Mara ya kwanza kutumia vilevi tofauti tofauti haya ndio yaliyonikuta

Mimi silewi na nilijiapiza sitalewa baada ya kuona mwanangu nilienda nae club kwenda kutita kwenye cube ya DJ
 
Hivi ulanzi unalewesha?
Mimi nimekunywa sana nipomaliza chuo nilienda iringa nikafanya kilimo maeneo ya Iyeme jirani mlandege nilikuwa nabeba lita na nusu daily naenda nao shambani nilikuwa nafuata mwenyewe ule ulichacha kabisa ulanzi ni biashara kubwa sana maeneo hayo!
Bangi hapana sijawahi vuta wala sitafuta nimekulia kwenye familia ambayo kuanzia mjomba babu bibi wote wanapiga bangi na hadi sasa ingawa age imeenda wanavuta
 
😂😂😂
 
😂😂😂
 
Brother wewe ni kichwa panzi ndio tunavyowaita kitaa.
Huo ulanzi nilikuwa naweka Lita 5 kwenye friji nauchakata taratibu hapo Veta mbeya.
 
UGORO
Wakuu asikwambie mtu kitu kula ugoro kwa mara ya kwanza...nakumbuka nlikua form v ile..toka mtaani nilikua namba kwenye uvutaji wa bangi na hainipi shida yoyote..

sasa kutokana na mazngira ya bweni kubana sikuweza kupata muda wa kutafuta bangi,nikaona bora nijifunze kula ugoro..

nlimuagiza mlinzi akaninunulia wa buku,wakati wa kwenda prepo,me nkaweka ugoro mdomoni halafu kwenye pilika pilika nkajikuta nmemeza mate yote,,nliuona moto..

nilianguka ghafla kama nadegedege bila kutikisika,macho nimefumba,jasho mwili mzima...wakamuita din of student alinipekua sana lakn hakukuta chochote..

Nakuja shtuka saa 4 asubuhi nipo kwenye hospital ya shule na nikapewa beji(waliosoma seminary wanaijua) ya specia case kuwa naumwa pumu... Ila ugoro nyie
 
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Nulikuwaga na wanangu 2015 Advance Njombe iyo, tumebaki Form 6 tu Shule nzima likizo ya mwisho wa Mwaka tukaenda kijijini ndani ndani uko wanauza Ulanzi na Kitimoto balaa yani ndoo ya ulanzi buku tu, sasa wanangu wote ni wa kule na wanalewa hasa, si wakanywa bwana mimi nipo zangu na mdudu mdogo mdogo, kuja kushtuka giza limeingia na hapo tuko kwenye vilabu vya pombe 😂😂
Ikaanza safari ya kurudi shule mimi peke yangu ndio mzima ilibiki nitafute fimbo ili nipige watu ndio tufike shuleni maana walikuwa wakikutana na mtu wanataka wampige
 
Nimecheka sana hapo kutafuta fimbo ili watu waende. Mimi mara ya kwanza nilikunywa Ulanzi pia. Tulikuwa form IV shule moja Njombe basi tukaenda kufanya project kijiji kimoja cha jirani na shule kinaitwa Matola. Imefika saa 10 jioni tukaanza kurudi mdogo mdogo shule kwa vikundi.

Basi tukawa tumeshikwa na kiu ya maji tukagonga nyumba moja kuomba maji ya kunywa tulikuwa kama 7 hivi hee naona mama anatoka na ndoo ya lita 20 ya Ulanzi na vikombe akasema kunyweni aisee ulikuwa mtamu kweli sijapata ona tukakaa chini kunywa.

Kimbebe ilikuwa kurudi shule njiani wengine walikuwa wanasumbua wameshalewa tulivyofika shule mimi nilipitiliza kulala. Kilichotuponza usiku kulikuwa na disco la shule waliolewa wakaenda kufanya fujo disco.

Matron na walimu wakafanya kazi ya kutuliza fujo tukaitwa assemble usiku ule ule amshwa mpaka tuliolala, inshort tuliokunywa wote tulijulikana tena nilivyoamka ndio ulanzi umekolea mahala pake kichwa kinaona nyotanyota tuu. Kesho yake head mistress akapata taarifa na majina ya walevi.

Ilikuwa tupate suspension ila tulilia sana kuomba wazazi wasijue tukaishia kupewa adhabu ya kulima wiki 2 nzima bonge la shamba asubuhi hadi jioni bila kuingia darasani. Ila Ulanzi mtamu jamani nikienda Njombe lazima nikaunywe tena maana toka kipindi kile sijaonja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…