Mapungufu niliyoyaona mechi ya jana Tanzania VS Sudan

Mapungufu niliyoyaona mechi ya jana Tanzania VS Sudan

Kocha Yuko vizuri ila anahitaji kujirekebisha maeneo fulani hasa ya kuchagua wachezaji sahihi na kufanya Sub sahihi na kwa wakati.
Washambuliaji kama Mwaikimba, ni vigumu kupatikana kwa urahisi, vijana wengi wenye nguvu na akili za kucheza Mpira wanachagua kusoma na kufanya biashara.
Badala ya kucheza mpira ambao kwao wanauona bado hauna security ya uhakika ya maisha yao.
 
Kosa la Kaseja kwenye lile goli ni lipi?
Kosa lake ni kuruhusu goli, angekuwa anapelekewa mashambulizi kama aliyokuwa anapelekewa kipa wa Sudan angekula hata tano..
.
Kaseja jua lake liko jioni sana, Manula sifa zimemzidi ameshajisahau ni wakati wa vijana wapya kushika hatamu Beno au Metacha
 
Tofauti kubwa kati yetu na Sudan wao wachezaji wao wazuri wanacheza ligi yao!! kwa sasa Tanzania nguvu yetu pale mbele inategemea uwepo wa Samata na Msuva!! Tatizo lingine kwa wachezaji waliochaguliwa kulikua hakuna plan B, kwa vimo vya wachezaji wetu krosi zile za Maganga ni kazi bure
Hata Hawa wakiwepo huwa sioni la ajabu taifa stars
 
mengi yatasemwa.. lakini bado nasema huo uwanja haufai kwa sasa una gungu/nuksi/mikosi katika mechi za mashindano za kimtaifa
kuna timu imeuharibu huo uwanja kwa mambo yao ya hovyo
Timu gn mkuu
 
mengi yatasemwa.. lakini bado nasema huo uwanja haufai kwa sasa una gungu/nuksi/mikosi katika mechi za mashindano za kimtaifa
kuna timu imeuharibu huo uwanja kwa mambo yao ya hovyo
Hahahaha nakubali mkuu, mechi dhidi ya As Vita asubuhi ya saa 12 kwenda saa 1 kuna pick up iliingiza nguruwe na ng'ombe mle ndani.
 
Hahahaha nakubali mkuu, mechi dhidi ya As Vita asubuhi ya saa 12 kwenda saa 1 kuna pick up iliingiza nguruwe na ng'ombe mle ndani.
hao sasa ndio waliouharibu uwanja na kuutia mkosi, wanatakiwa waende wakatengue mambo yao pale... la sivyo hakuna ushindi kwenye huo uwanja kwa mechi zijazo za kimataifa za kiushindani

Timu ilicheza vizuri kuanzia nyuma mpaka katikati japo kulikuwa na mapungufu ya Gadiel na Maganga kupiga krosi ambazo hazina macho. Makocha tuwape muda waendelee kwani sasa hivi japo timu inafungwa walau kidogo inaonyesha uhai wa kupambana. Nikiitizama timu ya sasa na ile ya Amunike naona hii ya sasa inahitaji marekebisho kwenye upande wa ushambuliaji kwani mabeki na viungo walipeleka mipira mbele lakini Nado, Chilunda na Lyanga walikuwa wanajigonga tu. Lakini makocha wetu nao wajifunze sio kila wakati lazima ucheze na washambuliaji mbele tunaona hata timu kubwa ulaya mara nyingine zinawatumia viungo waliotulia kuwa washambuliaji kwenye baadhi ya mechi. Kwa sababu kama mipira ilikuwa inafika mbele mara nyingi tu kilichohitajika ni mtu tu hata beki mwenye utulivu wa hali ya juu na jicho la mwewe kuutumbukiza mpira ndani ya goli.

Kwa upande wangu naona matatizo ya timu ya taifa yapo zaidi kwa washambuliaji namba 9 na 10. Boko umri umeanza kumtupa mkono na ana majeraha ya mara kwa mara, hawa Nado na Chilunda ni washambuliaji wa pembeni zaidi au nyuma ya striker namba 9 na tuwategemee zaidi baadaye na sio sasa. Kiujumla hatuna mshambuliaji mwenye uwezo binafsi wa kuamua matokeo ndio maana tulicheza sisi mpira muda mwingi wa mchezo lakini Sudan walifika kwetu mara mbili tu na hapo wakapata bao moja. Baada ya bao ndio wakaanza wao kucheza mpira. Watanzania kwa ujumla tuwape moyo vijana wetu wenye maumbo makubwa waanze kucheza soka badala ya kukimbilia basketball na kuwa mabaunsa kwani soka la sasa pamoja na ufundi linahitaji pia nguvu.
 
mengi yatasemwa.. lakini bado nasema huo uwanja haufai kwa sasa una gungu/nuksi/mikosi katika mechi za mashindano za kimtaifa
kuna timu imeuharibu huo uwanja kwa mambo yao ya hovyo
Iyo timu ina kombe gani la kimataifa..??
Yaani kufungwa jana sababu ni uwanja..? sio umakini wa foward zetu..?
Kweli kichwa cha mwendawazimu
 
ha haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa..........................
 
Kocha huyu hafai.. kwani hakuona hakuna strika kwenye list yake..
Watu wamesema mapema kabisa.. kaweka pamba masikioni
Ni nani mshambuliaji ambae hakuitwa.. AIYEE + BOCCO wagonjwa.
 
Back
Top Bottom