Marafiki hawadumu wanakuja na kuondoka, tuliowahi kuwa mabesti nao leo tunaishia kuchunguliana status hata "hi" hakuna

Daaa nami nina rafiki alikua mwema sana kwangu, ni mtu ambae sikuwahi kufikiria kama nitamtoa kwenye maisha japo mpaka sasa namkumbuka kwa wema wake kwangu,,
Tatizo letu nilimshauri kuhusu mwenendo wake wa matumizi ya pesa ila akachukulia tofauti alinitumia msg ambayo imegoma kufutika kwenye moyo "futa namba zangu na za mama yangu hatukuhitaji kwenye maisha yetu" daaa nilizifuta kweli na mpaka sasa ni miaka miwili bila mawasilianilo japo namwombea Mungu ambariki sana ktk maisha yake
 
''Za siku kaka naona Mambo yamejipa'', 🤣🤣🤣🤣 kauli ya dharau hii
 
Acha tu live your life and remember over expectations kills many 🤔
 
Marafiki huja na kuondoka kutokana na nyakati za maisha, Mfano mimi sahv watu nnao wasiliana nao sana ni watu wa kazini kwangu tuu, hawa wengine tunaishia kuangalia status tuu, lakini kitu kinachonipa amani sina kinyongo na mtu,siumii kuona sitafutwi na mtu, wala mafanikio ya mtu hayanipi pressure. Kikubwa nawaombea kheri katika maisha yao
 
Kuna tofauti kubwa kati ya rafiki na mtu wako wa karibu.
Lakini pia sio kile ulie soma nae, kuishi nae mtaa mmoja anaweza akawa rafiki.
Mkuu, kuna watu wanazaliwa kwa baba na mama mmoja lakini sio lazima wawe marafiki.
Na mwisho kabla sijasahau......
Mwanaume sio poa sana kujiendekeza kwenye hizo mambo za status mazee....☹️
 
Rafiki wa kweli pesa tu ,hao wengine viroboti tu.
 
Urafiki mara nyingi hujengwa kwa kitu fulani hasa labda ni shuleni, kazini, kanisan, nyumba za kupanga biashara ama kokote,

Kuna watu kweli wanatusaidia lkn siamini lazima niwafanye marafiki sana sana nita wa note in my diary na kuwatakia kila la khery!

Urafiki halisi mtakuwa na ups and downs km mapenzi yalivyo mtatofautishwa na vitu vichache ambavyo huwezi vipata make ni me na me, au ke to ke,

Nachoamini sisi ni binadamu tutatengana ama kuwa mbali huko atakutanna na watu wapya watakuwa marafiki huku nami nikipata marafiki pengine.....

Kinachokuja kuharibu urafiki ni kujiweka kwenye status according na watu unaokutana nao baada ya marafiki wa mwanzoni! Hiki hupelekea chogo, wivu, na kuanzana kuchukiana..

Nina mshkj o level alipo nipo! Mimi nilipo yupo lkn tulitenganishwa kwenda advance shule mbili tofaut so far sikupata rafiki advance mpk namaliza!


Hata namba za advance alumni nimekuja zipata tulipofika chuoni!


chuoni nilipata urafiki kiasi by then nikapunguza sana, nikiamini sio aina ya rafiki ninayemuhitaji!

So far na appreciate kwa kila Jema hata baya walinipa funzo na namna ya kumpokea mtu mpya kwenye cycle yangu!


NB:: family ninayotokea ndiyo marafiki zangu hasa wazazi wangu na ndugu zangu hata nikiwa mpweke, nazungumza na familia yangu..... Nadhani Mungu akijaalia familia nitayoenda itengeneza itakuwa the best pia kwangu na marafiki Bora kwangu.


Hovering Dr am 4 real PhD Determinantor secretarybird
 
Wanaokuhitaji wakati wa shida ndiyo marafiki wazuri.
Na wewe kama kuna rafiki ambaye ukiwa na shida unaenda kwake, huyo ndiyo rafiki mzuri.
 
NB:: family ninayotokea ndiyo marafiki zangu hasa wazazi wangu na ndugu zangu hata nikiwa mpweke, nazungumza na familia yangu..... Nadhani Mungu akijaalia familia nitayoenda itengeneza itakuwa the best pia kwangu na marafiki Bora kwangu.
Siku zote kaka na dada yako ndiyo ndugu zako wa kweli na marafiki zako wa kweli. Uhusiano wako na wao ndiyo unaokuelezea uhusiano wako na binadamu wengine.
Baba na mama hawatakuwepo uzeeni mwako na watoto wako hawatakuwepo utotoni na ujanani.
Kaka na dada zako watakuwepo karibu maisha yako yote na vice versa.
Unashauriwa kama una uwezo uzae watoto wengi kwa sababu ndugu wakiwa wamepatana, mafanikio kimaisha yanakuwa makubwa sana. Mnasomesha watoto wenu, mnaleana wakati wa ugonjwa etc..
 
Exactly 👊....
 
Ntaandika kitu hapa ngoja nipate utulivu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…