Mara: Mkuu wa Mkoa ashangaa Wanafunzi wa Darasa la 7 kutowafahamu Waziri Mkuu na Rais wa Zanzibar

Mara: Mkuu wa Mkoa ashangaa Wanafunzi wa Darasa la 7 kutowafahamu Waziri Mkuu na Rais wa Zanzibar

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Kiongozi huyo wa Mkoa, Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee ameyaeleza hayo wakati akizungumza na Walimu wa shule tofauti Mkoani hapo.

Amesema amewauliza wanafunzi wengi na wameonekana hawana ufahamu juu ya Sikukuu ya Mapinduzi, kutomfahamu Waziri Mkuu wa Tanzania wala Rais wa Zanzibar.

Amesema “Nimezunguka shule tatu tofauti nimepata mmoja tu ndio mjanja nikampa na Tsh. 10,000. Mtoto wa Darasa la Saba, mwaka huu anafanya mtihani kuhingia kidato cha kwanza lakini hana historia ya Nchi yetu, inaumiza.

“Tusiishie uangalia tu madaftari na sare za shule, nyie ni walimu, hii ni aibu.”

Chanzo & Video: Jambo TV
 
😂😂😂 Kuna watu watakuja hapa kulaumu mfumo wa elimu ya TZ.

Kujifunza siyo shuleni tu, ukitoa cartoon watoto wa siku hizi hawafuatilii sherehe za kitaifa ambazo mara nyingi unaweza kudaka vitu baadhi muhimu, kama kujua viongozi, historia ya taifa n.k.

Pia usomaji wa mageziti (siyo ya udaku) ni muhimu. Nakumbuka kipindi naanza kujifunza kusoma, mazoezi mengi nilifanya kupitia magazeti.

Mkuu wa mkoa kasema vizuri, wazazi nao suala la elimu wamewatupia walimu tu.
 
Sijaiangalia hiyo video lakini nataka nijue kama kweli RC amewauliza hao wanafunzi juu ya waziri mkuu wa zanzibar
Duuuh! ungekua mwanafunzi ungetoka droo na mwanafunzi aliyetaja embe kama tunda moja wapo la mapinduzi.Ni wewe tu na baadhi ya wanafunzi ndiyo mnajua Zanzibar wana waziri mkuu,na siyo wa JMT tu.
 
Mitaala wameiandaa wao..... Sasa hivi tuna kizazi cha hovyo hovyo sana
 
Duuuh! ungekua mwanafunzi ungetoka droo na mwanafunzi aliyetaja embe kama tunda moja wapo la mapinduzi.Ni wewe tu na baadhi ya wanafunzi ndiyo mnajua Zanzibar wana waziri mkuu,na siyo wa JMT tu.
Naona kama umekurupuka hivi. Kutaka kwangu kujua ni kutokana na heading ya mada ambayo inasema

"Mara: Mkuu wa Mkoa ashangaa Wanafunzi wa Darasa la 7 kutowafahamu Waziri Mkuu na Rais wa Zanzibar " s​

[emoji23][emoji23][emoji23] Kuna watu watakuja hapa kulaumu mfumo wa elimu ya TZ.

Kujifunza siyo shuleni tu, ukitoa cartoon watoto wa siku hizi hawafuatilii sherehe za kitaifa ambazo mara nyingi unaweza kudaka vitu baadhi muhimu, kama kujua viongozi, historia ya taifa n.k.

Pia usomaji wa mageziti (siyo ya udaku) ni muhimu. Nakumbuka kipindi naanza kujifunza kusoma, mazoezi mengi nilifanya kupitia magazeti.

Mkuu wa mkoa kasema vizuri, wazazi nao suala la elimu wamewatupia walimu tu.
Watafuatilia vipi wakati budget zake hutumika kwenye matumizi mengine. Hii ndio athari ya kupuuzia mambo ya kitaifa. Zamani wakati nasoma siku ya uhuru na siku nyingine tunaimba na nyimbo kabisa tukikutana shule tofauti. Siku hizi hamna hizo mambo
 
Naona kama umekurupuka hivi. Kutaka kwangu kujua ni kutokana na heading ya mada ambayo inasema

"Mara: Mkuu wa Mkoa ashangaa Wanafunzi wa Darasa la 7 kutowafahamu Waziri Mkuu na Rais wa Zanzibar " s​

Waziri mkuu ni mmoja tu, ndiyomaana kaandika waziri mkuu,ila kwa Rais,akaspesholaizi wa Zanzibar.Anyway have a gud moment.
 
Waziri mkuu ni mmoja tu, ndiyomaana kaandika waziri mkuu,ila kwa Rais,akaspesholaizi wa Zanzibar.Anyway have a gud moment.
Hivi nikisema 'Baba na mama Amina wanakuja' hivi maana yake ni baba juma na mama Amina au baba Amina na mama Amina ? Soma heading vizuri compare na mfano wangu ndio ujibu
 
Back
Top Bottom