Mapumziko ya Kitaifa baada ya Ushindi wa Taifa Stars

Mapumziko ya Kitaifa baada ya Ushindi wa Taifa Stars

Dah Uganda wamenifurahisha sana, yaani hapo tunahitaji draw tu tutoboe
Draw!! How..?? Tunahitaji ushindi leo.. tukishinda tunafikisha point 8 kitu ambacho lethoto wala carpe verde hawawezi fikia hizo points..
 
we unafanya shuguri gani, hivi unajua ni kiasi gani cha mapato tunayopoteza siku za mapumziko halafu mnataka muondokane na umasikini
Mkuu kupumzika haimaanishi umasikini na kufanya kazi sana haimaanishi utajiri. Tunapoteza mapato mengi huko kwa wakwepa kodi, wapiga madili Serikalini, uzembe wa baadhi ya wakusanya kodi, mikakati mibovu etc, USA wana holidays nyingi kuliko sisi ila wanatuzidi maendeleo.

Acha sisi tupumzike zetu
 
Unama
KOCHA AFANYIE KAZI YAFUATAYO:

1. Aachane kabisa na lile soka tulilocheza ugenini kule cape verde la kupaki basi

2. Ashambulie mwanzo mwisho na amiliki mpira muda wote ili kumyima adui mwanya wa kutuangamiza.

3. Wacheze pasi ndefu za chini chini lakini wakijiloga kucheza mipira ya juu wameumia maana majamaa ni marefu sana na nimesikia kuwa wameapa bora wafie uwanjani mbele ya mashabiki wao kuliko kufungwa.

4. Apunguze kumwamini sana SAMATTA na kumwogopa kwani mara nyingine hata kikosi anapanga yeye na kuwapendelea marafiki zake ambao viwango vyao vimeshaashuka ili kuwarudisha kwenye chati kama akina ULIMWENGU.

5. Wasikate tamaa mbele ya kelele za mashabiki wao amabao watakuwa wengi sana hata kama wakiwa wakwanza kufunga, wapambane na kurudisha bao hilo na kuongeza ushindi.

BAADA YA USHINDI WAKATI WA KUPOKEA TIMU.

1. Brass band za majeshi yote ziwe uwanjani na vifaa vyao na uniform full mzuka kuwapokea vijana hao.

2. Kikosi cha polisi cha farasi kitangulie wakiwa wamebeba bandera ya Taifa

3. Liwepo gari kubwa la wazi lililopambwa rangi za Taifa liwabebe mashujaa hao

4. Wananchi wakusanyike barabarani na ikiwezekana maduka yafungwe na shughuli zote zisimame kama ilivyokuwa alipokuja PAPA PAUL II

5. Ziwepo mbwembwe na sherehe za kila namna na vyombo vya habari vya nje na ndani virushe live ili h abari ziwafikie raisi wa fifa, caf na musonye popote walipo duniani.

6. Viongozi wa serikali wafike uwanjani wakiwa wamevalia jezi za timu ya taifa ili kuwapokea mashujaa.

7. Maandamano yapite mjini wakiongozwa na kundi kubwa la brass band za majeshi yote huku wakitembea polepole na kupiga nyimbo za kizalendo kama tuna imani na.... oya..oya..
unamakadilio ya juu Mzee
 
Kupumzika kisa ushindi wa Taifa stars ni uharibifu wa siku kiujumla.
 
Ni dhahiri kuwa baada ya Uganda kuichapa Cape Verde pale Kampala na hatimaye kufuzu AFCON 2019, Tanzania ina nafasi kubwa sana ya kufuzu pia.

Sasa wakati timu yetu ikisubiri kutupa zawadi hiyo tuliyosubiri kwa muda mrefu tangu 1980, na kwa vile Mh. Rais JPM ni mwanamichezo ni dhahiri kuwa hato tuangusha. Namaanisha atatangaza siku kadhaa za mapumziko ya Kitaifa kuisapoti timu na kusherehekea kufuzu huko.

