Marafiki wangapi uliokuwa nao wakati unasoma bado unao?

Marafiki wangapi uliokuwa nao wakati unasoma bado unao?

Yupo jamaa mmoja alikua mwana sana secondary hata mchongo wa kazi nilimuunganishia, badae akawa hapokei hata simu zangu 😂😂 , kumbuka wakati namuunganishia mimi ni jobless

Kama bahati nikapata mchongo kampuni hiyohiyo, jamaa akanikunjia hadi kunigombanisha na familia yangu chanzo ni (..)

Mpaka saivi bado na sort sana rafiki wakua nae
 
rafiki wa shule ya msingi duh tulipoachana shule kila mtu alikula kona, secondary nilikua naye mmoja tukaja kuachana huyu namtafta had leo sijajua n mzima au la kwa sasa ninaye mmoja tulikutana kazini she is my partner in crime mpaka sasa
🙄🙄Nimeduwaa kidogo hapo kwenye Partner in Crime.
 
Nilishawahi kuwa nae mmoja tuliyeshibana nikiwa O level...alifariki nikiwa chuo mwaka wa kwanza
Baada ya hapo sijawahi kuwa na rafiki yule wa kushibana kama ilivyokuwa yule ambaye hayupo tena

Zaidi ya hapo rafiki nayekuwa nae ni yule niliye naye kwenye mahusiano ya kimapenzi tu
 
Nna rafiki wa primary hatukusoma wote secondary na chuo lakini hadi leo mawasiliano yapo na tunasaidiana sana.
Sekondari(tulikutana advance) nna rafiki mmoja tunaendana mambo mengi sana. Chuo napo nimeambulia mmoja huwa tunawasiliana kwa mwezi hata mara mbili au zaidi.
Hawa wameshakuwa kama ndugu kwangu, nikiwasilisha changamoto yangu kwa hii familia yangu niliyojichagulia ikashindikana kutatulika basi nakubali uhalisia.
 
Nina rafiki mmoja niliesoma nae primary. Sasaivi wote ni watu wazima tuna maisha yetu na familia zetu. Wake zetu wanafahamiana na wamekua marafiki pia.

Nina rafiki mmoja nilieishi nae kitaa wakati tunasoma sekondari. Huyu jamaa tulikuja kua kama ndugu ikapelekea mpaka wazazi wetu na ndugu zetu wengi kufahamiana kupitia sisi. Kwa sasa jamaa yuko mbali sana na tunaweza kata mwaka hatujawasiliana, ila akija ni kama tulikua wote jana.

Nina rafiki mmoja wa a level. Jamaa ndie msimamizi wangu wa ndoa na mimi pia nimemsimamia. Mwanangu sana mpaka kesho

Nina rafiki mmoja wa chuo ambae ni wife. Cha ajabu wakati tunasoma hatukuwahi ku date.

Nina marafiki wawili wa kazini ambao hawa wamekua ndugu kabisa manake dah.. Hawa jamaa, wake zao, watoto wao, ndugu zao, ukoo wao wote tumekua kitu kimoja kwenye shida na raha tuko pamoja.
 
Sina rafiki yoyote niliyesoma nae hata sijui wapo wapi asee ..kwanza nilikuwa siwapendi walinionaga Muhuni sana ila ndio wakwanza kutoboa ..nikirudi kitaa nawazoom Kwa mbali wengine washazeeka .
[emoji16][emoji16] wewe hujazeeka
 
Back
Top Bottom