January hii nilikuwepo ila jamani kijijini kwetu kutamu, watu wana upendo na vile nilikuwa Nina muda sijaenda dah!
Vyakula vya kumwaga, unabembelezwa ule, mawifi zangu kila mtu anataka niende kula kwake, bibi zangu huyu akipika anatuma ujumbe home wananisubiri tule, zawadi sasa halipiti lisaa sijatumiwa zawadi, watoto ni kupishana," Shangazi mama kanipa hii nikuletee", Shangazi mama anakuita, Shangazi baba anakuita, nikifika nikukuta mboga 7 kuku wa kienyeji, kitimoto, sijui mbuzi mmh! Naishia kuonja maana huo ulaji siwezagi dah
Mama yangu sasa, kila kitu aliandaa kadri awezavyo dah.
Kijijini its all about eating, eating eating and eattttttttttt maisha safi ni kucheka ma kufurahi, hakuna stress kule kila kitu bure .
Wageni sasa , ndugu majirani, utaskia Dada huyu kaja kukuona, dah!
Siku ya kurudi nilifungiwa vitu nikawa nacheka mwenyewe maana siwezi mizigo hiyo yote. Dah kweli nyumbani ni nyumbani tu!
Hii corona mbaya sana nilitaka pasaka hii nirudi , kwa mwaka ntakuwa naenda Mara mbili.😁