Maradhi yanayomsibu binadamu na tiba yake

Maradhi yanayomsibu binadamu na tiba yake

Dawa ya Maradhi ya Tonsils aka Mafindofindo

Dawa ya TONSILS ni kusukutuwa maji yaliokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto.

Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia.

Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako.

Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafanya kazi na mdomo uko wazi basi pia unaweza kuumwa na Tonsils.

Vile vile kutoka nje kwenye joto kisha ukaingia pahala baridi huwa inasababisha Tonsils na maradhi mengine kama flu na kuumwa na kichwa..n.k

Au hii Dawa ya Maradhi ya Tonsils. Tonsil husababishwa na sababu nyingi tu. Pia husababishwa na upungufu wa white blood cells katika mwili ambazo cells hizi ndio hupigana na vidudu vyote venye kuleta maradhi ndani ya mwili sasa vinaposhindwa kufanya kazi lymph zinavimba na husababisha Tonsils.

Kila mtu na ukuwaji wake wa mwili, wapo ambao wanapata tonsils kwa kunywa maji ya baridi ambayo maji ya baridi huwa ni moja katika chanzo cha kupata tonsils, mavumbi huchangia vile vile pilipili na vitu vikali kama vile embe mbichi limau pia huwa ni sababu kuu ya kupata tonsil.

Wakati unapokuwa na tonsils muhimu zaidi kuacha maji ya baridi na vitu vyote vikali, zaidi utumie maji ya moto kama alivosema umahmed.

Dawa za tonsils ni : kama ni mtumiaji wa dawa za chemicals basi epincilin inasaidia sana kuondosha tonsils.

Dawa nyengine ambayo mimi binafsi naipendelea hii zaidi kwani inafanya kazi mara moja : Kamua ndimu moja katika glass yako kisha tia maji ya Uvuguvugu (warm water) na baadae tia vijiko vinne vidogo vya asali na kijiko robo cha chumvi kuroga uzuri na unywe pole pole.


Au Dawa hii Ya Maradhi ya Tonsils. To relieve the symptoms such as pain and fever that is normally associated with Tonsils, please take one non-aspirin containing Paracetamol (Panadol), or acetaminophen or ibuprofen three times a day. Aspirin may have negative effects on the aldready swollen tonsils. Swollen, enlarged tonsils may make swallowing painful and eating difficult. Encourage the person to consume liquids and soft foods such as ripen bananas, warm (Not Hot) porridge. Warm (not hot), very cold and bland fluids may soothe the throat. Gargling with warm salt water may also provide relief.

There are two kinds of Tonsillitis: Bacteria Tonsillitis and Viral Tonsillitis. Bacteria Tonsillitis can usually be treated with antibiotics (amoxicillin, doxycycline or cephalexin (Cipro), etc.) or an herbal supplement that contains a mixture of (Pulsatilla, Euphorbium, Hepar Sulphuricum, Calcarea Carbonica) but viral tonsillitis cannot. Please visit your physician to check what kind of tonsillitis you may have. A throat culture can confirm the presence of streptococci or other bacteria and will help your physician determine the appropriate care.
 
Dawa ya Maradhi ya Cancer Kansa

Pakaa mafuta ya HABBA SOUDA (Nigella oil seed )
mara tatu kila siku pamoja na kula kijiko kimoja cha unga wa HABBA SOUDA uchanganye katika juisi ya karoti (carrot) na ule kila unapomaliza kula. Endele kwa muda wa miezi mitatu.

Katika KITUNGUU THOUM (Garlic) muna kiinia kinachozuia Saratani (Cancer), kwa kila mgonjwa wa saratani anashauriwa ale kwa wingi kitunguu thoum na karoti (Carrot) kwa kuendelea. Bila shaka atapata matokea mazuri na shifaa kwa haraka sana kwa rehma zake Allah.

Chukua mkate wa nyuki kutoka mzingani moja kwa moja kiasi cha miligramu 100 kwa wiki mara moja, na kula asali pamoja na nnta yake kila siku kiasi cha kikombe kimoja, na sugua mwili wako kwa mafuta ya Habba souda, kisha oga kwa maji yenye uvuguvugu (warm water) na baadae kula asali iliyochanganywa na unga wa habba souda katika juisi ya karoti kila siku.

Dawa ya kizunguzungu na hata kuumwa na kichwa
Chukua Haba Sawda kisha kaanga na utie kwenye kitamba cheupe na uwe unanusa kila mara. Pia inasaidia kwa kuumwa na kichwa.

Kizunguzungu husababishwa na mambo mengi mfano:
1-Upungufu wa damu mwilini
2-kukosa kulala kwa uzuri
3-Mafikra yakizidi
4-Kukosa kula vizuri

Dawa ya Kuondosha weusi wa vipele vya uso
Kijiko cha chai kimoja -- Juisi ya Viazi mbatata
nusu kijiko cha chai -- Unga wa Lozi
robo kijiko cha chai -- Manjano

Changanya vitu vyote pamoja kisha pakaa kwenye vipele vyeusi (usipake uso mzima kwenye vipele tu). Iwache kwa muda wa nusu saa au hata unaweza kulala nayo. Pakaa kila siku kwa muda wa wiki mbili. Baadae utapaka kwa wiki mara mbili mpaka uone umeondoka weusi utastop.

Wacha kula vitu vya gas kama masoda pia vyakula vyenye pilipili na vitu vya sukari.

