Mapokezi ya Nyerere huko Uingereza

Mapokezi ya Nyerere huko Uingereza

Heshima kama hii bado ipo kwa viongozi wa sshv??!!!

Daima tutaendelea kujivunia kwa uongozi wako madhubuti mwl. Julius K. Nyerere.
 
Alianzisha taasisi za kuendeleza siasa zake. Mojawapo ni chuo cha chama cha Kivukoni. JK ni mmoja wa wahitimu kama sitakosea.

Tatizo ni kuwa siasa zake na hazilipi. Na mabadiliko ya kisiasa duniani yalipotokea, wale waliokuwa kwenye siasa hawakuwa na profession yoyote ya ku-survive nje ya siasa. Hivyo wamebaki kuwa mafisadi, case in point Lowassa, JK etc.

Unaposema hazilipi unamaanisha nini?
Legacy alioiacha hakuna kiongozi africa na tanzania atakayeweza kuendeleza.
Mfano tu viwanda, wakati wake alijenga zaidi ya viwanda 400 vya huduma na bidhaa muhimu.
Leo vipo wapi?
 
Unaposema hazilipi unamaanisha nini?
Legacy alioiacha hakuna kiongozi africa na tanzania atakayeweza kuendeleza.
Mfano tu viwanda, wakati wake alijenga zaidi ya viwanda 400 vya huduma na bidhaa muhimu.
Leo vipo wapi?

Nitajie top 5 CEOs or General managers ambao walivifanya kazi nzuri sana ya kukumbukwa Tanzania au Africa.
 
Nina imani Magufuli ataliletea taifa hili heshima kubwa kama Nyerere
 
Nyerere ataishi moyoni mwangu siku zote. Ndio mfalme wa siasa za Tz, hatakuja mwingine. Ni kama ambavyo hatatokea Michel Jackson Mwingine.
 
Huwa tunapishana sana "kiswahili " lakini kwa uzi huu tuko pamoja.
 
Asante sana Bwana N.Ngabu.
Umenisaidia kutunza historia.
Nashangaa kuona CCTV wameweza kufanya compilation hii. Je kwetu kuna waliojareibu? Kama wapo, kazi zao zinapatikanaje?
Asante tena!´´
 
Na kama umeangalia vizuri, hapo kwenye horse-drawn carriage wakati wapo barabarani watu walikuwa wanashangalia.

Kwa kweli alipewa heshima kubwa sana.
Jamani, mbona mnasahau hata Kikwete alipanda carriage ya farasi Canada alipokwenda kusaini mikataba ya kulinda maslahi ya wawekezaji wa Canada?
 
Hivi kwanini Nyerere hakutengeneza Nyerere wengine wa miaka 50 ijayo?
Sasa Tanzania tunasumbuka na marais wa ajabu sana.

Sometimes you just get soo damn good, it becomes hard to comprehend what you do is out of the ordinary. Story of Ferguson Manchester.., hadi leo hii anaalikwa business schools duniani kutoa mihadhara ya makosa ya succession...,
 
Alianzisha taasisi za kuendeleza siasa zake. Mojawapo ni chuo cha chama cha Kivukoni. JK ni mmoja wa wahitimu kama sitakosea.

Tatizo ni kuwa siasa zake na hazilipi. Na mabadiliko ya kisiasa duniani yalipotokea, wale waliokuwa kwenye siasa hawakuwa na profession yoyote ya ku-survive nje ya siasa. Hivyo wamebaki kuwa mafisadi, case in point Lowassa, JK etc.


Siasa za Sampuli ya Mwalimu ndio zinatawala Western Europe yote ambao account za benki bado zinasoma. Uingereza Nchi ina madeni kibao hadi inaogopa kukopa tena.

Tazama nchi za kisocialist kwa maana ya ujerumani, scandinavian countires etc.., zote zina common theme.., elimu ni ya kiwango kitakatifu, na inatolewa BURE. huduma za afya zina universal coverage na hazina mfanowe kwa ubora.


Hii marekani na holywood zimeharibu watu kudhani maisha bora yako kwenye pure capitalism peke yake. Merkel Ujerumani, na social democrat yao hadi kesho mabepari wanapanga foleni kuomba mikopo. CHINA na ucommunist wao hadi kesho marekani credit line haikauki.., na hawa ndio wamefanikiwa kwenye kumilikisha njia kuu za uchumi kwa wananchi wao wenyewe. Industrial revolution ya china kama kila kampuni kubwa ya china ingekuwa ya wageni, leo hii serikali ingekuwa apeche haina hata senti, kwani kodi hazitoshi. Bepari kulipa kodi ni mtihani mzito..,


Nyerere alikuwa bianadamu amefanya makosa, lakini huwezi sema likosa master plan.., ni vile tu sisi kama nchi hatukuw atayari kupitia proper HELL ili kuvuka..., wachina walipita kwenye hell late 70's walipovuka hapo wanamuachia kila mtu vumbi.., sisi mambo yalivyokaba tukanyoosha mikono juu na kugeuka ndondocha tusio na identity.
 
Mwaka gani hii ilikuwa?haya ya Jimmy Carter pia yalikuwa makubwa
Sijui ni mwaka gani lakini kwa muonekano wa Nyerere [mvi na uso kuanza kuwa na makunyanzi[ naweza kusema labda ni miaka ya 70 mwanzoni mwanzoni.....

Hii itakuwa kwenye mwaka 1975 maana namuona Mwalimu akiwa no.10 wakipiga picha na Harold Wilson (Waziri mkuu) na James Callaghan (waziri wa mambo ya nje), Callaghan alikuwa waziri kwenye ofisi hiyo kuanzia February 1974 na kuachia ngazi April 1976 chini ya waziri mkuu Harold Wilson.
 
Back
Top Bottom