Marafiki hawadumu wanakuja na kuondoka, tuliowahi kuwa mabesti nao leo tunaishia kuchunguliana status hata "hi" hakuna

Hii ilinitokea kwa rafiki yangu mmoja ambaye tulikua tumeshibana haswa kwa miaka mingi, niliamini tutakua close mpaka tukiwa vibibi. Huu urafiki ulivyoisha (kwa sababu ya mgogoro wa kifedha, tulianzisha biashara pamoja) iliniuma kuliko breakup ya mwanaume yoyote. Alihama nchi na hivi karibuni niliona ameview status yangu whatsapp, sijui ilikua kimakosa au alidhamiria. Huwa namkumbuka sana, na kila nikipiga hatua mpya kwenye kazi au maisha nafikiria angekuwepo tungefurahiaje pamoja hilo tukio, nabaki kuumia tu!
 
Pole sana,Maisha ni safari yenye konakona kama mto Nile!
 
Kila stage ya maisha inakuja na watu wake, ukishavuka hiyo stage wanakuja wengine kwa kipindi kingine. Ni aghalabu sana kutunza urafiki wa utoto hadi uzee hasa kwa zama hizi ambapo kila mtu anaenda huku na kule katika kusaka maisha.
 
Neno "gari" kwenye andiko lako umeliandika mara 80...., ndo kusema kwako gari ni kitu gani atii🥲
 
Urafiki ni bond inayotengenezwa kwa sababu flani au moment flani.

urafiki sio kufahamiana, urafiki ni kujuana.

Kwa hiyo kuwa katika shule, ofisi au mazingira yoyote ya kuwafanya mfahamiane, haimaanishi ni marafiki.

Na wengine mnaiva kwa season moja ila hali za kiuchumi au tu kukutana na watu wapya au ukuaji vinatufanya tutofautiane. Kwa walio na bond halisi, hili suala haliondoi urafiki ila kwa wengi. Urafiki hupotea
 
Bond inayotengenezwa nje ya damu ni ngumu kuitunza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…