Dawa ya chunusi za usoni

Chukuwa limau 1 bichi halafu suguwa yaani jitiye katika sehemu za muasho. au chukuwa mafuta ya halzetu changanya kijiko kimoja kisha jipake sehemu yenye muwasho na kupasuguwana halafu iwache kwa muda kama wa saa moja kisha ukoshe kwa sabuni na maji, fanya hivyo mara moja kwa siku mpaka utapoana muwasho unaondoka


Dawa ya Kusafisha uso

Kijiko kimoja kidogo unga wa mchele
Kijiko kimoja rob
Asali kijiko
nusu kijiko lozi ya unga.

chukua vitu vyote changanya pamoja pakaa kwenye uso wacha mpaka ikauke iwe kavu, baadae tia kidogo maji anza kusugua kidogo kidogo kama ukitia ( scrub) sugua baadae utakosha utaona uso wako laini fanya mara mbili kwa wiki

Dawa ya ugonjwa kwenye fizi ya meno

atafune chembe moja ya kitunguu saumu pale penye jaraha halafu akimaliza atie asali juu yake bila kuchelewa.Lakini ahakikishe hio asali iwe asali safi isiwe asali ya kutengeneza(feki).Na anapotia iwe anajaribu kuhakikisha kwa ulimi kama imefika pahala penye hilo jaraha.
Inshaallah Mola atamsaidia.
Mimi binafsi nilikuwa nina matatizo yanayofanana na hayo nikajirbu kutumia dawa hizi sasa hivi alhamdulillah sijambo kabisa.

Manufaa Za Kucheka
Manufaa za kucheka.
Wanasayansi wamekadiria kwamba kucheka kwa furaha kwa nusu dakika ni sawa na kupumzika kabisa kwa dakika 45. Kuangua kicheko kunalingana na kufanya mazoezi ya viungo kwa dakika tatu, hali kutabasanu kwa uchangamfu mara kumi ni sawa na kufanya mazoezi makali kama ya kuiga makasia kwa kutumia mashini kwa dakika kumi.

Manufaa mengine ya kucheka yanatia ndani kuongezeka mara tatu kwa kiasi cha hewa kinachovutwa ndani ya mapafu na vilevile kuborashwa kwa mzunguko wa damu, umeng'enyaji, kuyeyushwa kwa chakula, utendaji wa ubongo, na kuondolewa kwa vitu vyenye kudhuru.
"Napendekeza kwamba ili uwe mwenye furaha, jambo la kwanza unalopaswa kufanya kila asubuhi ni kutabasamu na kumwonyesha mwenzi wako na watoto wako tabasamu, kama huna hata jamaa zako.

" Jifunze kicheka unapokosea, na jaribu kuona mambo kwa njia nzuri hata wakati hali inapokuwa ngumu."
 
Asante kwa maelezo mazuri.. Kaka huna list uliyoorodhesha tafsiri ya majina ya hizo dawa/vitu tunavyotakiwa kutumia?. Manake karibu majina yote hayo ni mageni kwangu. Kama unaweza ujaribu kututafsria kwenye mabano kwa kiingereza hizo vitu zinaitwaje.. maana lugha inakuwa tatizo kubwa hapa.. Mungu akubariki!
 
Asante kwa maelezo mazuri.. Kaka huna list uliyoorodhesha tafsiri ya majina ya hizo dawa/vitu tunavyotakiwa kutumia?. Manake karibu majina yote hayo ni mageni kwangu. Kama unaweza ujaribu kututafsria kwenye mabano kwa kiingereza hizo vitu zinaitwaje.. maana lugha inakuwa tatizo kubwa hapa.. Mungu akubariki!
Asante bibie mpendwa naanza Dawa hii HABBA SOUDA kwa kiingereza inaitwa (Nigella Sativa oil seed) picha hii

Black Seed oil kwa kiswahili mafuta ya Haba soda au habbat Souda
MAFUTA YA HABBAT SAWDA.jpg


Majani ya Sanamaki. senna leaves

SANAMAKI.jpg


Maua ya babu naji (Chamomile)

chamomile.jpg



Mbeu za Anisuni kwa kiingereza inaitwa (aniseed)

ANISE.jpg



Majani ya Mnanaa kwa kiingereza inaitwa (Mint)

Mint leaves


MAJANI YA MNANAA.jpg



Pilipili Manga au Pilipili Mtama kwa kiingereza inaitwa Black Paper Seed

Pilpili Manga.jpg



Jirjir kwa kiingereza inaitwa (rocket)

Rocket leaves

Rocket leaves.jpg



Mbegu za Harmal, kwa lugha ya kiingereza inaitwa (Peganum harmala)

(Peganum harmala)

Peganum harmala.png



Kamun Aswad kwa kiingereza inaitwa Black chamomile au black Cumin
Black Cumin Seeds



black Cummin.jpg


Dawa zipo nyingi ninazozijua mimi zinafika mpaka dawa 40 lakini kwa leo naishia hapa ninafikiri utanielewa vizuri mkuu mayasa?
 
DAWAYA KUUMWA NA MGONGO

Gundi
( hili gundi limekaa kama ubani wa kufukiziya ) ukiwaambia wenye kuuza madawa wanafahamu. Unasaga unakuwa unga.
Lozi ( unaroweka kwa maji ya mfukuto kisha unatoa maganda na unazikausha kidogo kwenye oven kisha unazisaga.)
Sukari ya Mawe au sukari guru (sukari nyekundu)
Hiliki
Za'farani
siagi kidogo
Maziwa


** Unayayusha siagi yako kisha unatia sukari (mawe au guru) kisha unatia lozi unachanganya kisha unatia gundi, hiliki na za'farani. unaiyepua unaitia kwenye sinia.

