Akili ming
New Member
- Aug 27, 2022
- 1
- 1
Inawezekana ikawa mfumo wa elimu Tanzania ni mzuri kwa wengine Ila kwangu mimi mfumo huu unamapungufu mengi Na ulinifanya niteseke kwa miaka 7 nikitafuta maisha.
Nitasimulia Hadithi ya maisha yangu .
Mimi nimezaliwa mkoa wa Kagera ,wilaya Ya Bukoba vijijini.Nimesoma Elimu ya msingi mwaka 2003-2009.
Baadae nilijiunga Na sekondari nikafanikiwa kuitimu mwaka 2014.
Nilipokuwa nasoma sekondari (o-lever) Nilianza kuvutiwa na masomo ya computer hasahasa biashara mtandao (internet business).
Nilifanikiwa kufungua Blog ya habari na Kweli ilikuwa inawatazamaji na wasomaji wengi ingawa sikuweza kupata mafao (money) kwa sababu sikujua kama kitu kile kinaweza kulipa Pili sikuwa Na pesa ya kununua computer kupata uwezo wa kuchapisha machapisho mara kwa mara na Hii ni kwa sababu familia yangu ni maskini, kwahyo ilinibidi niende kwenye mighawa ya internet (internet cafe) kuweza kupata huduma.
Kipindi chote hicho nilikuwa nasubiria matokeo ya kwenda kusoma Advansi ( high school), matokeo yalipotoka nikawa nimechaguliwa kusoma mchepuo ya PCB ( physics, biology and chemistry),
Kitu ambacho sikupenda kabisa ila nilitaka kujua shule niliyochaguliwa ili nikabadilishe mchepuo, nilitaka nikasome mchepuo wowote utakaoniwezesha kusoma computer kwa maana nilikuwa nimeshapenda na kuzama kimazima kwenye masomo ya computer.
Nilipofika advansi nikawa sijapata uwezekano wa kusoma kozi za computer kwa sababu hiyo shule haikuwa Na mchepuo wowote unaohusu computer.
Nikapiga moyo konde Na kujiapia kusoma kwa bidii ili niweze kufaulu kwenda chuo kikuu ili niweze kujichagulia cha kusoma Na hiyo itakuwa computer.
Huwezi kuamini kipindi cha likizo nilikuwa nashinda maktaba za wilaya ili niweze kuongeza Ujuzi wa computer,nikajikuta nimesoma lugha za computer bila ata kuwahi kugusa keyboard kuandika code.
Yaani nilijikuta ninamaaba makubwa Na coding Na kuanza kusoma kuhusu masoko ya internet.
Basi nilipomaliza shule ya sekondari (high school) nilifaulu kwa daraja la Pili.
Kwa hiyo ikabidi niombe chuo pamoja kozi ya kusoma.
Kwa kipindi kile tulikuwa tunaomba kupitia TCU.(mamlaka ya vioo vikuu Tanzania).
Hapa ndo nilipopigwa za kichwa kwa maana niliomba kozi za computer nne na kozi moja Ya sayansi ya mimea pamoja Na chuo cha dar es salaam.
Kwa bahati nzuri nilichaguliwa chuo cha dar es salaam ila kwenye kozi ya sayansi ya mimea (botanical science). Jambo hilo liliniuma sana ila nikajiapia kwenda kubadili kozi nikifika chuoni.
Nilipofika UDSM nikaomba kubadili kozi kwa mara ya kwanza nikakataliwa,nikaomba mara pili nikakataliwa ikabidi nisome ivo ivo kwa shinikizo la wazazi nyumbani maana walikuwa wanasema niachane na mambo ya computer.
Huwezi amini kitu nilichaguliwa nilikuwa sikipendi, semister ya kwanza nilijitahidi kidogo ila semister ya Pili ilishindikana Kwahyo nikadisco chuo mwaka wa kwanza.
