzania kuwa kama peponi!.

Sasa Mwenge umetua viwanja vya mkesha. Linafanyika bonge la pati!.
Ya usiku naomba nisiyaseme!.
Pasco
 
Mwenge umeingia Kijiji cha Uhelela, hapa wamezindua mradi wa uvunaji mifugo na kumpongeza mfugaji tajiri Nduyuyaluha Lusendamila ana ng'ombe 370, mbuzi 76 na kondoo 57, ana wake 5 na wote wakiishi nyumba za tope zilizoezekwa kwa nyasi!.

Sasa amevuna mifugo yake, amejenga nyumba 6 za kisasa ya kwake na kila mke!. Amewanunulia kila mmoja gari la kutembelea na sasa ni mfanya biashara mkubwa anafikiria hadi kupunguza wake!.

Kwa iyo uyo nae ni bilionea?
Duu! nshaanza kuielewa ile topic ya siondoki Dar, ya lara 1
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Deshmo, Dr. Anatua leo saa 8 mchana na chopa ya Ndesa Pesa ambapo bado inaendelea kuitwa Helcopter ya Mbowe hata kama Mbowe hajatua nayo!.
Nitawashauri Chadema endapo watachukua nchi 2015 kutokana na makosa ya CCM kutomsimamisha yule mgombea, then serikali ya Chadema iwajibike kuendelea kumuenzi Baba wa Taifa kwa kuendeleza mbio za mwenge ila wauzungushe kwa helcopter!.
P.

P. 2015 Cdm ikuchukua nchi ntashauri mwenge ukae makumbusho atayetaka kuenzi atoe hela yake apande basi aende akauenzi huko makumbusho!
Kuliko ilivyo sasa baada ya kumpumzika vinalazimishwa kwenda kwenye mwenge
sehemu zingine huduma kama za maduka,vituo vya afya n.k
watu wanachangishwa michango isiyojulikana mraji nani na karibu 250ml na zaidi kila mwaka, pili itawapunguzia michango isiyo na misingi kwa wananchi
mf: mimi sehemu yangu ya biashara wamepitisha daftari kama mchango wa msiba wanataka 1000/= nikawaambia stoi hata mia bila risiti hawakurudi tena, nafka home watoto wametumwa 200/= za mwenge naamka asubuhi ile natoka tu
nakutana na balozi anataka 500/= nikamwambia ntatoa naye pia hakurudi hadi leo!
Hii ni kero nyeusi!!!!!
 
Kaka Pasco mgombea ameishaanza kuhundiwa zengwe nn? Mbona unajiahami mapema...Team EL mnawoga sana..by the way ulinihaidi kunambia salva wenu nani ila mpaka leo haujasema!
Salva wa El yupo na ni member humu.Kwa vile EL, bado hajawa, huyo Salva wake, naye bado hajawa, let's not preempt hiyo kitu, tusubiri awe nitakutajia!.

Formula ya EL, tutajadili kuvuka daraja tukifika darajani .
J.
 
Kuanzisha sare za wafanyakazi wa serikali? Pasco nani anagharamia?
Kwa kawaida sare zote hadi za harusi, wahusika huchanga. What if Halmashauri imekusanya surplus na wakaamua kutoa bones Kwa kununua matenge ya wax za kente ?.
 
Pasco, hebu jaribu kuleta post za maana, hizi habari za kibatari -mwaka 2013 ni utani usiokubalika!
Mkuu

FJM, Pasco wa jf ni mwandishi wa habari za kimaendeleo Kwa kujitolea. Miradi ya zaidi ya 1.2 billions imezinduliwa!. Hayo ndio maendeleo tunayoyazungumzia katika safari ya kuelekea kwenye maisha bora kwa kila Mtanzania. Mkiishaipa tena CCM term nyingine ya miaka 5 ya mwisho, maisha bora kwa kila Mtanzania yatapatikana, hivyo 2020, there will be no need to think otherwise!.
 