*** Ikisha kupoa unatia kwenye chupa au pahala kuihifadhi.

NAMNA YA KUTUMIA:- Kijiko cha supu kimoja asubuhi utakula na usiku kimoja.
MAZIWA UTAKUNYWA GILASI MOJA ASUBUHI BAADA YA KWISHA KULA HIYO DAWA NA USIKU GILASI MOJA BAADA YA KWISHA KULA DAWA.
 
Ugonjwa wa figo na vijiwe

UGONJWA wa mawe kwenye figo siyo mgeni miongoni mwa watu hivi sasa, hasa wenye umri mkubwa. Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni, ukubwa wa tatizo hili umeongezeka, kwani hata vijana wanapatwa na tatizo hili ambalo kitalaamu linajulikana kama ‘Gallstones’.

Mawe ya kwenye figo siyo mawe halisi, bali huwa ni vitu vinavyojitengeneza kwenye figo taratibu na baada ya muda mrefu hugeuka umbo na kuwa mfano wa vijiwe vidogo na wakati mwingine huwa vikubwa mfano wa dole gumba. Hutokana na ulaji wa vyakula usio sahihi.

Tiba ya tatizo la mawe kwenye figo, mara nyingi huwa ni upasuaji wa kuvitoa na hugharimu fedha nyingi na pia husababisha maumivu wakati wa kufanya oparesheni hiyo. Lakini kwa kutumia tiba mbadala ya vyakula, unaweza kuondoa mawe hayo bila kufanya oparesheni.

Maelezo haya huwezi kuambiwa na daktari hospitali hata siku moja lakini kwa kusoma makala kama haya utajifunza njia nyingine ya kuutibu mwili wako kwa njia ya vyakula. Kama mawe yaliingia tumboni kwa njia ya vyakula, bila shaka yanaweza kutoka pia kwa vyakula.

JINSI YA KUONDOA MAWE KWENYE FIGO
Kuna tiba mbadala za aina nyingi, lakini katika makala yangu ya leo nitawajulisha njia mbili unazoweza kuchagua moja wapo. Moja ni kufanya kwa muda wa siku sita mfululizo na nyingine ni ya kufanya kwa siku moja tu, chaguo ni lako.

NJIA YA SIKU SITA
Katika siku tano za kwanza, kunywa juisi halisi ya tufaha (pure apple juice) glasi kubwa nne kila siku kwa siku tano mfululizo. Au kula tufaha nzuri tano badala ya juisi. Ili kuwa na uhakika na juisi halisi, ni vyema ukanunua tufaha za kijani (green apple) na ukatengeneza juisi mwenywe. Juisi hii au matufaha hayo yatafanya kazi ya kulainisha kwanza mawe tumboni.

Siku ya sita, anza siku yako kwa kula mlo wako wa kawaida hadi saa nane mchana, kuanzia saa nane utatakiwa ufunge usile kitu chochote mpaka asubuhi siku inayofuata ndiyo ule chakula chako.

Ikifika saa 12 jioni, kunywa kikombe au glasi moja kubwa ya maji uliyochanganya na kijiko kimoja kidogo cha magneti salfeti (Magnesium Sulphate) inapatikana kwenye maduka ya madawa. Weka maji kwenye glasi au kikombe, chukua chumvi ya mawe, chota kijiko kimoja kidogo, tia kwenye maji hayo na changanya, kisha unywe mara moja. Chumvi ya mawe husaidia kufungua njia.

Ikifika saa mbili usiku, rudia kunywa mchanganyiko huo wa maji na chumvi. Baadaye saa 4 usiku, changanya nusu kikombe cha juisi halisi ya limau (fresh lemon juice) na nusu kikombe cha mafuta halisi ya mzaituni (pure olive Oil). Hiki ndiyo kitakuwa kinywaji chako cha mwisho usiku huo, kisha nenda kalale.

Vinywaji hivyo vitasaidia mawe kutoka kwa njia ya haja kubwa bila shida. Usiku huo huo, unaweza kusikia haja ya kwenda chooni, au vinginevyo utasikia asubuhi.

NJIA YA SIKU MOJA
Ukisha kula chakula chako cha usiku, usile kitu kingine tena hadi kesho yake asubuhi ambapo utakunywa glasi kubwa tatu za juisi ya tufaha za kijani. Usile kitu kingine hadi mchana unywe tena juisi ya tufaha 3. Usile kitu kingine tena hadi usiku wakati wa chakula cha usiku, unywe tena juisi ya tufaha kubwa 3 za kijani kama mlo wako wa usiku.

Iwapo utashindwa kutengeneza juisi mwenywe, basi bora ule tufaha zenyewe kiasi kilichotajwa. Katikati ya mlo na mlo, utaruhusiwa kunywa maji ya kawaida tu na siyo kitu kingine. Hii ina maana utafunga siku moja kwa kula tufaha na maji tu.

Muda mfupi kabla ya kwenda kitandani, tengeneza juisi halisi ya malimau matatu, changanya na nusu kikombe cha mafuta ya mzaituni
(Pure olive oil) kunywa kisha panda kitandani, kinywaji kinaweza kisiwe na ladha nzuri, lakini usijali, ndiyo dawa.

Ukiwa kitandani, lalia ubavu wako wa kulia na ukunje magoti kadiri uwezavyo na ulale hivyo kwa muda utakaoweza au hadi hapo utakapopitiwa na usingizi. Ulalaji wa aina hii huwezesha utokaji wa mawe kwenye figo na kwenda tumboni kwa ajili ya kutoka kwa njia ya haja kubwa.

Ukijisikia haja ya kwenda chooni, fanya hivyo haraka, vinginevyo utalala hadi asubuhi ndiyo utakwenda chooni. Ili kuona kama vimawe vimetoka, weka utaratibu wa kukagua haja yako na utaona vitu rangi ya kijivu au kijani vinavyong’aa na hapo utakuwa umefanikiwa.
 
