March 04 2013: Kenya's historic poll - Kenya decides!

March 04 2013: Kenya's historic poll - Kenya decides!

Thanks mkuu kwa uongo wako coz hapo taita taveta odinga amepata ushindi mkubwa zaidi ya 92% mkuu refference fuatilia result zinzotangazwa Bomas of Kenya, mkuu.
 
Kaka wakalenjini na wakikikuyu kura zinatosha 51perc > hata wakienda kuhesabia Marekani.... Wait and c

Mkuu nakubaliana na wewe lakini at this point, inabidi tuwasaidie wenzetu kuondoa unnecessary tensions ambazo zinaweza kuleta madhara kwa kuweka kwenye mitandao matokeo yasiyo kuwa rasmi. I believe mwisho wa zoezi itakuwa kama ulivyotabiri.

Tiba
 
ukienda kulala ukiamka jua imekula kwako mkuu!...huyo isaack mwenyewe nasikia kapiga 36hrs bila
usingizi. Zile kura za '07 watu walienda kulala walipoamka wakamkuta kibaki tayari keshaapishwa!

Ogopa sana watu sampuli hii.
umenifurahisha sana (nimecheka sana). Kweli i le ya kibaki inafaa iwekwe kwenye world book of records . Nakumbuka alisema hivi baada ya kuapishwa,' 'Sasa raisi ameshatangazwa na ameshaapishwa, mimi ndie raisi tuheshimiane ''
 
Hiki ni kichekesho Tanzania kuunda tume huru? tangu lini. Tuna rundo la kesi tumeshindwa kufanya hizo tume. Tuliangalie suala hili upesi na lifanyiwe kazi. 2015 si mbali

Tukiwa na nia na tukaacha maamuzi ya ushabiki tutafika. Ni ngumu pale watu wanapochukua pande na kuzishabikia bila kupima uzito wa hoja na uwezo wa mgombea binafsi. Tunatakiwa kuondokana na maamuzi ya kijumla jumla na kuanza kuzingatia yanayosemwa na kuahidiwa na wagombea mmoja mmoja bila kujali itikadi ya chama. Kwa mfano, unaweza kwenda kwenye mkutano wa hadhara wa chama chochote, na ukakuta wanasiasa wanatoa sera za kukashfu, lakini wananchi waanashangilia kwa nguvu zao zote bila kuhoji maswala yao ya kimsingi na kimaendeleo. Sasa kweli hapo tutafika au tutazidi kuwatengenezea mianya ya kutunyonya? Mwisho wa siku tutabaki kushabikia vyama kama tushabikiavyo timu za mpira, wakati tukiendelea kunyonywa na kugandamizwa na tuwashabikiao..
 
umenifurahisha sana (nimecheka sana). Kweli i le ya kibaki inafaa iwekwe kwenye world book of records . Nakumbuka alisema hivi baada ya kuapishwa,' 'Sasa raisi ameshatangazwa na ameshaapishwa, mimi ndie raisi tuheshimiane ''

Kibaki alicheza kama ccm ndo maana alikuja kuaga
 
duuu wasiwasi wangu ni Kinana tu, akikajua hako kamchezo ka ku-hack haki ya mama CDM hatuna chetu 2015

Jamani hebu tujaribu kujiepusha na uzushi. Sababu za IEBC kusitisha on line provisional results si kwa kuwa wamekuwa hacked. Ukweli ni kwamba kulikuwa na technical mistake kwamba zile provisional results zilikuwa zinaonyesha idadi ya kura na percentage kwa kila mgombea. Bahati mbaya, hizo figures hazikujumuisha spoilt votes ambazo zinapashwa kuwa part ya kura zote zilizopigwa. Kama mkiangalia kwa makini hizi final results wameondoa suala la kila mgombea ana % ngapi. Hii imefanyika ili mwisho wa siku mshindi atakayetangazwa awe amekidhi vigezo vyote kisheria.

Sidhani kama Safaricom wanaweza kuwa wajinga kukubali kushiriki kwenye wizi wa kura!!!!

Acha Conspiracy zako Tiba.
Unadhani mambo hayaeleweki? Ni Busara tu imetumika kutoeleza (kwenye media) sababu ya kuanza 'afresh" counting/tallying. Lakini Uwezekano upo kuwa kuna hacking/umafia umefanyika kwenye system ya IEBC, NA SIYO SABABU LEGELEGE unayotaka kutuaminisha hapa ati """Ukweli ni kwamba kulikuwa na technical mistake kwamba zile provisional results zilikuwa zinaonyesha idadi ya kura na percentage kwa kila mgombea. Bahati mbaya, hizo figures hazikujumuisha spoilt votes ambazo zinapashwa kuwa part ya kura zote zilizopigwa. Kama mkiangalia kwa makini hizi final results wameondoa suala la kila mgombea ana % ngapi. Hii imefanyika ili mwisho wa siku mshindi atakayetangazwa awe amekidhi vigezo vyote kisheria.""...This is absurdity Sir!
 
Last edited by a moderator:
ODINGA: 40.7%374,508 votes
50% Official Presidential Results from 23 of 291 constituencies as announced by IEBC at Bomas, Nairob
 
The Dubwana so far, so bad called IEBC has created a situation where a loser won't accept defeat. What a hell is out there?
 
Kweli mpambano ni mkali haswa kati ya Kenyatta na Raila. Hadi kesho asubuhi kitakiwa kimeeleweka.

Kwa upande mwingine naona Bling Bling Mike Songo amemkamata pabaya Bishop Wanjiru. Nakumbuka kuna siku Sonko alikuwa akihojiwa aksema hamuogopi Bishop Wanjiru akasema come Margret come baby! Huyu jamaa anazichemsha sana siasa za Nairobi. Ni machachali kweli kweli ni kijana wa mujini hasa. Huwa nikimuona naishia kucheka tu jinsi anavyovaa na kuongea. Mungu amjalie ashinde nitafurahi. kuna wazee kama akina Sam Ongeri na Ole Ntimama wamepigwa chini. Naona nguli wa siasa za Mombasa akina Kajembe na Balala wameangukia pua. Mukhsa Kitui naye chali!
 
Capture.JPG
Mambo yanaendelea
 
Mkuu ukwelikitugani ni hakika kwamba technolojia imekumbwa na tatizo kubwa na huenda imeingiliwa. Hassan anasema kwamba watumiaji hawakupata elimu ya kutosha kutumia mtandao huo pamoja na mtandao wa simu pamoja na kwamba Safaricom waliwapa VPN kwa ajili yao. Kuna kitu kikubwa tu zaido ya hayo tuliyoambiwa. Tutasikia tu kwamba karatasi zilizosainiwa zimeibwa wakati zikipelekwa Bomas. Fikiria returning officer asafiri na karatasi toka Mandera hadi Nairobi kweli kuna usalama hapo? Afrika ni ngumu kama jiwe
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom