Mara: Bibi kizimbani kwa tuhuma za kumuua mjukuu kwa kutumia Tsh. 2,000 bila ruhusa

Mara: Bibi kizimbani kwa tuhuma za kumuua mjukuu kwa kutumia Tsh. 2,000 bila ruhusa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Nkwandu Kayenze (76) Mkazi wa Kijiji cha Natta Wilayani Serengeti mkoani Mara amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Serengeti kwa tuhuma ya mauaji ya mjukuu wake Matoja Deus (11) ambaye anadaiwa kumpiga hadi kufa baada ya kutumia Shilingi 2,000 bila idhini yake.

ITV
 
Miaka 76 unapata kesi ya kuua? Dah hatari sana.

Ila haya mambo ni kama pepo.

Kuna kipindi mama yangu alikuwa anaumwa tukawa tunachangishana ndugu apelekwe india mwezi unaofata. Na alikuwa mtumishi wa uma. Kuna binti mtoto wa mama yangu mdogo akamshauri waende kwa mganga wa kienyeji. Mama akaenda bank akakopa milioni 8 kimya kimya kisha wakaenda kumlipa mganga wa kienyeji huyo.

Yaani nilivyogundua nilitamani nimkate panga huyo binti wa mama yangu mdogo na mama pia. Japo deni lilikuwa lake mama. Mganga kapiga piga ramli feki akacheza na saikolojia yao tu akamwambia mama amerogwa na dada yake huku ukweli mama alikuwa na kansa. Kisha akavuna milioni 8 zote

Kilichofata akawa hana hela ya kula sababu ya deni la malipo ya mganga. Yaani watoto wake ndie tumtunze mama huku yeye ana ajira kabisa na wanae tunaunga unga kipindi hicho

Haya mambo yasikie tu. Si ajabu huyo bibi hiyo 2000 aliipata kwa shida sana. Na shetani akamuingia siku hiyo ikawa balaaa
 
Miaka 76 unapata kesi ya kuua? Dah hatari sana.

Ila haya mambo ni kama pepo.

Kuna kipindi mama yangu alikuwa anaumwa tukawa tunachangishana ndugu apelekwe india mwezi unaofata. Na alikuwa mtumishi wa uma. Kuna mama yangu mdogo akamshauri waende kwa mganga wa kienyeji. Mama akaenda bank akakopa milioni 8 kimya kimya kisha wakaenda kumlipa mganga wa kienyeji huyo.

Yaani nilivyogundua nilitamani nimkate panga huyo mama yangu mdogo na mama pia. Japo deni lilikuwa lake mama.

Haya mambo yasikie tu. Si ajabu huyo bibi hiyo 2000 aliipata kwa shida sana. Na shetani akamuingia siku hiyo ikawa balaaa
Hii dunia ukipumzika kumcha Mungu tu ndipo hapo shetwani anajitwalia point 3, ila kwa neema zake Mungu huwa tunawezeshwa kuvuka mitihani mikubwa sana.

Lakini wakati mwingine unaweza jikuta unapita mahali pagumu ukikokotoa mahesabu kwa akili za kibinadamu unagundua haiwezekani hata kwa 0.0001%, pia kukumbukwa kimaombi na watakatifu wa Mungu bila muhusika kutambua huwa kunatuweka karibu na Mungu zaidi kiwokovu.
 
Sidhani kama dhamira yake ilikuwa kuua ndio mana hata kupigana na mtu ni hatari. Labda mtu ana ugonjwa fulani, unampiga kidogo , anakufa.
 
Aisee!! Hapo kabakia na majuto tu.

Na kwa umri wake kakipande ka uhai wake kalikobakia anaenda kukamalizia jela.
 
Back
Top Bottom