''Your food shall be your madicine"

Your food shall be your madicine.jpg



Fruit are one of the oldest forms of food known to man. In fact Sayyidna Adam (A.S), wa the first man ate an apple, " the forbidden fruit" of heaven. There are many reference to fruit in ancient literature.
According to Qur-aan, the fruits like grape, date, fig, olive and pomegranate are the gifts and heavenly fruits from Allah (S.W)

Fresh and dry fruits are the natural stape food of man. They contain substanial qunatities of essential nutrients in a rational proportion. They are excellent sources of minerals, vitamisn, and enzymes.

Person subsisting on this natural diet will always enjoy good health.

NATURAL BENEFITS OF FRUIT
Fruit have highly benefiacial effect on human system.

Hydrating Effect

Taking fruit or fruit juice is most pleasent way to hydrating the organism. The water absorbed by sick person in this manner has an added advantage of supplying sugar and minerals at the same time.

Fruits are highly beneficial in maintaining acid-alkaline balance in the body. The neutralise the toxic condition of the body resulting form excessive intake of acid-forming foods.

Fasting is considered as NATURE'S method which was bring to us by our Prophet MUHAMMAD (S.A.W) it is the best method of treating DISEASE.
The best and safest way of fasting is juice fasting, the procedure is to take the juice of an orange or any other fruit dilute with water 5.0:50 every two hours from 8am to 8pm nothing else. Canned or frozen juice should not be used.
The totaly daily liquid inatke should be about 6 - 8 glasses.


NATURAL BENEFITS AND CURATIVE PROPERTIES

APPLE: are invaluable in the maintenance of good health and in the treatment of many ailments. The modern version saying " an apple a day keeps the doctor away".

Anemia:
Apples, being rich in iron arsenic and phosphorus are highly benefiacial in the treatment of anaemia. It will be particulary useful in the form of "freshly prepared apple juice", it may taken in qunatities of 2Kg daily. The best time to take the juice half an hour before meals and before bed.

Constipation & Diarrhoea:
Apple are beneficial in the treatment of both constipation and diarrhoe. Raw apples are good for constipation atleast two apples should be taken daily for proper evacuation. Cooked or baked apples are good for diarrhoe.

Dysentery:

Apples have been found useful ina cute and chronic dysentery among children. Ripe and sweet apple should be crushed into pulp and given to children several time.

Headache:
Appl are highly beneficial in the treatment of all type of headache, a ripe apple should be taken with a little salt every morning on empty stomach. This should be continue for about a week.

Heart Disease:

Apple are special value to heart patients. They are rich in potassium and phosphorus but low in sodium. From ancient time apple with honey in considered very effective remedy forfuctional disorder of heart.

High Blood Pressure:
Apple are considered invaluable in cases of high blood pressure, the apple diet has rapid and considerable diuretic effect cause increase of secretion of urine and thus briging down the bllod pressure to normal.

Rheumatic:
Apples are regarded an excellent food medicine for gout arthiritis and rheumatism especially when these disease are caused by uric acid poisoning .
Boil the apple till turn like jelly and make a good paste and should rubbed freely on the affected area.

Dry Cough:
Sweet apples are valuable in dry hacking cough, you should take apples every day for abput a week.

Kidney Stone:
Apples are useful in kidney stones, you should take everyday.

Dental disorder:
Tooth-decay can be prevented by regular eating of apples as they posses a mounth cleansing property. You should take every after meals because they have effect as a tooth brush in cleasing the teeth.
Apple are thus regarded as natural preserver of the teeth and should be taken ina ll tooth troubles.

Precaution:
Apples should not be eaten on empty stomach as it may cause indigestion. Apples often sprayed with poisonous chemical to prevent them from decay, thus fruits should be washed before eat.
 
Dawa ya Maradhi ya kifua kikuu

Kifua kikuu ni ugonjwa Hatari sana kwa binadamu na ugonjwa ambao unaambukiza kwa njia ya hewa. n
Na ugonjwa huu unaathiri mifupa na mapafu dalili za ugonjwa huu ni hizi zifuatazo:
1. Kupungua uzito wa mwili.
2. kuumwa mara kwa mara.
3.Kifua (kikohozi kisichopona).
4.Kukohowa na kutoka damu.

Chukua juisi ya Kitunguu Thaumu kikombe kimoja changanya na kijiko kimoja kikubwa kilichojaa unga wa habbat sauda kwa kiingereza inaitwa
(Nigella sativa Seed) koroga vizuri kisha unywe kila siku kikombe kimoja Asubuhi na jioni kwa muda wa miezi miwili. Kwa uwezo wa Allah utapona. Pia mgonjwa anatakiwa ajiepushe na kazi nzito ikiwemo ya kufanya mapenzi. Na mgonjwaanatakiwa apate chakula cha kutosha na kilicho bora.
 
Maradhi ya cholestrol Dawa yake ni hii hapa

Chukua majani ya mvuje (fresh) wahindi wanaita currypata na majani ya mchaichai (fresh) chemsha na maji ufanye kiasi yasiwe majani mengi yawe kiasi na maji kiasi kisha kunywa gilasi moja, kwa siku mara 3 au 4 na peleleza ukifanya haja ndogo utaona mafuta yanatoka au yanang`ara ng`ara yaani ndio mafuta yanatoka tumia kwa mwezi kisha kacheki na ukiwa una cholestrol kubwa unaweza kutumia zaidi ya mwezi kisha ukachek. SUBHANALLAH! mambo yakustajabisha wengi waliotumia wamefanikiwa.
JARIBU UTAONA MIUJIZA YA ALLAH.
 
