Marafiki wa kweli ni wa utotoni

Marafiki wa kweli ni wa utotoni

Write your reply...mshana umenikumbusha mbali ,nina rafiki yangu huyo miaka saba tulikuwa tunaongoza wote kwenda na kurudi.mda mwingine mnapita mtoni kuoga mkirudi macho mekundu wanajua hawa leo walipita mtoni,mpaka kesho ni rafki yangu .
 
Mimi sina bahati ya Marafiki [emoji24]
Sina Rafiki wa Utotoni wala wa Ukubwani,
Hua natamani sana nikiona Marafiki wameshibana, wanataniana, wanasaidiana, wanaambatana sehemu pamoja, hata nikiangalia movies inayoonesha marafiki fulani wamepambana pamoja hua nawish na mimi ningempata Mtu/Watu wa namna hiyo,

What is wrong with me [emoji24][emoji24][emoji24]
Duuuh poleee dear, hope utapata tyuuh rafiki mzuri.
 
Usiumizwe sana na marafiki wa ukubwani
Usiwaamini sana marafiki wa ukubwani
Wachache sana huwa wakweli na wasio na agenda kificho
Marafiki wa kukutana high school
Marafiki wa kukutana vyuoni
Marafiki wa kukutana makazini
Marafiki wa kukutana ukubwani kwenye biashara, uchumba nknk.. Si marafiki halisi bali ni marafiki kwa sababu fulani

Hawa ni mpaka mkae muda mrefu sana pamoja kwenye hali zote shida na raha, kukosa na kupata, kuumia na kuumizwa! Wengi wao rangi zao halisi hujifunua huku!

Rafiki uliyekua naye mkasoma wote shule ya msingi, mkacheza pamoja, mkachunga pamoja,mkalima pamoja mkatembeleana, mkacheka pamoja mkalia pamoja, familia zenu zinafahamiana ndugu zenu wanafahamiana.. Hawa ndio huwa marafiki wa kweli kwakuwa bond wanayoijenga huwa na vyanzo vingi.. Hawadahauliani na ni vigumu mno kusalitiana!

Tunakutana na watu wapya kila siku, wema na wabaya! Na wabaya waliojificha kwenye joho la wema! Sio dhambi kuwa na marafiki wapya! Maisha ni watu bila watu hakuna maisha ama maisha yanakuwa hayana maana!

Rai tangu ni hii kuwa makini sana unapochagua marafiki wa ukubwani.. Wengi ni marafiki wa agenda.. Wengi ni marafiki kwa sababu . Agenda ikiisha/ikifa ama sababu ikikoma na urafiki nao hufika tamati

Ninao marafiki wengi na ninawaamini sana ila baadhi wameniachia makovu .. Siumii kwakuwa natambua marafiki wa kweli ni wale wa utotoni[emoji2827]

Hata hao wa utotoni pia mkue mkiwa katika level za kiuchumi ambazo hazipashani sana., mwenzako akitoboa alafu wewe bado hauna ramani ushapoteza rafiki hapo maana ataanza kujichanganya na watu wapya wa level yake
 
Kuna mtu ni Rafiki yangu Sana tangu 1998 hasa mama yake alituacha 2001 nimesoma nae Hadi o level!ndio jamaa ninae wasiliana nae kuliko hata ndugu zangu AISEH!

Siku nikipata u namba MOJA nitamuweka karibu Sana!

Sidhani kama atanisaliti AISEH!

Huyu jamaa Dah!kwao walikuwa matawi ya juu Sana!Sasa sio kiviile ndio mtu pekee ninaweza mwambia Siri nzito kuliko hata ndugu yeyote yule Jamaa!!
 
Daah kumbe sipo peke yangu.
Nimewahi kuwa na rafiki wa kweli mmoja tu.
Nasikitika maisha yalitutenga tukapotezana...Danel/Danyo popote ulipo
Mi pia alikuwepo huyo tu Frida.... sijui shetani gani alipita kwakweli, sijawahi kuwa na mtu mwingine kama yeye alikua ni yeye tu. Siku hizi naishi kama nipo kaburini mwenyewe mwenyewe....ila am okay
 
Sisi wa geti kali tusemeje sasa 🌬️🤣🤣

Mi pia alikuwepo huyo tu Frida.... sijui shetani gani alipita kwakweli, sijawahi kuwa na mtu mwingine kama yeye alikua ni yeye tu. Siku hizi naishi kama nipo kaburini mwenyewe mwenyewe....ila am okay
Polee.
Unaweza kucheka au kuwa na kampani ya watu wengi na watu wakafikiri una marafiki wengi kumbe huna hata mmoja
 
Back
Top Bottom