Mara: Mkuu wa Mkoa ashangaa Wanafunzi wa Darasa la 7 kutowafahamu Waziri Mkuu na Rais wa Zanzibar

Mara: Mkuu wa Mkoa ashangaa Wanafunzi wa Darasa la 7 kutowafahamu Waziri Mkuu na Rais wa Zanzibar

Hao wanafunzi sio observational.

Itakuwa huwa wanasikia redioni ila hawatilii maanani.

Kuna vituo huwa havifundishwi shuleni,ili kuvijua inakuhitaji kuwa msikivu ukiwa unaongea na watu,ukisikiliza redio,luningani na kadhalika.
 
Kujifunza siyo shuleni tu, ukitoa cartoon watoto wa siku hizi hawafuatilii sherehe za kitaifa ambazo mara nyingi unaweza kudaka vitu baadhi muhimu, kama kujua viongozi, historia ya taifa n.k.

VIPINDI MAALUM VYA UZINDUZI, MAPOKEZI, MIKUTANO YA CCM N.K KTK KITUO CHA TELEVISHENI TBC VIFUTWE.

Huu ni ushahidi kuwa CCM na serikali yake imepuuzwa na familia nyingi Tanzania.

Ina maana TBC pamoja na kuweka vipindi vya ghafla virefu ktk TV kuhusu Kuapishwa kwa Viongozi vigogo Ikulu, mafanikio ya miradi ya kimkakati ya serikali ya CCM au uzinduzi wa kipande cha reli SGR DSM MORO, uchaguzi unaofanywa na Halmashauri haufuatiliwi na watanzania walio wengi.

 
Kiongozi huyo wa Mkoa, Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee ameyaeleza hayo wakati akizungumza na Walimu wa shule tofauti Mkoani hapo.

Amesema amewauliza wanafunzi wengi na wameonekana hawana ufahamu juu ya Sikukuu ya Mapinduzi, kutomfahamu Waziri Mkuu wa Tanzania wala Rais wa Zanzibar.

Amesema “Nimezunguka shule tatu tofauti nimepata mmoja tu ndio mjanja nikampa na Tsh. 10,000. Mtoto wa Darasa la Saba, mwaka huu anafanya mtihani kuhingia kidato cha kwanza lakini hana historia ya Nchi yetu, inaumiza.

“Tusiishie uangalia tu madaftari na sare za shule, nyie ni walimu, hii ni aibu.”

Chanzo & Video: Jambo TV
Inasikitisha watoto wako makini kwenye singeli, bongofleva,, taarabu, vigodoro na tamthlia za kichina lakini hawajui chochote kuhusu masomo. Kuna shida mahali sio bure!
 
Kwani Zanzibar Kuna cheo kinaitwa waziri mkuu?
Kule kuna makamu wa kwanza wa rais na makamu wa pili wa rais; hakuna waziri mkuu kiongozi. Kwani mwanafunzi aliuliza waziri mkuu wa Zanzibar?
 
Sijaiangalia hiyo video lakini nataka nijue kama kweli RC amewauliza hao wanafunzi juu ya waziri mkuu wa zanzibar
Unashangaa watoto na huyu je wazir mkuu WA Zanzibar!!!??? Hii nchi Kuna shda hasa[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom