Marafiki wangapi uliokuwa nao wakati unasoma bado unao?

Marafiki wangapi uliokuwa nao wakati unasoma bado unao?

Yupo jamaa mmoja alikua mwana sana secondary hata mchongo wa kazi nilimuunganishia, badae akawa hapokei hata simu zangu [emoji23][emoji23] , kumbuka wakati namuunganishia mimi ni jobless

Kama bahati nikapata mchongo kampuni hiyohiyo, jamaa akanikunjia hadi kunigombanisha na familia yangu chanzo ni (..)

Mpaka saivi bado na sort sana rafiki wakua nae
Tueleweshe vizuri hicho chanzo
 
Nilishawahi kuwa nae mmoja tuliyeshibana nikiwa O level...alifariki nikiwa chuo mwaka wa kwanza
Baada ya hapo sijawahi kuwa na rafiki yule wa kushibana kama ilivyokuwa yule ambaye hayupo tena

Zaidi ya hapo rafiki nayekuwa nae ni yule niliye naye kwenye mahusiano ya kimapenzi tu
Pole sana baby sisy
 
Nina rafiki mmoja niliesoma nae primary. Sasaivi wote ni watu wazima tuna maisha yetu na familia zetu. Wake zetu wanafahamiana na wamekua marafiki pia...
Hongera mkuu ila hapo kwa rariki yako aliyekusimamia ndoa halafu na wewe ukamsimamia ilikuwaje? Nimechanganyikiwa kidogo
 
Hongera mkuu ila hapo kwa rariki yako aliyekusimamia ndoa halafu na wewe ukamsimamia ilikuwaje? Nimechanganyikiwa kidogo
Sisi ndio tulianza kufunga ndoa so yeye na mchumba ake walitusimamia wakiwa hawajaoana bado, sisi tukaja kuwasimamia walipooana.
 
Sisi ndio tulianza kufunga ndoa so yeye na mchumba ake walitusimamia wakiwa hawajaoana bado, sisi tukaja kuwasimamia walipooana.
Aisee kumbe
Taratibu za makanisa zinatofautiana maana mimi nilikuwa najua wanaosimamia ndoa ni wanandoa tu kumbe sehemu nyingine wachumba wanaruhusiwa
 
Aisee kumbe
Taratibu za makanisa zinatofautiana maana mimi nilikuwa najua wanaosimamia ndoa ni wanandoa tu kumbe sehemu nyingine wachumba wanaruhusiwa
Hata mimi nilidhani hivyo, ila kipindi chote cha maandalizi ya ndoa hatukuwahi kuambiwa na wala siku walipoenda kanisani kujitambulisha kama wasimamizi wetu hakuna aliyewauliza kama wameoana au la. So tukaendelea.
 
Back
Top Bottom