Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Jeshi la Polisi mkoani Mara linawashikilia watu 18, wakiwemo dereva, kondakta na abiria 16, kwa tuhuma za kumpiga askari wa usalama barabarani aliyekuwa akikagua gari walilokuwa wamepanda. Tukio hilo lilitokea Septemba 18, 2024, saa 12 jioni katika mkoa wa Mara.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Ofisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Trafiki Kuu, Butusyo Mwambelo, amesema kuwa askari huyo alikumbwa na kipigo wakati akijaribu kushusha abiria waliokuwa wamesimama kwenye gari. Hata hivyo, kondakta wa gari hilo alifunga mlango na wote waliokuwa ndani ya gari, akiwemo dereva, kondakta, na abiria, walianza kumshambulia askari huyo.
“Askari wetu alikuwa akitekeleza wajibu wake wa kuwataka abiria waliokuwa wamesimama kwenye gari washuke. Lakini ghafla walimzonga kwa maneno ya kebehi, na kondakta kufunga mlango wa gari. Ndipo dereva, kondakta na abiria wao wakaanza kumpiga askari akiwa ndani ya gari. Je, kweli tumefika hatua hiyo kama Watanzania?” alisema Mwambelo.
=============
Wananchi wanahasira sana hadi kufikia hatua ya kumtwaga askari mh tunapoelekea sasa ni balaa tupu!
Soma Pia: Abiria watakiwa kupaza sauti kwa Madereva wasiofuata Sheria za Usalama Barabarani