Swali ni je! Mh. Rais atangaze siku ngapi za mapumziko? Mi nadhani siku tatu zitafaa sana. Yani mfano tukifuzu kesho jumapili basi tupumzime hadi jumatano.

Sasa nyie wachezaji wa Taifa Stars msituharibie ratiba yetu ya mapumziko. Inatakiwa mshinde tu... Watu tumeshajipanga kwa long break
Tunachohitaji leo nikuomba na wachezaji wajitume tushinde kwanza
usipange sherehe kabla muolewaji hajakubali....halafu ndio kucheherekea
 
Nimeangalia statistics kwa umakini mkubwa, nimegundua hata tukipigwa 1 - 0, bado tunafuzu, ila tukipigwa 2 - 0 ndio bye bye
kufuzu kwetu ni kushinda mechi ya leo timu hizo mbili chini yetu hazitafikia point zetu vinginevyo lesotho naye nafasi atakuwa nayo.kumbuka kila timu inatakiwa icheze mechi 6
 
kufuzu kwetu ni kushinda mechi ya leo timu hizo mbili chini yetu hazitafikia point zetu vinginevyo lesotho naye nafasi atakuwa nayo.kumbuka kila timu inatakiwa icheze mechi 6
Okay, nilidhani mchezo wa leo ndio wa mwisho eti
 
Mh Rais katamka neno KUSHINDA mara nyingi zaidi kuliko neno lolote.
.......
Sasa TAIFA STAR wasiyasahau maneno yake na hasa neno USHINDI.
.....
HAKIKA KWA KUWA WATANZANIA WALISHACHOKA KUWA WASINDIKIZAJI NA KICHWA CHA MWENDEWAZIMU BASI ATAKACHOAMUA RAIS JUU YAO BAADA YA KUSHINDWA ITAKUA NI KWA MASLAHI YA TAIFA.
.....
HATUWEZI KUWA NA WACHEZAJI AMBAO KILA SIKU WAKIINGIA KWENYE VIWANJA VYA MPIRA, WAO SOKA WANAONA NI BORA WANACHEZA.

USHINDI WAO NDIO JASHO LA WATANZANIA
 
Inanikumbusha mbaali sana. Mwaka 1993 wakati Simba walipokua wanapepetana na Stella Artois ya Ivory Coast katika mechi ya pili ya marudiano ya fainali ya Kombe la CAF wakati huo likiitwa kombe la Abiola. Mchezo wa kwanza uliokua umechezwa Abijan, walikua wametoka suluhu ya kutokufungana

Kulikua na MC pale Uwanja wa Taifa-Shamba la Bibi akitoa matangazo ya namna gani Kombe litakavyokua linatembezwa katika mitaa na viunga vya jiji la Dar mara baada ya mchezo. Hii ni kutokana na imani kubwa waliojipa mashabiki kwamba Simba wataitandika Stella kwa mabao mengi tu

Haikua hivyo, kwani Jean Boli Zozo alizima ndoto hizo hasa ilee dakika ya sabini alipomchambua akimgeuza kama anachoma chapati ile beki Rashid Abdallah Magongo kisha kuachia block buster iliyompita udisputed Tanzania One wakati huo Mohamed Mwameja akiwa kasimama tu na kuiandikia Stella Abijan bao la pili

Yalitokea haya katika uwanja wa nyumbani wa Simba mbele ya Rais Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Zanzibar wakati huo Salmin Amour, John Malechela akiwa Waziri Mkuu na mawziri mbalimbali wa JMT

Basi tujufunze kotakana na historia, tusibweteke sana kwa kubebwa na Uganda. Tujue kua bado hatujamaliza kazi,inabidi tupate ushindi leo, tuwape moyo wachezaji wetu na tuwachagize wasijiamini kupita kiasi wakawadharau Lesotho, na huku dua zetu zikiwa kwa vijana wetu hodari kabisa wa Taifa Stars
 
Back
Top Bottom