Wakati nipo shule ya msingi kuna jamaa yangu baba yake alikuwa hataki jamaa asome.
Basi yule mzee kipindi cha likizo anamchukia jamaa'ngu akampeleka vijijini huko ndanindani akamuacha akae na bibi yake ili amsaidie kazi za shamba na kuuza mazao ili aishi huko.
Shule zikafunguliwa mwamba hatumuini shule, mara paap mzee wake akaja akasema jamaa yetu alishafariki na wameshazika huko kijijiniš
Basi tukatangaziwa pale shule, maninja tukasikitika sana mwisho tukamuombea Sir God ampokee mwanetu huko alipo.
Kumbe kule kijijini jamaa anashangaa mbona mzee wake haendi kumchukua, jamaa akajichanga akapata kinauli akarudi.
Asubuhi tupo darasani tunamsubiri mwalimu wa somo, tunakuta mwamba huyo anaingia klasi kama vile katoka kufufuka kama masia.
Ile jamaa anakaa tu kwenye deski watu wote nduki, akajikuta yupo peke yake darasani.
Tukaenda kumuita mwalimu, akaja darasani, ndio jamaa akampa kisa chote jinsi mzee wake alivyomfanyia