Miaka 76 unapata kesi ya kuua? Dah hatari sana.
Ila haya mambo ni kama pepo.
Kuna kipindi mama yangu alikuwa anaumwa tukawa tunachangishana ndugu apelekwe india mwezi unaofata. Na alikuwa mtumishi wa uma. Kuna mama yangu mdogo akamshauri waende kwa mganga wa kienyeji. Mama akaenda bank akakopa milioni 8 kimya kimya kisha wakaenda kumlipa mganga wa kienyeji huyo.
Yaani nilivyogundua nilitamani nimkate panga huyo mama yangu mdogo na mama pia. Japo deni lilikuwa lake mama.
Haya mambo yasikie tu. Si ajabu huyo bibi hiyo 2000 aliipata kwa shida sana. Na shetani akamuingia siku hiyo ikawa balaaa