Hawa wawili wote ni marehemu kwasasa sidhani kama nitakuja kupata marafiki kama wale japo mmoja tulikutana chuoni
Nick huyu ndio tulikutana chuoni tukaishi zaidi ya ndugu baada ya kumaliza chuo kukawa hakuna ajira miaka ile ya 90 mwanzoni, hustle za mtaani tukawa wote na kwa mara ya kwanza kunywa bia ya serengeti kubwa kipindi hicho ilikuwa kwenye geto lake Tmk[emoji16] nikiwa na mchumba
Baadae alienda kuripoti Mafia kazini mimi nikatimkia South
Alikufa kwa kuzama baharini wakati akirudi toka Likizo Dar na kisababishi ni kaka yake aliyechukua pesa yake mpaka ya nauli ikabidi mwana apande mtumbwi.. Hakufika Mafia na alionekana baada ya siku 3 akiwa kaharibika vibaya... Alizikwa hukohuko