KOCHA AFANYIE KAZI YAFUATAYO:
1. Aachane kabisa na lile soka tulilocheza ugenini kule cape verde la kupaki basi
2. Ashambulie mwanzo mwisho na amiliki mpira muda wote ili kumyima adui mwanya wa kutuangamiza.
3. Wacheze pasi ndefu za chini chini lakini wakijiloga kucheza mipira ya juu wameumia maana majamaa ni marefu sana na nimesikia kuwa wameapa bora wafie uwanjani mbele ya mashabiki wao kuliko kufungwa.
4. Apunguze kumwamini sana SAMATTA na kumwogopa kwani mara nyingine hata kikosi anapanga yeye na kuwapendelea marafiki zake ambao viwango vyao vimeshaashuka ili kuwarudisha kwenye chati kama akina ULIMWENGU.
5. Wasikate tamaa mbele ya kelele za mashabiki wao amabao watakuwa wengi sana hata kama wakiwa wakwanza kufunga, wapambane na kurudisha bao hilo na kuongeza ushindi.
BAADA YA USHINDI WAKATI WA KUPOKEA TIMU.
1. Brass band za majeshi yote ziwe uwanjani na vifaa vyao na uniform full mzuka kuwapokea vijana hao.
2. Kikosi cha polisi cha farasi kitangulie wakiwa wamebeba bandera ya Taifa
3. Liwepo gari kubwa la wazi lililopambwa rangi za Taifa liwabebe mashujaa hao
4. Wananchi wakusanyike barabarani na ikiwezekana maduka yafungwe na shughuli zote zisimame kama ilivyokuwa alipokuja PAPA PAUL II
5. Ziwepo mbwembwe na sherehe za kila namna na vyombo vya habari vya nje na ndani virushe live ili h abari ziwafikie raisi wa fifa, caf na musonye popote walipo duniani.
6. Viongozi wa serikali wafike uwanjani wakiwa wamevalia jezi za timu ya taifa ili kuwapokea mashujaa.
7. Maandamano yapite mjini wakiongozwa na kundi kubwa la brass band za majeshi yote huku wakitembea polepole na kupiga nyimbo za kizalendo kama tuna imani na.... oya..oya..