FAIDA NA MANUFAA YA (MAFUTA YA MBARIKA)

1-Mafuta haya yanalainisha ngozi na kuondowa natatazo yake.

2-Pia hitumiwa katika kuponesha kitovu cha mtoto kama kitachelewa kukauka pale anapokatwa, pia husaidia kutoa zaidi maziwa na mama
kwa kupakwa.


3-Pia hupakwa watoto wachanga zikichelewa kuota nywele zao. Hupakwa mara mbili kitika wiki, huwachwa usiku kucha, asubuhi anakoswa-faida ikipatika anapunguziwa na kupakwa mara moja kila mwezi, hadi ionekane faida yake inshallah.

4-Pia huponesha kidonda kwa kupakwa.

5-Pia huponesha maumivu ya miguu-kupakwa mara mbili Kila siku kwa muda wa wiki usiku ukipaka kisha unavaa soksi-hondowa maumivu na hulainisha ngozi ya miguu.
 
Nilipoona neno ALLAH, hamu ya kuendelea kusoma ikaniishia. Sorry, kama watu watakwazika kwa kuwa muwazi kiasi hiki.
 
Kuumwa kwa Mgongo (Sehemu ya Chini):

Changanya asali pamoja na ¼ (robo) kijiko cha Habbat-Sawdaa na iwe kitu cha kwanza kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufungua kinywa.


Maumivu ya mgongo ni tatizo kubwa sana linalowakumba watu tofauti.
Maumivu hayo hutokana na ukaaji kitako wa mtu, matatizo ya kibinafsi
(stress) pamoja na uzito wa mwili wa mtu mwenyewe.

Mara nyingi maumivu ya mgongo huanzia katika kiungo cha kiuno mgongoni na pia maumivu hayo hupandi hadi kufikia katikati ya mgongo.

Na wengi wao huumwa na aina ya mgongo inayoitwa "cervical and lumbar spondylosis" hii hutokana mifupa kuregea na kuachana katika nafasi zao.

Sababu:
Moja katika sababu za kuumwa na mgongo ni upungufu wa harakati za mwili. Mtu hatakiwi kujipweteka siku nzima ni lazima uwe na harakati ili mwili uchangamke na kwa yule anayeweza kufanya mazoezi basi vyema kufanya mazoezi hayo.

Kati ya sababu nyengine ambazo pia huchangia kuumwa na mgongo ni kwa wale wenye matatizo ya kidney na wenye matatizo ya kike (uzazi n.k)

Sababu hii ni sababu ambayo wengine wetu huumwa mgongo kwajili ya ukaaji sana kitako na pia kuvaa viatu vyenye heels refu.
Unapokaa sana ujue namna ya kukaa unatakiwa lazima unyooshe mgongo wako sio ushafika ofisini unajipweteka ndio hapo unaporudi unajikuta mgongo sio wako.
Na kwa wale wanaopenda kuvaa viatu virefu ni vyema wasivae viatu hivo ikiwa watakuwa na harakati nyingi au mwendo mrefu., kwani unalazimisha mascles zako zifanye kazi overload ndipo baadae huchoka zile muscles na hutoa maumivu ya mgongo.


Tumia dawa zifuatazo ili uweze kuponesha mgongo wako:

kitunguu saumu:
Chukua mafuta yoyote uyapendayo ikiwa ya nazi au ya ufuta kiasi cha 60ml uweke katika frying pan na utie vichembe vitatu vya Kitunguu saumu yakaange mafuta hayo mpaka Kitunguu saumu zibadilike rangi, baadae ujipake mgongoni bila kuchua na ukae nayo kwa muda wa masaa matatu baada ya hapo unaweza kwenda kukoga tena kwa maji ya vugu vugu (warm water).

NDIMU:
Kamua juici ya ndimu katika glass ya maji utie na chumvi kijiko kimoja kunywa kwa siku mara mbili. Mungu akipenda utapata nafuu.

Ulaji bora:
Mwenye matatizo ya mgongo anatakiwa ale salad kwa wingi kama vile tungule, carrot, cabbage, matango na vile vile anatakiwa achemshe hizi mboga mboga (asichemshe sana) pia anatakiwa ale fruit kwa wingi isipokuwa ndizi asile.
Ulaji wa asubuhi:
fruit na maziwa
Ulaji wa mchana:

mboga mboga zilizoshemshwa kdg tu pamoja na chapati za unga wa ngano nzima
Ulaji wa jioni:
Fresh juice au fruit.
Ulaji wa usiku:
Bakuli zima la Salad


Unatakiwa uache kula vyakula vya mafuta pamoja na vyakula vya sukari nyingi.

Sigara na aina zote za tobacco anatakiwa mwenye backache aache mara
moja.


Unaweza kujikanda kanda (pole pole) kwa kutumia mpira ya maji ya moto.
 
