#COVID19 Marais wa EA wapata chanjo ya Corona, isipokuwa wa Tanzania

#COVID19 Marais wa EA wapata chanjo ya Corona, isipokuwa wa Tanzania

Kataa wewe binafsi usiunganishe wa TZ wote.

Huko nje wanasema kwamba:

"The most mutated variant of the coronavirus yet was found in travelers from Tanzania, prompting scientists to call for greater monitoring in a country that has largely ignored the pandemic".

Acha hao scientists wamalize utafiti wao wake na kitu kamili.

Bado tunamalizia maombolezo ya msiba kwa sasa.
Mungu atuhepushe na janga hili, maana kwa mikusanyiko ile ya wiki nzima isiyokuwa na tahadhari yoyote tunaweza kuongeza maombolezo badaya ya kumaliza maombolezo.

Kapten, walisema hivyo hivyo alipofariki Maalim Seif, na Unguja ilivyo ndogo, nikajua kisiwa kitabaki ukiwa, nikawahi bara kuepuka maambukizi ili nikakamatie beach plot, lakini hadi sasa tunavyoongea watu wanaendelea na maisha kama kawaida. Mbaya zaidi, warusi wamejaa kila kona ya mtaa.

Mungu ataendelea kuepushia mbali na kutufanyia wepesi.
 
Corona ni biashara ya mabeberu wameona hela za ARV haziwatoshi wameamua kuleta Corona na chanjo yake,TZ hakuna corona ndugu zangu ,tusipende vya wazungu

Cc: marehemu Jiwe a.k.a John Pombe Magufuli
Hizo ARV huwa unazinunua?

ARV zinatolewa bure kwa wahanga kupitia misaada ya watu wa marekani(hao mnaowaita mabeberu)

Hizo propaganda zenu za kuita washirika wa maendeleo majina ya ajabuajabu nadhani zimefika mwisho. Madam President, H E Samia Suluhu Hasani naamini hatafuata njia hiyo ya kishamba!
 
View attachment 1735780View attachment 1735781View attachment 1735782

Hatimaye wakuu wa EA wamepata chanjo ya kujikinga na gonjwa hatari la Corona, isipokuwa Rais wetu Mama Samia...
Kama uzi hauhitaji hoja, hiyo taarifa si ungepeleka moja kwa moja Lumumba kwa wajinga wenzako ambao hawakumshauri Rais aanze kuchanja yeye kwanza na Makamu afuate wote wangekuwa hai wanachapa kazi.

Rais aliyopo hana namna ya kupata Chanjo haraka maana Mtangulizi wake alikataa na kuzuia mgawo wetu wa bure toka WHO badala yake kuwa agizo lake waganga wa kienyeji wajanja wakaiuzia Serikali mashine feki za kujifukiza ambazo hata yeye mwenyewe hazikumsaidia. Rais aende Muhimbili, Mloganzila Mtangulizi hakufanikiwa!
 
Hao manesi mbona wao wamevaa barakoa wakati na wao tayari wameshapata chanjo
Chanjo haizuii maambukizi ya Covid19. Chanzo inazuia mhanga kuugua Corona akipata maambukizi.

Unaweza kujuta mtu amechanjwa lakini yuko Covid19 positive hivyo ili asiambukize wengine,uvaaji wa barakoa ni mijini,kuzuia virusi kusambaa kutoka kwake kwenda kwa wengine.

Narudia tena kazi ya chanjo ni kuzuia mhanga wa Covid kuugua korona anapopata maambukizi ya kirusi cha Covid19.
 
Nimefurahi kumuona m7 akipata chanjo naona mpango wake wa kutawala milele unaelekea kufaulu.
 
Mleta mada una hiana na Tanzania. East Africa ina nchi 6 na waliochanjwa ni Marais wa nchi 3 tu. Unasemaje isipokuwa Tanzania?? Mbona huitaji Burundi na South Sudan??!
 
Wengine Hirizi tu walizonazo na Majini wanayoyamiliki 24/7 ni Chanjo tosha Kwao zaidi ya Pfizer, Astra Zeneca na J & J Vaccines za Covid-19 ( Corona )
 
Acha hao scientists wamalize utafiti wao wake na kitu kamili....
Kuna njia mbili za kufikia herd immunity. Njia ya kwanza, inayopendekezwa na wanasayansi, ni kutumia chanjo kufikia herd immunity.

Njia ya pili ni kuacha nature itake control. Acha virusi visambae hadi asilimia 70 ya watu wawe infected halafu badaye, watakaokufa wafe, watakaoishi watapata natural immunity.

Tanzania imechukua mkondo wa pili, na ubaya wa hii option ni kwamba watu wanakufa wengi sana na kuna uwezekano wa kutengeneza mutant variants walio hatari zaidi , uzuri wa hii option ni kwamba tunafikia peak na herd immunity mapema zaidi.

Kwa ishu kama ya Corona bado naamini option 2 ndio inayofaa kwa nchi kama zetu. Option 1 ni very expensive, economically and practically. Kuvaccinate watu 70% ya population ya watu milion 60 ili kufikia herd immunity si kitu kidogo.
 
Magufuli alizembea na ujuaji wake umegharimu maisha yake.

Tanzania mnasema mnamtegemea mungu, sijui wengine wanategemea mawe?

Ujinga una gharama kubwa sana.
MKUU kwani wewe umekatazwa Usichanjwe mbona Unatoa Povu sana?

Kama unataka kuchanjwa unavukatu Boda unaenda kuchanjwa MKUU. Tusilazimishane Machanjo tusiyoyajua ni Hatari kwa Afya zetu.
 
Kuna njia mbili za kufikia herd immunity. Njia ya kwanza, inayopendekezwa na wanasayansi, ni kutumia chanjo kufikia herd immunity.

Njia ya pili ni kuacha nature itake control. Acha virusi visambae hadi asilimia 70 ya watu wawe infected halafu badaye, watakaokufa wafe, watakaoishi watapata natural immunity.

Tanzania imechukua mkondo wa pili, na ubaya wa hii option ni kwamba watu wanakufa wengi sana na kuna uwezekano wa kutengeneza mutant variants walio hatari zaidi , uzuri wa hii option ni kwamba tunafikia peak na herd immunity mapema zaidi.

Kwa ishu kama ya corona bado naamini option 2 ndio inayofaa kwa nchi kama zetu. Option 1 ni very expensive, economically and practically. Kuvaccinate watu 70% ya population ya watu milion 60 ili kufikia herd immunity si kitu kidogo.

Ndio maana tokea awali nilisema, hadi sasa, kuna baadhi ya nchi zimejitahidi, zingine zimeshindwa na wengine bado wanapambana.

Kwa ufupi, hakuna suluhu moja ambayo imeshaonekana kufaa na kuwa bora zaidi kwa nchi zote, haipo. Tumeshuhudia juzi baadhi ya nchi wakisitisha matumizi ya chanjo kupisha uchunguzi.

Hata Sie hii tuliyochagua ni miongoni kwa njia za kupambana na hili janga
 
Nini ya Corona hata ya mbwa wachanje haitusumbui.
 
Very soon Mama Samia atapata chanjo na watanzia wote tukiongozwa na Mataga wote tutapata chanjo.
 
Mara paaap! Mmoja wao anapata, "blood clots" (mgando wa damu), nchi yake inakuwa kwenye maombolezo, tunamzika, tunamsahau, maisha yanaendelea.

Wacha tusubiri, tutaona matokeo yake.
 
Back
Top Bottom