March 04 2013: Kenya's historic poll - Kenya decides!

March 04 2013: Kenya's historic poll - Kenya decides!

sehemu kubwa ya matokeo ni kutoka strong holds za kenyatta, tusubiri kwanza watangaze ya kisumu

Hakuna cha strong hold wala nini. Tayari baadhi ya vituo muhimu huko Kisumu na maeneo ambayo ni strong hold za Raila matokeo yametoka kama vile Siaya, Busia, Kisii, Homa Bay, Migori n.k. Hebu niambie ni strong hold gani mebaki hapo? Lolote laweza kutokea kwani mpaka sasa hawajahesabu zaidi ya kura 2,000,000 ukilinganisha na idadi iliyotarajiwa ya almost millioni 10.

Tiba
 
unajua maana ya utabiri?

Sikumaanisha maana halisi ya utabiri. Kwa maana halisi ya utabiri, hata anayesema fulani atashinda baada ya kuona trend ya kura siyo anatabiri. Neno hilo limetuika vibaya. Lakini umeelewa nilimaanisha nini. Au hujaelewa nilimaanisha nini?
 
12.2% ya matokeo, Uhuru anaendelea kuongoza kwa 54% na Odinga 39%.
 
Update saa 4:10 usiku

Uhuru - 663,384 55.95%
Raila - 473,598 39.91%

Tiba
 
Haya matokeo yanatoa picha mbaya sana kwa Wakenya. Inakuwaje mtu anapata almost 100% ya kura zote eneo moja na 0% eneo lingine. Ukabila utawatafuna wakenya siku moja
 
Kenyatta 677,384
odinga. 481,042

mudavadi 30,537
kenneth. 6,249
kiyiapi. 4,627
karua. 4,383
dida. 2,659
muite. 1,328
 
Update Saa 4:30 Usiku

Uhuru - 680,458 54.04%
Raila - 483,266 39.80%

Tiba
 
Baba yake Karume alikuwa raisi, baba yake Bush alikuwa raisi, baba yake Kabila alikuwa raisi-huko kote sijaona kama uraisi umefanywa wa ukoo!!!
uongozi si kila koo zaweza kushika uongozi . hata zamani zilikuwepo koo za watawala ,wengine walinzi,wengine wahunzi n.k hilo suala ni natural.hata waingereza leo pamoja na kujifanya wakongwe wa demokrasia malkia au mfalme hutoka kwenye koo fulani na hurithiwa.na huheshimika na kila mmnoja kama alama ya umoja na upendo
 
Kuna habari mbaya kutoka Garissa kwamba kuna mtu ametupa hand grenade kwenye polling station ambako kurazilikuwa zinahesabiwa. Bila shaka hawa ni Al Shabab!!! Hakuna mtu aliyejeruhiwa. Pia kuna taarifa kwamba watu wenye silaha huko Garissa wanavishikiria vituo viwili ambako kura zilikuwa zinahesabiwa.

Tiba
 
Kwa kweli mchuano ni mkali, mpaka sasa kuna gepu kama la kura Laki 2, Uhuru anaongoza.
 
Back
Top Bottom