Mara ya kwanza kumuamini mwanamke ilikuwa baada ya kuzama kwenye penzi zito na yeye

Mara ya kwanza kumuamini mwanamke ilikuwa baada ya kuzama kwenye penzi zito na yeye

Travis Walker

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2017
Posts
323
Reaction score
334
Kuna mtu alinifunza kuipenda haki. Kwa kuyapitia maumivu na mazito nilijifunza kuwa na huruma. Kwa mara ya kwanza nikamuamini mwanamke. Ama kweli mapenzi ni matamu mno, nilijikuta nazama zaidi kwenye penzi zito. Nikampa moyo wangu nikampenda kupita maelezo. Kabla ya hapo sikutaka kabisa kumuamini mwanamke yoyote ila akanibadilisha mtazamo wangu.

Nikaamini yupo kwa ajili yangu nikachagua kumfanya wa maisha. Niliamini ananipenda kweli ila yote yalikuwa ni maigizo. Alikuja kuharibu karibu na mwisho. Ilikuwa ni muda mchache tufunge pingu ya maisha pamoja.

Niliumia zaidi ya kuteseka mpaka nikajiuliza yawaje mimi mwanaume nimenasa kwenye mtego wa kitoto. Alifanya kuigiza kila kitu, nikajisahau uongo nikauwona ni ukweli mtupu.

1620379558219.png

 
Kila siku tunawaambia ...ukikamata demu .....piga na kusepa .....mnajifanya waoaji
gono sugu litakalo ozesha dushe Lako... linakunyemelea... Litaziba mirija hao watoto utawatazama wajirani tu
 
  • Thanks
Reactions: THT
Mkuuu...pole Sana
Ila Mimi naomba nimquote Zuchu

"Filimbi nitapuliza kuita ndege waje...Raha zimefululiza KWAKO NATOKAJE..."

Pambana na Hali yako mkuuu...msiba kwako kwa jirani sherehe
Yani nalioga sio kunawa 😀😀

Mapenzi haya
 
Pole sana, ila muhimu akili za kiume zimekurudia, hao ndivyo walivyo mkuu, kwao hakuna upendo kuna maslahi wasipoyapata au wakipata makubwa sehem nyingine wanasepa, Tafuta Pesa hayo mengine utaongezewa
 
Mkuuu...pole Sana
Ila Mimi naomba nimquote Zuchu

"Filimbi nitapuliza kuita ndege waje...Raha zimefululiza KWAKO NATOKAJE..."

Pambana na Hali yako mkuuu...msiba kwako kwa jirani sherehe
Vipi wewe maombolezo yashaisha?😂
 
Back
Top Bottom