March 04 2013: Kenya's historic poll - Kenya decides!

March 04 2013: Kenya's historic poll - Kenya decides!

ha ha haaa, Africa bado sana na mambo ya technology! Mnakumbuka kipindi kile kwa Bush, USA ilibidi jimbo moja, nafikiri California ilibidi kura zihesabiwe kwa mkono?

Ni Florida mkuu
 
Yawezekana anacholisema Tiba ni sahihi lakini ukweli ni kwamba kura hazijaisha kuhesabiwa kwa hiyo sio rahisi kujua idadi ya watu waliopiga na kama wameshajua idadi ya waliopiga toka jana kazi ingekuwa imeshaisha maana hizo percentage toka jana zinatolewa kwa maana hiyo kama unakubali maelezo ya Tiba kwamba idadi ya waliopiga inajulikana obvious kwa muda wote huo hata kura za mmoja mmoja zingekuwa zishajulikana na kazi ingekuwa imeshaisha.

Masuke,unaijua cheque book?ukiandika ukaitoa si kinabaki kishina?hata karatasi za kura zipo hivyo,vile vishina ndio vinatoa jumla ya watu waliopiga kura,hilo ndio jambo la kwanza kujua,na kwa taarifa yako kati ya watu million 14 waliojiandikisha tayari inajulikan waliopiga ni million 10,ikiwa ni 70% ya waliojiandikisha

Una swali?
 
....... inavyoonekana uhuru atashinda ilingali wengi hawakubaliani nalo wanasubiria kesho kuona watu watapokeaje hayo matokeo. kweli africa sijui tukoje tuwaombee hili jambo lipite salama lisipopita ni balaa, maana kenya mambo yakiharibika ni matatizo hata kwetu

Uhuru Kenyatta

  • Son of Kenya's first President Jomo Kenyatta

Raila Odinga

  • Son of first Vice-President Jaramogi Oginga Odinga


Yeyote kati ya hawa akishinda, hii Kenya ibadililishe jina.

Itoke katika mfumo wa republic...kwenda Kingdom of Kenyatta au Sultanate of Odinga.

Recycling of the family politics.
 
Hapo yawezekana mabeberu wameagiza hivyo baada yakuona kipenzi chao anapelekwa puta.
Server zita crush vipi zote kwa mkupuo? ktk IT huwezi deploy system ambayo haina redundancy, yani server ambayo ipo active inakuwa ina replicate copy ya data hizo ktk server zingine ambazo zinakuwa standby for taking over if any. kama primary server ina-crush basi standby inachukua role promptly, active na standby haziwezi crush kwa wakati mmoja maana haziwi active kwa wakati mmoja. Hii wanayosema mie sii amini sana kama ni sababu.
 

Mkuu ni sawa lakini usimchanganye Mungu kwenye mambo ya uchaguzi, kwanza utawala wa Mungu hauna cha kupiga kura, ni dictatorship kama jeshi!!


Mtumishi wetu, Usimuelewe Mungu vibaya, Mungu anaheshimu upigaji Kura na kunawakati anaruhusu matakwa ya wanadamu.Sitaki kuendelea sana katika hili,nilichosema na ninachosema tuwaombee wakenya wamalize mchakato wa uchaguzi kwa amani.Sababu ni kwamba Mungu anahusika na ukamilifu wa miasha yetu yote
 
Ndio kilichofanyika. Baada ya IEBC kupewa report ya hizo failures ikatoa ruhusa kwa wasimamizi kutumia hard copies kuidentify voters. Wanasema walikuwa na hard copies ready just in case. Halafu mtandao ukaenda down for 6 hours kwa hiyo kukawa hakuna mawasiliano kati ya IEBC na vituo kwa muda huo kupitia mtandao uliowekwa. Mimi sio mtaalam wa IT lakini kwa kutumia common sense mojawapo ya sababu ya mitandao kuwa chini marekebisho kufanyika, sasa hapa tunaweza kujiuliza kuna marekebisho gani yalikuwa yanafanyika?

Kunaposibility kubwa kuwa main server yao imepigwa na-Virus ndio maana imeanza kwikwi. Tena wale Virusi wanao-duplicate data, kwa hiyo msishangae kuona wakirudi hewani ngoma mchezo ushakwisha....:shut-mouth:
 
Hapo yawezekana mabeberu wameagiza hivyo baada yakuona kipenzi chao anapelekwa puta.
Server zita crush vipi zote kwa mkupuo?.... Hii wanayosema mie sii amini sana kama ni sababu.

Hilo liko wazi....yule waliyemfungulia mashtaka ICC akishinda tu...wanatoa arrest warrant.
 
Hv wamesahau yale ya nwka 2007?kupiga kura sio ishu,ishu iko kwenye matokeo Vurugu nyingi ndo huanzia!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForumse
 
Zimeharibiwa makusudi ili kuhakikisha wanampa "ULAIS" wamtakaye. Kama zimeharibika kihalali basi waziweke hadharani tuthibitishe kwamba kweli zimeharibika maana ni nyingi mno.

Hawa IEBC mimi nina soo nao especially when it comes to civil education. Nashangaa kwa nini hawakufanya
elimu jamii in regards to this matter. Kura zilizoharibika ni nyingi mno!
 
Back
Top Bottom