Marafiki wangapi uliokuwa nao wakati unasoma bado unao?

Marafiki wangapi uliokuwa nao wakati unasoma bado unao?

Khantwe

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
59,415
Reaction score
119,473
Habari za wakati huu,

Rejea swali hilo hapo juu...katika maisha ya ukuaji, masomo, utafutaji huwa tunajikuta tunakutana na watu wengi... wengine wanabaki kuwa tu watu tunaofahamiana nao na wengine wanakuwa marafiki tena wengine huwa tunashibana kiasi cha kuwa kama ndugu.

Nakumbuka shule ya msingi nilikuwa na rafiki yangu mmoja anaitwa A ..ni hulka yangu kuwa na rafiki mmoja tu wakizidi sana wawili. Of course wanaweza kuwa wapo na wengine ila wa karibu huwa ni mmoja.

Huyu tumekua wote hadi chuo lakini baada ya hapo kila mtu alipoingia kwenye kutafuta maisha tukajikuta tunakuwa mbali, mawasiliano yakapungua kama sio kukatika kabisa.

Kila mtu ana namba ya mwenzie ila tuna miaka zaidi ya mitatu hatujawasiliana, hata tukipigiana simu hatuna stori.

Huo ni mfano mmoja tu ila wapo niliokutana baada ya hapo , tulikuwa karibu sana ila sasa hivi tumekuwa total strangers.

Nilichogundua ili watu muwe na muendelee kuwamarafiki lazima kuna vitu muwe mnafanana, mazingira yaliyowakutanisha yakibadilika tu kila kitu kinabadilika.

Mfano mlikutana mkiwa single mmoja akiwa na familia urafiki kwa vyovyote utakufa tu.

Mlikutana hohehahe mmoja akifanikiwa urafiki utakufa au unabadilika kutoka urafiki hadi uchawa...labda yule aliyefanikiwa awe na moyo wa kumuinua mwenzake.

Mkikutana hamna ajira mmoja akipata kazi anakutana na marafiki wapya.

Au nyie wakuu mnaonaje? Niwatakie jioni njema
 
rafiki wa shule ya msingi duh tulipoachana shule kila mtu alikula kona, secondary nilikua naye mmoja tukaja kuachana huyu namtafta had leo sijajua n mzima au la kwa sasa ninaye mmoja tulikutana kazini she is my partner in crime mpaka sasa
 
Kuna marafiki mimi nilikuwa nao tulishibana haswaa hadi nashangaa kwa nini sasa hivi hatuwezi hata kupiga stori
 
Yupo mkaka mmoja .... classmate primary school....huwa ananinunulia kababu ninavyokwenda kazini asubuhi....mishe zake ni dereva wa Costa....wanamwita fuvu sababu ana kichwa kikubwa ila ukarimu wake hajabadilika aisee....ngoja kwanza,ninampango ninunulie hata soksi maana baridi kweli asubuhi🤒
poa msalimie fuvu
 
Marafiki wa high school baadhi tuko karibu sana ila cha ajabu sina rafiki hata mmoja niliesoma nae darasani [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hawa nilionao walikua madarasa mengine kabisa. Chuo pia marafiki baadhi wapo ila wengi ni wapya wa mtaani... na hawa wa mtaani wengi wamenifaa sana kwenye maisha [emoji120][emoji120]
 
Yupo mkaka mmoja .... classmate primary school....huwa ananinunulia kababu ninavyokwenda kazini asubuhi....mishe zake ni dereva wa Costa....wanamwita fuvu sababu ana kichwa kikubwa ila ukarimu wake hajabadilika aisee....ngoja kwanza,ninampango ninunulie hata soksi maana baridi kweli asubuhi[emoji855]
[emoji16][emoji16] hongera kwa kuwa na rafiki anayekujali
 
Marafiki wa high school baadhi tuko karibu sana ila cha ajabu sina rafiki hata mmoja niliesoma nae darasani [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hawa nilionao walikua madarasa mengine kabisa. Chuo pia marafiki baadhi wapo ila wengi ni wapya wa mtaani... na hawa wa mtaani wengi wamenifaa sana kwenye maisha [emoji120][emoji120]
Hongera mwenza unaonekana wewe ni mtu wa kujichanganya[emoji16] sisi wengine wazito sana kutengeneza marafiki
 
Back
Top Bottom