Mapungufu ya kisheria katika Kesi ya Yesu (kwa mujibu wa sheria ya wayahudi)

SONGOKA

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
1,841
Reaction score
1,843
(mode hii ni ya ki intelijensia zaidi, usiihamishe plse)

Usiku Yesu alipokamatwa alifikishwa mbele ya wafuatao kwa mashtaka, Caiaphas - Kuhani mkuu (na aliye agiza yesu akamatwe na pia ndiye aliandaa mashtaka), Annas - Kuhani mkuu mstaafu, na Sanhedrini - Baraza la makuhani. Kwa kuwa hawa ni viongozi wa kidini Yesu hapa alishtakiwa kwa makosa mawili;

1. Kufuru (blasphemy), 2. Kajitangaza kuwa ni mwana wa Mungu na Messiah

Baadaye akapelekwa kwa kwa Pilato, na huko mashtaka ghafla yakabadilika na kuwa matatu yafuatayo;

- Kutaharakisha jamii na kusababisha uasi (rioting)
- Kukataza watu kulipa kodi
- Kujitangaaza kuwa ni mfalme wa wayahudi (uhaini).

Makosa haya chini ya utawala wa Rumi adhabu yake ni kifo;

Hapa tunaona mashtaka yanabadilishwa kwa sababu nia ya Caiaphas ilikuwa yesu afe na kwa kuwa bataza la makuhani halina mamlaka ya kutoa hukumu ya kifo na pia mashtaka ya kwanza hayakuwa na mashiko wala hayakuwahusu watawala (Rumi), akaona ni vyema abadilishe mashtaka ili apate uhalali wa kumfikisha yesu mbele ya pilato (Gavana) na pia apate hukumu ya kifo.

Kumbuka yesu alikamatwa na askari wa hekalu (temple guards) kwa maagizo ya caiaphas na si askari wa utawala wa Rumi

Kesi ya Yesu chini ya viongozi wa kidini (kuhani mkuu na baraza la makuhani) iligubikwa na uvunjifu wa sheria za kiyahudi katika hali ya juu na waziwazi kiasi cha kutisha. Yafuatayo yalikiukwa kwa mujibu wa sheria za wayahudi za wakati huo;

1. Haikuruhusiwa kesi/shauri lolote kuendeshwa wakati wa sikukuu au maandalio ya sikukuu (No trial was to be held during feast time) lakini haohao viongozi wa sheria za kiyahudi waliendesha shauri la yesu wakati wa sikukuu ya pasaka

2. Kila mjumbe wa baraza alipaswa kupiga kura binafsi wakati wa maamuzi yeyote ya hukumu ( Each member of the court was to vote individually to convict or acquit) lakini yesu alihukumiwa kwa kura ya pamoja (but Jesus was convicted by acclamation.)

3. Kama mtu akihukumiwa kifo, hukumu hiyo itatekelezwa siku ifuatayo (If the death penalty was given, a night must pass before the sentence was carried out) lakini yesu alihukumiwa na hukumu ilitekelezwa muda mfupi tu baada ya hukumu kutolewa.

4. Wayahudi hawakuwa na mamlaka ya kutoa hukumu ya kifo, lakini hukumu ya yesu ilipendekezwa na wayahudi na wakampeleka kwa pilato kuomba ruhusa ya utekelezaji (The Jews had no authority to execute anyone.)

5. Haikuruhusiwa shauri lolote kuendeshwa wakati wa usiku (No trial was to be held at night) lakini shauri la yesu liliendeshwa usiku.

6. Mtuhumiwa yeyote alipaswa kupewa uwakilishi na uhuru wa kuleta mashahidi ( The accused was to be given counsel or representation) lakini yesu hakupewa nafasi hii.

7. Mashtaka ya mtuhumiwa yalipaswa kubakia hayo hayo katika kila hatua ya kesi, lakini yesu mashtaka yake yalibadilika kila stage ya kesi.

Kimsingi kesi ya Yesu ndo kesi iliyoongoza kwa uvunjifu wa sheria na utaratibu wa kuendesha mashauri na kesi na rekodi hiyo haijavunjwa mpaka leo.

