Mara ngapi umekutana na mtu uliyedhani amefariki kitambo? Na nini ulifanya?

Mara ngapi umekutana na mtu uliyedhani amefariki kitambo? Na nini ulifanya?

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Sizungumzii misukule kama ile ya mikoa ya kanda ya ziwa ambapo watu huzika mtu halafu akaokotwa baada ya muda miji ya mbali.

Nazungumzia vile hujamuona mtu fulani au mzee wa eneo bila kuuliza au bila kupata habari zake kiuhakika baadae ukamuona siku ya siku kwenye mishughuliko yake.

Vile vile nazungumziaj pale anapotkea mtu akatoa taarifa ya kifo cha mtu fulani na kwa wasifu wake huo ukatosheka kuwa ni mtu fulani unayemfahamu. Lakini ya miezi au miaka ukakutana naye tena njiani au sokoni.

Kama imewahi kukutokezea hiyo kama ambavyo imenitokezea mimi mara nyingi nini ulifanya kwa huyo mtu ujliyejenga sura kuwa tayari ni mchanga.
 
Kwan we uliifanyaje ulipo waona?
Siku hiyo nilipata taarifa za kifo cha mwenzetu mmoja na mtani wangu wakati niko safarini.Nikarudi haraka kijijini kushiriki mazishi.Bila kuuliza zaidi nikakuta watu wameshafika makaburini.
Kumaliza mazishi tunatoka kuna mtu akanipiga begani kiutani.Vipi Ami salama ?.Sauti niliyosikia ikanishangaza.Kugeuka ni yeye.
Nikamwitikia tu salama na sikutaka kuongeza neno.Kumbe aliyenitaarifu hakukusudia utani isipokuwa na yeye alipokea habari kimakosa na akafanya haraka kunipa taarifa.
 
Kuna siku nyengine nilipata taarifa ya jamaa aliyefariki na alikuwa mshirika wangu sana kwenye shughuli za kujitafutia riziki.Aliyenipa taarifa nikamuuliza vizuri isiwe amemchanganya na mtu mwengine.Akinihakikishia ni yeye yule na kunipa alama zote mpaka nikaridhika kweli ni yeye.Baada ya miezi kama mitatu hivi akajitokeza tena kwangu kufuata huduma.Nikamsaidia shida yake huku nikimuangalia vizuri usoni.Kwa hakika alikuwa yule yule lakini sikutaka kuongeza neno.Baada ya hapo tumeshakutana tena mara nyingi tu.
 
K

Kwahio hukustuka?🤔🤔🤔
 
K

Kwahio hukustuka?🤔🤔🤔
Nilishangaa na kushukuru Mungu tu.Sikushtuka na sikutaka nimshtue yeye mwenyewe.
Ningeshtuka kama ningemuona na dalili ngeni kwenye mwili wake.Lakini alikuwa yule yule na hata nguo ni zile zile nilizomzoea nazo akizivaa.
 
Hii hutokea sana kwa wale ambao tunakuwa mbali na nyumbani. Utasikia leo kulikuwa na msiba wa fulani. Unasikitika na maisha yanaendelea.

Unarudi, ghafla unakutana naye. Unaanza kurecall taarifa uliyopewa kuwa alifariki. Huo mshtuko ni mkali sana.

Lakini, kuna mmoja nilijichanganya mwenyewe. Kuna mzee alikuwa ni mgonjwa haswa. Lakini wapo na wengine kwenye familia yao.

Sasa nikapokea taarifa kuwa mzee wa familia ya fulani kafariki. Pasipokujiuliza nikajihitimishia kuwa ni yule mzee mgonjwa katuponyoka. Nikasikitika na kumuombea pumziko jema.

Nilikaa muda kama miezi nane sijarudi. Niliporudi, nikasema niende kutoa pole kwa familia. Ile nafika anayenipokea ni yule mzee niliyedhani kafariki, akiwa na unafuu mkubwa. Nipo kwenye gari najitafakari kushuka, mzee ananiangalia tu.

Isingelikuwa mke wake kutoka, wala nisingeshuka.
 
Kuna familia moja kilikuwa na vijana (watoto wao)tulikuwa tunakaa wote jirani miaka ya 90 mwanzo na wakahama mwanzoni mwa 2000 so tukaja kusikia Mmoja Wa wale vijana (Rika yetu) amefariki Wa wamezika huko kwao Shinyanga. Ikapita miaka zaidi ya 15 ,Kuna Siku mwaka 2015 napita Mbezi kwa Zuwena nakuta Jamaa yupo getini Security anafanana na mshikaji,ikabidi nipark gari pembeni nimfuate,aliponiona yeye mwenyewe akaniita kwa jina langu la Mtaani,nikamsalimia na akaanza kunipa story ya Familia Yao,kumbe aliyefariki ni dada yake so watu walichanganya na kudhani ni yeye.
Kila mara nikipita pale huwa tunasalimia ,akaja poteza simu na pale akahamishwa ,sijawahi kumuona tena tokea 2017 mpaka Leo hii
 
Kuna mwamba alimpiga bos wake kama mil 15 hiv akakimbilia kwa madiba kusikilizia akapata taarifa kwamba bos wake bado anamtafuta aka-fake kifo cha ajali na ikaonekana amezikwa huko huko south ili kuwapoteza maboya ndugu na jamaa kweli wakajua hivyo yule bos alivyosikia akaita wapambe wake akafanya sherehe ya kula na kunywa kufuraia kifo cha jamaa, huko south jamaa kapambana mkwanja ukaongezeka maradufu hiyo ilikuwa miaka ya 2000 mwaka 2017 jamaa akadondoka bongo akamkuta bos wake kachoka mbaya....
 
Amlipe boss wake wa zamani hela alizoiba ili wayamalize coz kesi bado ipo pale pale tu,amlipe jamaa ili aishi kwa amani zaidi,kama Boss wake kachoka basi hata yeye inawezekana akaja kuchoka pia japo simuombei afike huko.
 
Kilichotokea ni kuwa boss alikuwa bandidu Kila mzunguko was biashara jamaa alitakiwa alipwe mil 2 akulipwa mpaka ikafikia mil 6 Kila akiomba chake boss anasema atampa huku akiendelea kumtumia kwenye issue zake za biashara round ya mwisho ndo hivo jamaa akapita mazima
 
Kwanini unaamini kua ni lazima kila mtu imtokee?

Mimi haijawahi kunitokea.
Ikiwa haijakutokezea itakuwa ndo kwanza unamaliza darasa la saba au ni mtu usiyependa kuchanganyika na watu.
 
Back
Top Bottom