Marangu Coach imefikia hatua hii

Marangu Coach imefikia hatua hii

Hujui wala huna uhakika na unalolisema. Wao nao ni shida tu na zile marcopolo zao. Kuna uzi humu wa changamoto.

Hao marangu mara nyingi huwa na gari standby kwa dharura kama hizo. Nashangaa wameshindwa kuwaletea gari ingine.
Labda kwakua siku hizi wana safari za usiku hivyo kukosa za standby.
 
Siwezi sema alitaka sifa mkuu. Kumbuka hiyo ni pesa ameweka hapo. Ila usimamizi ndo shida na service. Yaani ni kama dar ex press. Madereva ni very reckless. Ni kama pia aliisusa sasa alaamua kujikita kivingine. Mbali na yote boashara ya mabasi siyo kazi aisee
Kuivest Hela yako kwenye biashara ya bus inatakiwa uwe umevuta bangi na uwe na moyo wa chuma.
 
Mkuu yale mataa ya rangi huenda ndio kivutio kwao,ushamba ni mzigo.
Ni kweli mkuu, wanalewa mapambo, lakini ukweli utabaki palepale, scania ndiyo usafiri pekee wa uhakika hata comfortability na entertainment mechanism yake imejengwa kiustadi zaidi kuliko hizo zingine
 
Ah watu wanataka wakipanda kuna zile taa zipo juu kama kwenye rolls royce zinaitwa nn nshasahau nilipanda basi moja la kichina nikaziona
Nilicheka😂😂😂
Hapo ndo wakiona zile huwatoi kwenye bus
Na vile vimulimuli kama vya kwenye raba za watoto
 
Note: Ukiona basi lina namba A au B la Kilimanjaro Express usipande, ni gari ya mkaa, tripu moja shamba nyingine garage, ni spana mkononi.
Mkuu sibishani na wewe ila Kilimanjaro wana mabasi 6 mapya sijui ni scania generation gani yana vyoo ndani ni mazuri sana nimesafiri nayo zaidi ya mara 16 mwaka huu sijaona usumbufu wowote natamani kama kuna mwenye picha zake ayaweke hapa ushuhudie namba zake yote ni D za mawishoni
 
Naomba mwenye picha ya magari mapya ya Kilimanjaro Express atusaidie kuweka hapa maana watu wameng'ang'ania kuwa KLM hajawawa na magari mapya ya usajili wa D
 
Zinaharibika ndege iwe marangu coach, pia elewa spare kutoka Moshi siamini ila Naona kama umeweka ushabiki
Shika unalojua wewe, haulazimishwi kuamini kwani halibadili lililotokea, tuhitimishe kwa kukubaliana kuwa safari haikuwepo.
 
Sasa ww gari imeharibika Bagamoyo wanasubiri spea kutoka Moshi bado umegandiana tu na hilo basi!!???
Bagamoyo kuna gari nyingi sana.
Acha hizo, hilo basi abiria wanalipa nauli kwenye ofisi siyo kwa kondakta kama ulivyozoea kwenye daladala, kama ni tajiri kama wewe unaweza ukaisamehe shs 40,000/= ukalipa nyingine kwenye basi lingine, tumia pesa ikuzoee.
 
Inawezekana kbs mkuu. Inategemea na office kuu ziko wapi. Pia gharama
Na wako wafanya biaahara wengi hapo mjini wametoboa kwa kununua spare kenya. Na mpk leo wanafanya. Kama alivypsema mwingine hapo juu kwamba gharama ni ndogo. Pia wenye magari mengi wana tabia ya kununua spare za jumla nanhata tairi halafu wanachhkua store wakiwa na uhitaji. So sishangai. Naweza enda china nikafunga mzigp wa kutosha kupunguza gharama
Kilichonishangaza Moshi na bagamoyo ni mbali Sana, wasingefanikiwa kuondoka Siku hiyo kama spare ingetoka Moshi hivyo story imetia mashaka
 
Jana Jumatano 04/10/2023 basi la Marangu Coach liliondoka Dar es Salaam asubuhi kama kawaida na abiria wakiwa na matarajio ya kufika Moshi kwenye saa 10 hivi bila kujua lililo mbele yao, basi lilipofika wilaya ya Bagamoyo likaharibika ikabidi spea iagizwe toka Moshi iletwe Bagamoyo! Akili mbovu.

Spea haikuletwa kwa ndege wala ungo, Moshi siyo Dar masaa yalipita Mungu Mkuu ikafikishwa na basi likatengenezwa na kuendelea na safari, likaingia mkoa wa Tanga likaharibika tena na likatengenezwa na kuendelea na safari, mpaka saa nne usiku basi lilikuwa wilaya ya Same! Usingizi ukanipata nikazimika na sijui Moshi liliingia saa ngapi ila lilifika salama, hiyo ndiyo Marangu Coach.
Kama binadamu wanaumwa itakua gari? Ungepanda ndege!
 
Kilichonishangaza Moshi na bagamoyo ni mbali Sana, wasingefanikiwa kuondoka Siku hiyo kama spare ingetoka Moshi hivyo story imetia mashaka
Kama basi ilifika Moshi saa tano usiku kwanini isiwezekane ndani ya saa 17 za safari.
 
Acha hizo, hilo basi abiria wanalipa nauli kwenye ofisi siyo kwa kondakta kama ulivyozoea kwenye daladala, kama ni tajiri kama wewe unaweza ukaisamehe shs 40,000/= ukalipa nyingine kwenye basi lingine, tumia pesa ikuzoee.
Kwa hiyo hata siku tatu ungeganda hapo kisa umelipa Tzs40000 acheni hizo bana!! time is money. Unless uniambie hukuwa na haraka. Na ulikuwa unakwenda Moshi kula maboga
 
Kwa hiyo hata siku tatu ungeganda hapo kisa umelipa Tzs40000 acheni hizo bana!! time is money. Unless uniambie hukuwa na haraka. Na ulikuwa unakwenda Moshi kula maboga
Time is money to you rich guy who has the money, to me 40,000/= is alot of money enough for my two weeks meals. Siwezi kushindana na mtu kama wewe unayeweza kulipia meza ya watu wawili kwenye onesho kwa shs500,000/=, masikini akipata matako hulia mbwata, na kijijini kwao hususa haendi. Yaani nipande basi kwenda Moshi kwa shs 80,000/=! Simply eti mzungu kasema time is money! Wewe na Mramba aliyetuambia tutakula nyasi baada ya kutuona sisi manyani ni ndugu moja.
 
Tuliposema mabasi ya kichina ni hovyo tulishambuliwa tukaambiwa hatuendi na wakati, huo upuuzi hutausikia Kilimanjaro Express, wale gari zao nyingi kama siyo zote ni toughened and trusted Scania.
Hii inadhihirisha kwamba hapa TZ mmiliki wa biashara akifa, uwezekano ni mkubwa baishara aliyoacha nayo itakufa kwa usimamizi mbovu
 
Back
Top Bottom