Mapokezi ya Rais akitokea Marekani kwenye UNGA ni ufujaji wa kodi za walalahoi

Mapokezi ya Rais akitokea Marekani kwenye UNGA ni ufujaji wa kodi za walalahoi

Hii nchi mbona tumekuwa watu wa ajabu sana? Kwanini waliopewa mamlaka ya kiuongozi wamekuwa wajinga kiasi hiki?

Hivi kweli hili nalo ni tukio la muhimu kiasi hicho? Rais kurejea nchini ni tukio la kufanya kuwa kama shughuli ya kitaifa? Kwanini lisingefanyika kwa protocol za kawaida tu?

Huu ni ufujaji wa kodi za walalahoi. Hizo gharama za hizi shughuli zingetumika kuwajengea wamachinga mnaowavunjia vibanda vyao maeneo mazuri wafanye biashara zao ili waondoke mabarabarani wanapofanyia biashara.

Kweli tulidhani kuwa tumemaliza kuyaona maajabu enzi za mwendazake kumbe sasa ndio tuna viongozi wanaojipendekeza kwa rais kiasi cha kufanya mambo yasiyo ya msingi kabisa.

Ongezeni tozo.

View attachment 1951669
Mlimpokea Lissu Kwa maelfu

Hebu tulieni kidogo
 
Ujinga, Umasikini bado vyatusumbua toka 61
 
Mh.Chifu Mkuu Hangaya....

Kipenzi chetu mh.Rais SSH....

HAKIKA KWELI NI NYOTA.....💪😍👊

2935117_Screenshot_20210920-071732.png
 
Hii nchi mbona tumekuwa watu wa ajabu sana? Kwanini waliopewa mamlaka ya kiuongozi wamekuwa wajinga kiasi hiki?

Hivi kweli hili nalo ni tukio la muhimu kiasi hicho? Rais kurejea nchini ni tukio la kufanya kuwa kama shughuli ya kitaifa? Kwanini lisingefanyika kwa protocol za kawaida tu?

Huu ni ufujaji wa kodi za walalahoi. Hizo gharama za hizi shughuli zingetumika kuwajengea wamachinga mnaowavunjia vibanda vyao maeneo mazuri wafanye biashara zao ili waondoke mabarabarani wanapofanyia biashara.

Kweli tulidhani kuwa tumemaliza kuyaona maajabu enzi za mwendazake kumbe sasa ndio tuna viongozi wanaojipendekeza kwa rais kiasi cha kufanya mambo yasiyo ya msingi kabisa.

Ongezeni tozo.

View attachment 1951669
Mbona hatuonyeshwi ndege aliyo tumia?
 
Ametoa mshahara wake au? Rais hawezi kutoa hela yakufanya maendeleo maana sio yake. Yeye anaidhinisha kutolewa kwa hela hiyo. Siasa uchwara muache.
Vuta pumzi Chalii.....🤣

"Kuidhinisha" fedha ya UMMA kwa ajili ya hayo nako ni maamuzi kuntu bwashee💪
 
Huu utaratibu wa AHADI ni uhuni wa kila msimu unafanywa, wakulima hujikuta wanasubiri ahadi hewa hivyo kuendelea kukopa pembejeo kupitia vikundi vya vyama vya msingi (Korosho na Tumbaku ndiyo waathirika wakuu).

CCM bhana!
Mkuu mbona hizo bilioni 60 zimeshatengwa kaka....

Tusiandikie mate muda UTAONGEA....

#SiempreJMT
#NakupendaTanzaniaNchiYaAmaniNaTulivuKulikoZoteAfrika
 
Ukiona harakati za namna hii, ujue kuna jambo kiuongozi haliko sawa. Hivyo kuna makundi ya watu wanahangaika/wanalazimika kumtia moyo mama hata pale anapoharibu au ameshindwa kufikia matarajio ya Watanzania walio wengi
Wanajaribu kumpa moyo na support. Alionekana kupwaya sana kwenye ile hotuba yake.....!!
 
Back
Top Bottom