Note: Uchambuzi huu ume base kutoka, (John 18:19-24; Matthew 26:57, John18:23, Luke 23:7, Luke 23:11-12, John 18:28, Luke 23:7, Luke 23:11-12, Luke23:25 na sheria za kiyahudi ni kwa mujibu wa mwanahistoria na mwandishi nguli Josephus aliyeishi wakati wa Yesu.)
 
(

Jesus is God. That is why the pharisees said He blasphemy when He compared Himself to God.
 
Kitu kingine ulichosahau ni kuwa Yesu alikuwa maskini hivyo hakuweza ku-afford a good lawyer, kama ambavyo inatokea kwenye jamii zetu mpaka leo.
It is a lie.

Jesus was not poor. He had 12 people working for Him. Nonetheless, He had a personal accountant. You don't have that.

Can a poor man be able to employ 12 people who were business men and an accountant?
 
Jesus is God. That is why the pharisees said He blasphemy when He compared Himself to God.

I agree but the bible itself quotes the jews separating these two allegations against jesus, checkn my references below the post
 
When Jesus said He is God few things happened.
(a) The Pharisees destroyed their clothes.
(b) The Pharisee who were mosaic scholars indicted Jesus for blasphemy charges.

Luke 5: 21 And the scribes and the Pharisees began to reason, saying, Who is this which speaketh blasphemies? Who can forgive sins, but God alone?
 
Hakuna sheria hapo mmekosa kazi nyie.
Mnashindwa kumshtaki Muhammad ambae amevunja sheria nyingi na Ame abuse haki za watoto mnakimbilia kwa Yesu Kristo. Mnaakili kweli?
 
Who is lawyer among of you

mkuu nafikiri kuna kitu hujakielewa vizuri, ebu niulize nikujibu.

na hapa tunaongelea sheria za kuendesha mashauri kwa wayahudi,wakati wa Yesu. Si sheri za Israel sasa ivi
 
It is a lie.

Jesus was not poor. He had 12 people working for Him. Nonetheless, He had a personal accountant. You don't have that.

Can a poor man be able to employ 12 people who were business men and an accountant?

personal accountant alikuwa nani?ingekuwa vipi MPESA na Tigopesa zingekuwa kipindi kile,yuda msaliti angetumiwa pesa za kumsaliti kwenye simu yake,na yesu angekuwa anatumia simu gani.na ngekuwa anaendesaha gari gani
 
(mode hii ni ya ki intelijensia zaidi, usiihamishe plse)

Usiku Yesu alipokamatwa alifikishwa mbele ya wafuatao kwa mashtaka, Caiaphas - Kuhani mkuu (na aliye agiza yesu akamatwe na pia ndiye aliandaa mashtaka), Annas - Kuhani mkuu mstaafu, na Sanhedrini - Baraza la makuhani. Kwa kuwa hawa ni viongozi wa kidini Yesu hapa alishtakiwa kwa makosa mawili;

1. Kufuru (blasphemy), 2. Kajitangaza kuwa ni mwana wa Mungu na Messiah

Baadaye akapelekwa kwa kwa Pilato, na huko mashtaka ghafla yakabadilika na kuwa matatu yafuatayo;

- Kutaharakisha jamii na kusababisha uasi (rioting)
- Kukataza watu kulipa kodi
- Kujitangaaza kuwa ni mfalme wa wayahudi (uhaini).

Makosa haya chini ya utawala wa Rumi adhabu yake ni kifo;

Hapa tunaona mashtaka yanabadilishwa kwa sababu nia ya Caiaphas ilikuwa yesu afe na kwa kuwa bataza la makuhani halina mamlaka ya kutoa hukumu ya kifo na pia mashtaka ya kwanza hayakuwa na mashiko wala hayakuwahusu watawala (Rumi), akaona ni vyema abadilishe mashtaka ili apate uhalali wa kumfikisha yesu mbele ya pilato (Gavana) na pia apate hukumu ya kifo.

