Mara ngapi umekutana na mtu uliyedhani amefariki kitambo? Na nini ulifanya?

Mara ngapi umekutana na mtu uliyedhani amefariki kitambo? Na nini ulifanya?

Mzee huyu Mungu amrehemu
Ni mzee sana na mara nyingi nikifikiria watu wanaoandika historia hutamani wangefanya mahojiano naye mapema.Alikuwa ni mtumishi wa serikali na mcheshi sana na hodari wa kuzungumza na vijana.
Mara ya mwisho nilipoonana naye aliniambia anaumwa sana na anamsubiri mwanawe ampeleke hospitali ya rufaa.Nilipokuwa simuoni muda mrefu nikadhani ndio keshatangulia tena.Sikuwa na mtu wa kumuulizia habari zake.Miaka kadhaa ikapita.Siku hiyo ghafla nikaonana naye.Kwa furaha wala sikukumbuka kuchukua mawasiliano yake ili niwatume vijana wangu kwake. Miaka kadhaa imepita tena.Sijui kama tutakutana tena hpa duniani.Na kama nikikutana naye basi siku hiyo sitomuachia aende peke yake kwake.
 
Sizungumzii misukule kama ile ya mikoa ya kanda ya ziwa ambapo watu huzika mtu halafu akaokotwa baada ya muda miji ya mbali.

Nazungumzia vile hujamuona mtu fulani au mzee wa eneo bila kuuliza au bila kupata habari zake kiuhakika baadae ukamuona siku ya siku kwenye mishughuliko yake.

Vile vile nazungumziaj pale anapotkea mtu akatoa taarifa ya kifo cha mtu fulani na kwa wasifu wake huo ukatosheka kuwa ni mtu fulani unayemfahamu. Lakini ya miezi au miaka ukakutana naye tena njiani au sokoni.

Kama imewahi kukutokezea hiyo kama ambavyo imenitokezea mimi mara nyingi nini ulifanya kwa huyo mtu ujliyejenga sura kuwa tayari ni mchanga.
Sjawah kwakwel mazeeh
 
Mimi nishawahi kukutana na hio scenario dogo mmoja kitivo akamwambia rafiki yangu mmoja eti yule brother anafanana na brother wangu aliyekufa kila akiniona nikajua labda alikuwa anampenda sana brother wake ila akiona wengine anahisi ghost wake
 
Tangu udogoni nlikuwa mtu wa shule na nasoma shule za mbali kidogo na home nikawa siwajui baadhi ya wanakijiji vzr nkiambiwa flan kafariki hua naitikia tu lkn nakua simjui vzr! Likizo moja hv nlienda stendi nkachelewa kurudi njiani nikakutana na jamaa moja umri wa makamo hv akili yangu inanambia huyu mtu alishafariki nlivomkaribia mwili ukasisimka nlitoka nduki kinoma nlipita kwenye pario Moja la hatar Lina giza kinoma kadri navokimbia nahis kama ananikimbiza😁
 
Wakati nipo shule ya msingi kuna jamaa yangu baba yake alikuwa hataki jamaa asome.
Basi yule mzee kipindi cha likizo anamchukia jamaa'ngu akampeleka vijijini huko ndanindani akamuacha akae na bibi yake ili amsaidie kazi za shamba na kuuza mazao ili aishi huko.
Shule zikafunguliwa mwamba hatumuini shule, mara paap mzee wake akaja akasema jamaa yetu alishafariki na wameshazika huko kijijini😅
Basi tukatangaziwa pale shule, maninja tukasikitika sana mwisho tukamuombea Sir God ampokee mwanetu huko alipo.

Kumbe kule kijijini jamaa anashangaa mbona mzee wake haendi kumchukua, jamaa akajichanga akapata kinauli akarudi.
Asubuhi tupo darasani tunamsubiri mwalimu wa somo, tunakuta mwamba huyo anaingia klasi kama vile katoka kufufuka kama masia.
Ile jamaa anakaa tu kwenye deski watu wote nduki, akajikuta yupo peke yake darasani.
Tukaenda kumuita mwalimu, akaja darasani, ndio jamaa akampa kisa chote jinsi mzee wake alivyomfanyia
 
Visa vya kweli vyote.Kama hayajakutokea soma wenzako wanavyofunguka.
Nilipokuwa mdogo nilikuwa na rafiki yangu kipenzi na mcheshi sana.Mimi nilichaguliwa kusoma sekondari shule moja ya mbali mkoa mwengine.Siku chache baada ya kurudi kwa ajili ya mapunziko mara ya mwanzo yule rafiki yangu akapata homa kidogo na baba yake akampeleka hospitali.Usiku tumelala ikaingia gari na maiti yake.Ilikuwa huzuni kubwa kwa kila mmoja pale kijijini.Mimi ilikuwa ni huzuni na hofu kubwa kwani ilikuwa mara ya mwanzo kushuhudia mtu wa karibu yangu kufa.
Pale kijijini kulikuwa na bibi ambaye ni bibi yake mzaa mama yule rafiki yangu ambaye kila mtu alijuwa ni mwanga.Siku kama ya nne baada ya kuzika yule bibi tukakutana kwenye uchochoro wa nyumba za pale kijijini asubuhi mapema.Akanitazama kwa mshangao halafu akauliza nafsi yake kwa sauti. Haa huyu si fulani akitaja lile jina la mjukuu wake na rafiki yangu aliyefariki.Loo nikatoka mbio mpaka kwa mama kumsimulia.Mama akang'aka "Mchimvi na mwanga mkubwa yule.Keshakula mjukuu wake sasa anataka kula na wa wenzake lakini hakupati ng'o.Siku ya pili yake Mama akaenda kumwita sheikh akaja kunisomea dua nzito.
Nilipoanza kumjua kuwa huyu bibi si mzuri ni pale kabla kwenda alikuwa na mjukuu wake mwengine wa kike kwa mtoto wake mwengine ambaye alikuwa akiishi nyumba kama ya tano tu kutoka nyumba yake.Alikuwa msichana mzuri sana na nilimpenda sana.Kwa vile mimi nilikuwa nasoma shule ya mbali na pale nyumbani nilikuwa nawahi kutoka asubuhi.
Nikitoka napita pale nyumjbani kwao yeye anafyagia uwanjani.Kwa jinsi alivyokuwa mzuri na alivyopendeza na mimi kumpenda basi ilikuwa nikimuona natetemeka hata nakosa maneno ya kumsalimia vizuri.Alijuwa kuwa nampenda na namuogopa kwa mapenzi basi na yeye akazidi kunifanyia visa nikipita pale kwao anaongeza na tabasamu na mimi nazidi kuchanganyikiwa.
Baadae yule msichana akaumwa na maradhi yake akawa kama mwehu hataki kukaa popote isipokuwa kwa bibi yake.Bibiyake anapoingia na yeye anaingia na kila anapokwenda yupo nyuma yake.Mtoto akakonda mpaka uzuri wake wote ukaisha.Mwishowe akafa.Kama ingekuwa watu wanafufuka kweli basi huyu nikimuona sitamkimbia lakini wapi sijamuona tena mpaka leo.
 
Back
Top Bottom