Nilipoona neno ALLAH, hamu ya kuendelea kusoma ikaniishia. Sorry, kama watu watakwazika kwa kuwa muwazi kiasi hiki.
ulitaka niandike jina gani Mkuu?kwani kuandika Allah au Mwenyeezi Mungu kuna makosa? nimeandika Allah kutokana na mimi muislamna imani yangu , usilete mambo ya Udini hapa kama unataka mambo ya Dini nenda kule kwenye jukwaa la Mambo ya dini mkuu samahani kama nitakuudhi...
 
ubarikiwe mku ila ntarudi kukuuliza baadhi ya material uliyotaja, mengine cjawahi kuyasikia...unga/mafuta ya 'habat soda' let me go through b4 i come back......
Unga ni unga tu na /mafuta ya 'habat soda' kwa kiingereza inaitwa (Nigella Sativa seed Oil)
31UB5LHvteL._SS400_.jpg
 
Ijue Faida ya kula Samaki

SAMAKI (FISH)• Huyayusha damu, huifanya kuwa nyepesi• Huilinda mishipa ya damu isiharibike• Huzuia damu kuganda• Hushusha shinikizo la damu• Hupunguza hatari ya kupatwa na mshituko wa moyo na kiharusi• Hutuoa ahueni kwa wenye ugonjwa wa kipandauso• Husaidia kuzuia uvumbe mwilini• Huendesha mfumo wa kinga ya mwili• Huzuia saratani• Hutoa ahueni kwa wenye pumu• Hupambana na dalili za awali za ugonjwa wa figo• Huongeza nishati ya ubongo

KITUNGUU SAUMU (GARLIC)• Hupambana na maambukizi• Ina kemikali zenye uwezo wa kudhibiti saratani• Hufanya damu kuwa nyepesi• Hupunguza shinikizo la damu na kolestro• Huamsha mfumo wa kinga ya mwili• Huzuia na kutoa ahueni kwa kikohozi kilaini.• Huweza kutumika kama dawa ya kifua

TANGAWIZI (GINGER)• Huzuia ugonjwa wa kutetemeka• Hufanya damu kuwa nyepesi

ZABIBU (GRAPE)•ina uwezo wa kufanya virusi visifanyekazi• Huzuia meno kuoza• Ina mchanganyiko wenye uwezo wa kuzuia saratani

PILIPILI HOHO (GREEN CHILLIES)• Dawa nzuri ya mapafu• Hutumika kama dawa ya kifua• Huzuia na kuponya kikohozi kikali• kuyeyusha mabonge ya Husaidia damu• Hutoa maumivu• Huweza kumfanya mtu kuwa na furaha

ASALI (HONEY)• Huua vijidudu (bacteria)• Huondoa wadudu kwenye vidonda na malengelenge• Huondoa dalili za maumivu• Hutoa ahueni kwa wagonjwa wa pumu• Hutuliza maumivu ya vidonda vya koo• Hutuliza mishipa ya damu, humpatia mtu usingizi• Hutoa ahueni kwa mtu anayeharisha

MAZIWA (MILK)• Huzuia ugonjwa wa mifupa (osteoporosis)• Hupambana na maambukizi, hasa kuharisha• Hurekebisha kuchafuka kwa tumbo• Huzuia vidonda vya tumbo• Huzuia kuoza kwa meno• Huzuia mtu kupatwa na kikohozi• Huongeza nishati ya ubongo• Hushusha shinikizo la damu• Hushusha kiwango cha kolestro mwilini• Hudhibiti baadhi ya saratani

UYOGA (MUSHROOM)• Hufanya damu kuwa nyepesi• Huzuia saratani• Hushusha kiwango cha kolestro• Huchangamsha mfumo wa kinga ya mwili• Hudhoofisha virusi

SHAYIRI (OATS)• Dawa bora ya moyo• Hushusha kolestro mwilini• Hurekebisha sukari kwenye damu• Ina mchanganyiko wa virutubisho unaodhibiti saratani• Hupambana na kuvimba kwa ngozi• Ina uwezo sawa na dawa ya kumpatia mtu choo

KITUNGUU MAJI (ONION)• Dawa kubwa ya magonjwa ya moyo• Huimarisha kolestro nzuri (HDL)• Huifanya damu kuwa nyepesi• Hushusha kiwango cha kolestro mbaya• Huzuia damu kuganda• Hurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu• Huua vijidudu• Huzuia saratani
 
APPLE (Tufaha)
• Dawa nzuri ya ugonjwa wa moyo
• Hushusha kolestro
• Hushusha shinikizo la damu
• Huimarisha kiwango cha sukari katika damu
• Huongeza hamu ya kula
• Linakemikali yenye uwezo wa kuzuia saratani
• Juisi yake inaua virusi vinavyoambukiza magonjwa

BANANA (NDIZI MBIVU)
• Huzuia na kutibu vidonda vya tumbo
• Hushusha kolestrol katika damu

BEANS (MAHARAGE YA AINA ZOTE)

• Hupunguza aina mbaya ya mafuta mwilini
• Hudhibiti kemikali mbaya za saratani
• Hudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu
• Hushusha shinikizo la damu
• Hurekebisha mwenendo wa utumbo mkubwa
• Huzuia na kutibu ukosefu wa choo
• Huzuia kutokwa damu kwenye haja kubwa (haemorrhoids) na matatizo mengine ya tumbo

CABBAGE (KABICHI)
• Hupunguza hatari ya kupata saratani, hasa ya utumbo
• Huzuia na kutibu vidonda vya tumbo (hasa juisi yake)
• Huchangamsha mfumo wa kinga ya mwili
• Huua bakteria na virusi mwilini
• Huharakisha ukuaji wa mwili

CARROT (KAROTI)
• Inaaminika kuzuia saratani, hasa zitokanazo na uvutaji sigara, ikiwemo saratani ya mapafu.
• Hushusha kolestro katika damu
• Huzuia ukosefu wa choo (Constipation)

COFFEE (KAHAWA)
• Kahawa si kinywaji cha mtu kupendasana kutumia, lakini kinapotumiwa kwa kiasi kidogo na kwa tahadhari, kina faida zake:
• Huboresha utendaji kazi wa ubongo
• Hutoa ahueni kwa wagonjwa wa asma (asthma)
• Hutoa ahueni kwa wenye homa
• Huongeza nishati ya mwili
• Huzuia meno kuoza
• Ina kemikali ambayo huzuia saratani kwa wanyama
• Hutoa uchangamfu