Kumbuka yesu alikamatwa na askari wa hekalu (temple guards) kwa maagizo ya caiaphas na si askari wa utawala wa Rumi

Kesi ya Yesu chini ya viongozi wa kidini (kuhani mkuu na baraza la makuhani) iligubikwa na uvunjifu wa sheria za kiyahudi katika hali ya juu na waziwazi kiasi cha kutisha. Yafuatayo yalikiukwa kwa mujibu wa sheria za wayahudi za wakati huo;

1. Haikuruhusiwa kesi/shauri lolote kuendeshwa wakati wa sikukuu au maandalio ya sikukuu (No trial was to be held during feast time) lakini haohao viongozi wa sheria za kiyahudi waliendesha shauri la yesu wakati wa sikukuu ya pasaka

2. Kila mjumbe wa baraza alipaswa kupiga kura binafsi wakati wa maamuzi yeyote ya hukumu ( Each member of the court was to vote individually to convict or acquit) lakini yesu alihukumiwa kwa kura ya pamoja (but Jesus was convicted by acclamation.)

3. Kama mtu akihukumiwa kifo, hukumu hiyo itatekelezwa siku ifuatayo (If the death penalty was given, a night must pass before the sentence was carried out) lakini yesu alihukumiwa na hukumu ilitekelezwa muda mfupi tu baada ya hukumu kutolewa.

4. Wayahudi hawakuwa na mamlaka ya kutoa hukumu ya kifo, lakini hukumu ya yesu ilipendekezwa na wayahudi na wakampeleka kwa pilato kuomba ruhusa ya utekelezaji (The Jews had no authority to execute anyone.)

5. Haikuruhusiwa shauri lolote kuendeshwa wakati wa usiku (No trial was to be held at night) lakini shauri la yesu liliendeshwa usiku.

6. Mtuhumiwa yeyote alipaswa kupewa uwakilishi na uhuru wa kuleta mashahidi ( The accused was to be given counsel or representation) lakini yesu hakupewa nafasi hii.

7. Mashtaka ya mtuhumiwa yalipaswa kubakia hayo hayo katika kila hatua ya kesi, lakini yesu mashtaka yake yalibadilika kila stage ya kesi.

Kimsingi kesi ya Yesu ndo kesi iliyoongoza kwa uvunjifu wa sheria na utaratibu wa kuendesha mashauri na kesi na rekodi hiyo haijavunjwa mpaka leo.

Note: Uchambuzi huu ume base kutoka, (John 18:19-24; Matthew 26:57, John18:23, Luke 23:7, Luke 23:11-12, John 18:28, Luke 23:7, Luke 23:11-12, Luke23:25 na sheria za kiyahudi ni kwa mujibu wa mwanahistoria na mwandishi nguli Josephus aliyeishi wakati wa Yesu.)

mwanahistoria Josephus hakuishi kipindi cha Yesu.

Mgawanyo wa mamlaka kati ya Roma kuu na Uyahudi haukuwa kwenye mstari mnyoofu kama unavyopendekeza uonekane achilia mbali sheria za Uyahudi kama dini na jamii.
 
mwana historia josephus aliishi wakati wa yesu...that's a fact.

unaposema mgawanyo wa madaraka unamaanisha nini??
 
rejea kesi ya paulo na utambulisho wake wa kirumi.
Mfumo wa sheria za Rumi kuu ulisheheni busara za kupindukia, utawala wao ulikuwa wa kiuchumi pale wanapokuta jamii iliyojengeka kiustaarabu mf. Uyahudi, wataweka shinikizo kwenye uongozi wa juu wa jamii k.m. Mfalme n.k. kisha kuiacha jamiii ijiendeleze kwa sheria zake zisizopinga Rumi kuu kwa ngazi ya tuseme mahakama ya mwanzo; kwa ufupi juu ya mgawanyo wa mamlaka/madaraka.

Huyu mwanahistoria aliishi angalau vizazi viwili baada ya Yesu "hii ni fact".
 
sioni kama kuna tatizo kati ya unachosema kuhusu utawala wa rumi vs uyahudi na point nilizo raise, mimi nimezungumzia jinsi kuhani mkuu na senhedrin "balaza la makuhani" walivyo vunja sharia za kiyaudi katika kuendesha mashtaka ya yesu. kumbuka dola ya rumi hawauwa na interest na yesu kabisa. Wala Pontius Pilate hakumfahamu yesu kabla.

Kuhusu, Josephus, katika vitabu vyake (mkusanyiko wa maandiko yake) na pia ushahidi mbalimbali unathibitisha kuwa aliishi wakati wa yesu, na wakati pilato akiwa gavana wa Judea. Nakulete proof ya hili
 
Back
Top Bottom