Nina rafiki mmoja niliesoma nae primary. Sasaivi wote ni watu wazima tuna maisha yetu na familia zetu. Wake zetu wanafahamiana na wamekua marafiki pia.
Nina rafiki mmoja nilieishi nae kitaa wakati tunasoma sekondari. Huyu jamaa tulikuja kua kama ndugu ikapelekea mpaka wazazi wetu na ndugu zetu wengi kufahamiana kupitia sisi. Kwa sasa jamaa yuko mbali sana na tunaweza kata mwaka hatujawasiliana, ila akija ni kama tulikua wote jana.
Nina rafiki mmoja wa a level. Jamaa ndie msimamizi wangu wa ndoa na mimi pia nimemsimamia. Mwanangu sana mpaka kesho
Nina rafiki mmoja wa chuo ambae ni wife. Cha ajabu wakati tunasoma hatukuwahi ku date.
Nina marafiki wawili wa kazini ambao hawa wamekua ndugu kabisa manake dah.. Hawa jamaa, wake zao, watoto wao, ndugu zao, ukoo wao wote tumekua kitu kimoja kwenye shida na raha tuko pamoja.