CORN (NAFAKA- MAHINDI, MCHELE, N.K)

• Zina aina fulani ya kemikali ambazo huzuia saratani
• Hupunguza hatari ya kupatwa na aina fulani za saratani, magonjwa ya moyo na kuoza kwa meno
• Mafuta yake hushusha kolestro mbaya mwilini
 
BAADHI YA MAGONJWA YA WATOTO YA KUAMBUKIZA NA MATIBABU YAKE

TETEKUWANGA:
Ugonjwa wa tetekuwanga husababishwa na vijidudu vidogo sana aina ya vijasumu. huanza wiki 2 hadi 3 baada ya mtoto kukaa na mtoto mwingine ambaye tayari anao ugonjwa huu.
Kwanza kabisa, madoadoa au vipele vidogo sana vyekundu na ambavyo huwasha, huanza kutokea.
Hivi, hubadilika na kuwa malengelenge na mwishowe, kufanya ganga vyote kwa wakati mmoja.
Kawaida huanza kwenye mwili na baadaye hutokea kwenye uso, mikono na miguu.
Kunaweza kukawa na vipele, malengelenge, na ganga vyote kwa wakati mmoja. Kwa kawaida homa ni kidogo tu.


Tiba:

Ugonjwa hupona baada ya wiki moja. Mkogeshe mtoto kila siku kwa sabuni na maji ya uvuguvugu ili kupunguza kuwasha. Tumia nguo baridi zilizoloweshwa kwenye maji yaliyotokana na shayiri iliyochemshwa na kukamuliwa.
Kata kucha za mikono ziwe fupi kabisa. Kama ganga zinapata ugonjwa, paka gentia violet (g.v) au mafuta ya kuua vijidudu.

SURUA

Ugonjwa huu mkali ambao husababishwa na vijasumu pia ni wa hatari sana kwa watoto wenye utapiamlo au kifua kikuu.
Huanza siku 10 baada ya kukaa karibu na mtu mwenye surua, kwa dalili za mafua homa, makamasi, macho mekundu na kikohozi.
Mtoto huzidi kuwa na hali mbaya. Mdomo unaweza kuwa na vidonda sana na anaweza akaanza hata kuharisha.
Baada ya siku mbili au tatu, madoadoa meupe kama chembe za chumvi hutokea mdomoni. Siku ya kwanza na ya pili baadaye, vipele hutokea. Kwanza kabisa, nyuma ya masikio kwenye shingo, halafu kwenye uso na kwenye mwili na mwisho kabisa, hutokea kwenye mikono na miguu.
Baada ya vipele kutokea, kwa kawaida mtoto huanza kupata nafuu. Vipele huchukua siku tano.

MATIBABU:

Mtoto ni lazima apumzishwe kitandani, apepeswe maji ya kutosha na chakula bora. Kama mtoto hawezi kunyonya kutoka kwa mama, basi mpe mtoto maziwa yaliyokamuliwa kutoka kwa mama kwa kijiko.
Kwa homa na maumivu, toa "asetominofeni" au asprini. Kama anapata ugonjwa wa sikio, toa dawa ya kuua vijidudu.
Kama dalili za kichomi, ugonjwa wa uti wa mgongo au maumivu makali ya sikio au tumbo yanatokea, tafuta msaada wa mganga haraka sana.

KINGA YA SURUA.

Watoto wenye surua ni lazima wakae mbali na watoto wazima. Hasa ni muhimu sana kujaribu kuwazuia watoto wenye utapiamlo au mwenye kifua kikuu au ugonjwa mwingine wa muda mrefu kuchanganyika na watoto wazima.
Watoto kutoka familia zingine wasiruhusiwe kwenda nyumba ambayo kuna surua.
Ikiwa watoto wengine kwenye familia ambayo kuna ugonjwa wa surua, bado hawajaugua surua, ingefaa wasiruhusiwe kwenda shuleni, sokoni au madukani kwa muda wa siku kumi.
Ili kuzuia surua isiwauwe watoto, hakikisha kuwa wanakula chakula bora na cha kutosha. Watoto wazindikwe kuzuia surua wakati wanapofikia umri wa miezi nane hadi kumi na nne.

SURUA YA KIJERUMANI (German measles or Rubella).

Surua ya Kijerumani si kali kama surua ya kawaida, huchukua siku tatu au nne. Vipele vichache mara nyingi tezi zilizo nyuma ya kichwa na shingo huvimba na kuuma.
Mtoto ni lazima apumzike kitandani na atumie asprini kama ni lazima.
Wanawake ambao huugua surua ya Kijerumani katika miezi mitatu ya kwanza ya mimba wanaweza wakajifungua watoto wenye hitilafu au kilema.
Kwa sababu hii, wanawake wenye mimba ambao hawajawahi kuugua surua ya Kijerumani au hawana uhakika ni lazima wakae mbali sana na watoto wenye aina hii ya surua.

MUMPS
Dalili ya kwanza huanza wiki mbili au tatu baada ya kukaa karibu na mtu ambaye ana mumps.
Mumps huanza kwa homa na maumivu wakati wa kufungua kinywa au kula, baada ya siku mbili uvimbe laini hutokea chini ya masikio kwenye pembe za taya. Kwanza, upande mmoja na baadaye upande mwingine.

TIBA:

Uvimbe hupona wenyewe baada ya siku 10 bila hata ya kutumia dawa.
Aspirini inaweza kutumiwa kwa sababu ya homa na maumivu, mpe mtoto chakula bora kilicho na maji maji na weka kinywa chake safi wakati wote.