Kwa kawaida sare zote hadi za harusi, wahusika huchanga. What if Halmashauri imekusanya surplus na wakaamua kutoa bones Kwa kununua matenge ya wax za kente ?.
Ndio hapo tunaposema Tundu Lissu anapoint kuhusu kuwachangisha wananchi masikini kuwa ni mwiko kama Halmashauri zinakusanya mapato yake in surplus na bado kuna fedha zingine zinarudishwa Hazina eti hazikutumika na mwaka wa fedha umeisha.
 
Nchii bhana mie mpaka leo sielewi umuhimu wa mbio za mwenge licha ya kutumia pesa nyingi! Mambo ya kizamani kweli
Mbona kwenye avatar yako nakuona unauwasha?, mi mwezio chama kitakachoahidi kusitisha mbio za mwenge ndo ntakichagua
 
Mkuu

FJM, Pasco wa jf ni mwandishi wa habari za kimaendeleo Kwa kujitolea. Miradi ya zaidi ya 1.2 billions imezinduliwa!. Hayo ndio maendeleo tunayoyazungumzia katika safari ya kuelekea kwenye maisha bora kwa kila Mtanzania. Mkiishaipa tena CCM term nyingine ya miaka 5 ya mwisho, maisha bora kwa kila Mtanzania yatapatikana, hivyo 2020, there will be no need to think otherwise!.
o

Achilia mbali miradi mliyozunduwa mwaka jana, ile ya mwaka juzi mmeshakamilisha?
 
Mbio zimeingia Bahi mjini. Mji mzima umezizima kwa nderemo na vifijo!.
Bahi Sokoni wamezindua mradi wa mashine za kuvunia mpunga wenye thamani ya Milioni 14!. Vijana wa boda boda hawakuachwa nyuma, wameshushiwa milioni 2!. Funga kazi ni mradi wa nyumba za watumishi wa umma zenye thamani ya Shilingi milioni 540.

Jumla ya miradi yote zaidi ya Bilioni 1.2 kama bomba la gesi!. Tofauti ni kwenye bomba la gesi ni $ Bilioni 1.2 miradi ya Bahi ni Bilioni 1.2!. Hii sio kufuru?!.

Tukiioatia tena CCM another 5 years term!, itaigeuza Tanzania kuwa kama peponi!.

Sasa Mwenge umetua viwanja vya mkesha. Linafanyika bonge la pati!.
Ya usiku naomba nisiyaseme!.
Pasco

Mkuu Pasco,asante kwa kujitolea kutuhabarisha.Hata kama unalipwa, ila si JF wanao kulipa kutuletea habari, katika hili pokea heshima unazostahili.Asante.Wabezya sana nkoi!

Pamoja na hayo, naona heri utangaze nia mapema:Jimbo gani lakini--maana naona chapuo unalopiga kwa chama kinachokimbiza mwenge ni kubwa...?

Sambamba na hilo, kweli miaka mitano CCM itaigeuza Tanzania peponi?Sahau habari za TANU ambacho CCM amerithi mikoba yake, je, kuna chama kingine kimewahi tawala zaidi ya kilichopo madarakani? Kama miaka hamsini ya uhuru wameshindwa kuigeuza pepo, sembuse miaka mitano?
 
Mkuu

FJM, Pasco wa jf ni mwandishi wa habari za kimaendeleo Kwa kujitolea. Miradi ya zaidi ya 1.2 billions imezinduliwa!. Hayo ndio maendeleo tunayoyazungumzia katika safari ya kuelekea kwenye maisha bora kwa kila Mtanzania. Mkiishaipa tena CCM term nyingine ya miaka 5 ya mwisho, maisha bora kwa kila Mtanzania yatapatikana, hivyo 2020, there will be no need to think otherwise!.

Mkuu Pasco, sidhani kwamba ili hiyo miradi ya bilioni moja ionekane ni lazima watu wakeshe kwa kunywa na kufanya ufuska pamoja na matumizi mengine yasiyokuwa ya lazima. Tufike mahali tubadilike, tusifanye mambo kwa mazoea/historia bali kwa sababu za kisayansi.
 
Back
Top Bottom