Cha ajabu semister ya Pili nilikuwa nimefanikiwa kufungua website ya kuuza bidhaa mtandao (e-commerce website). website niliitengeneza mwenyewe ,ule muda wakwenda discussion na kusoma material mimi nilikuwa busy kusoma computer.
Baada ya kudisco chuo kikuu ilinibidi niende mtaani,kumbuka mjini sina ndugu wala sina pesa ya kuanza maisha,yaani ndo mwanzo ambao sitakuja kuusau maana niliishi maisha ya tabu sijawah kuona.
Nilienda kukaa kwa mshikaji Wangu ambae alikuwa anasoma chuo cha Elimu DUCE ,sikutaka kurudi nyumbani kwa maana sababu iliyonifanya nidisco chuo nilikuwa naidai ilikuwa inabidi inilishe na kunipa maisha ya kuishi mjini.
Kumbuka mjini ndo nilikuwa na mwaka mmoja sijui chaka wala sina connection yeyote.
Niliteseka sana nikawa kama ombaomba kwa washkaji niliowaacha chuo ingawa wengi walinikataa,nikawa mtoto wa uswahilini.kitu ambacho nilijifunza ni kuwa kuna elimu mbili ya shule Na ya mtaani ukimlea mwanao mfundishe Elimu zote.kitaa (mtaa) kinaitaji Elimu ambayo sio ya shule Na hii unaipata kwa kupata uzoefu mtaani,ndo maana mhua (mkopesha vyombo mjini) anaweza kuishi mjini bila mshahara.
Navyokwambia nimeteseka kwa zaidi ya miaka mitatu,nimeomba sana kazi ili nijipatie kipato hakuna kitu pamoja nakuwa Na vyeti, ilifika mahala nikatembeza pipi Na sigara mtaani, ila sikuwai kujutia uamuzi wangu wa kudisco kitu ambacho kilikuwa nakidai ni computer, kila siku nilijiamba kwamba computer inatakiwa kunilipa Na kunifanya bilionea.
Basi mambo yaliendaa hivohivo baadae mungu alisaidia nikaanza biashara za online ,nilipoanza biashara za online nikaanza kupata mafanikio ,unajua ni kwanini?,nilifanya biashara mtandao huku nikichanganya Na ujuzi wa masoko niliowahi kusoma/kujifunza nyuma.kumbe nilikuwa Na madini ambayo yamechanganyika na mchanga.
Tunavyoongea sasa hivi nina duka kubwa tu la kuuza bidhaa, pia nina webiste ya mauzo ya online. Soon nitafungua kampuni yangu.
Kwa Kutumia hadithi yangu hapo juu, haya hapa ni baadhi ya mapungufu ya mfumo wa Elimu Tanzania.
1: Mwanafunzi kutopewa uhuru wa kusoma kile anachopenda (ingawa nasikia siku hizi mifumo ya udahiri imebadilika)
2: Mfumo kutokujua soko la ajira linataka nini. (ukimshindanisha Mkenya Na mtanzania katika interview kivyovyote mtanzania atashindwa)
3: Mfumo kutozingatia zaidi practical badala ya nadharia (theory)
Dunia yetu inaenda kwa kasi, mwanafunzi anaitaji kufanya practical nyingi zaidi kusoma nadharia, shuleni watu wanashindana kufaulu mtihani
4: Mfumo hauruhusu ubunifu (wabunifu wengi nchini Tanzania hawaeshimiwi wala kutengenezewa njia za kufikia ndoto zao na hii inaanzia shuleni, yule mbunifu hatengenezewi njia)
5; Ukosefu wa shule nyingi za Tehama.
Mimi nimeteseka na kushindwa kufikia ndoto zangu mapema kwa sababu shule nilizosoma zote hazikuwa Na tehama.
6: Kutoweka masomo ya tehama kama masomo ya kimkakati.
Sio lazima ujenge shule ya tehama Ila kunaweza kuweka mkakati wa shule zote kufundisha tehama kwa kila mwanafunzi kwa maana dunia inaitaji computer ili iweze kwenda kwa sasa.

Upvote
1