HATARI:

Kwa watu wazima na watoto walio na umri zaidi ya miaka kumi na moja, huweza kukawa na maumivu ya tumbo au uvimbe unaouma kwenye makende(wanaume) au matiti (wanawake).
Watu wenye uvimbe huu ni lazima wapumzike kitandani kabisa na kuweka mabonge ya barafu au nguo baridi zilizolowanishwa kwenye sehemu zilizovimba ili kusaidia kupunguza maumivu na uvimbe.
Kama dalili za ugonjwa wa uti wa mgongo zinatokea jaribu kupata msaada wa mganga.

KIFADURO:

Kifaduro hutokea wiki moja au mbili baada ya kukaa karibu na mtu aliye nacho. Huanza kama mafua kwa homa, makamasi hutoka puani, na kikohozi.
Wiki mbili baadaye, kifaduro hutokea.

Ghafla, mtoto huanza kukohoa haraka haraka sana bila ya kuvuta pumzi mpaka kohozi linapovutika hutoka, na hewa huingia haraka kwenye mapafu yake kwa mlio wa ajabu unaoitwa kifaduro.
Baada ya hiki kifaduro, anaweza kutapika katikati ya nyakati hizi za kukohoa mtoto huwa mzima kabisa.
Kifaduro huchukua miezi 3 au zaidi.
Kifaduro ni cha hatari hasa kwa watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja kwa hiyo wazindikwe mapema.
Watoto wadogo hawapati kikohozi chenye kifaduro kamili kwa hiyo ni vigumu kuwa na uhakika kama wana kifaduro au hapana.
Ikiwa mtoto mchanga anazimia anapokohoa au macho yake yamevimba panapokuwepo wagonjwa wa kifaduro kwenye sehemu yake mtibu kama mgonjwa wa kifaduro mara moja.

TIBA:

Katika hatua za mwanzo za kifaduro, erythoromycin, tetracyline au ampisilini zinaweza kusaidia. Chroramphenicol husaidia pia lakini, ina hatari zaidi. Ni muhimu.
Kwa wagonjwa wa kifaduro ambao wamezidiwa sana, phenobarbital inaweza kusaidia hasa ikiwa kikohozi kinamzuia kulala au kinasababisha degedege.
Ili kuzuia kupungua kwa uzito na hatimaye utapiamlo, ni lazima mtoto apate chakula bora na ale mara baada ya kutapika.
Wakinge watoto wako wasipatwe na kifaduro hakikisha kuwa wanazindikwa kuzuia kifaduro wanapofikia umri kutokifunga.

DIPHTHERIA.

Ugonjwa huu huanza kama mafua na homa, kuumwa na kichwa na maumivu ya koo. Ganga lililo kama ngozi la rangi ya kijivujivu au njano huweza kutokea kwenye koo na mara nyingine kwenye pua au midomo. Pumzi hunuka sana.
Ikiwa unashuku kuwa mtoto ana Diphtheria:-

Mweke kitandani kwenye chumba tofauti na watu wengine.
Tafuta msaada wa mganga haraka sana. Kuna dawa maalum (antitoxin) kwa diphtheria.
Toa penisilini kidonge kimoja cha uniti 400,000 mara tatu kila siku kwa watoto wakubwa

asukutue mdomo kwa maji yenye chumvi kidogo, Avute mvuke wa maji moto mara kwa mara.
Kama mtoto anaanza kupaliwa au kugeuka rangi na kuwa bluu, jaribu kuondoa ganga kutoka kwenye koo ukitumia kitambaa cha nguo kwenye vidole vyako.
Diphtheria ni ugonjwa wa hatari unaoweza kuzuiliwa kwa urahisi kabisa kwa zindiko la DPT hakikisha kuwa watoto wako wamezindikwa.

POLIO (Ugonjwa wa kupooza wa watoto):

Polio hutokea zaidi kwa watoto walio na umri chini ya miaka miwili.
Ugonjwa huu unaosababishwa na vijidudu vya virus, huanza kama mafua kwa homa, hutapika na maumivu ya misuli.

Mara nyingine, hizi ndizo dalili zinazoonekana tu.
Lakini, wakati mwingine sehemu fulani ya mwili hulegea au kupooza.
Mara nyingi hii hutokea kwenye mguu au mkono mmoja. Baada ya muda mguu au mkono uliopooza huwa mwembamba na haukui kwa haraka kama huo mwingine.

TIBA:

Ikiwa ugonjwa umekwishaanza hakuna dawa itakayoweza kuondoa kupooza. Dawa za kuua vijidudu hazisaidii. Tuliza maumivi kwa asprini au astaminofeni na kukanda misuli inayouma kwa maji moto.

KINGA:

Mweke mtoto mgonjwa kwenye chumba tofauti mbali na watoto wengine. Mama ni lazima anawe mikono kila mara baada ya kumgusa. Kinga iliyo nzuri kuliko zote kwa polio, ni zindiko la polio.
Hakikisha kuwa watoto wamezindikwa kuzuia polio kwa matone akiwa na umri wa miezi miwili, mitatu na minne.

Mtoto aliyelemazwa na polio ni lazima ale chakula bora na kufanya mazoezi ili kuipa nguvu misuli iliyobaki. Kwa mwaka wa kwanza, nguvu inaweza kurudi kidogo.
Msaidie mtoto ajifunze kutembea kwa jinsi anavyoweza. Weka nguzo mbili ili aweze kuegemea. Baadaye, mtengenezee magongo ya kutembelea.
 
Back
Top Bottom