100 others
JF-Expert Member
- Aug 5, 2017
- 10,825
- 38,702
Donald Trump kupitia mtandao wake wa truth social amesema kuwa Marekani itasitisha kwa muda operesheni yake ya kuziongoza meli kupitia Mlango bahari wa Hormuz huku (blockade) kizuizi kikiendelea katika eneo hilo.
Trump anasema Uvushaji wa Meli kupitia Mlango bahari wa Hormuz utasitishwa kwa muda mfupi ili kuona kama Makubaliano yanaweza kukamilishwa na kutiwa saini.
Mapema May 05, Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio alisema kuwa operation epiq fury imefika mwisho, na akasema kwamba Marekani sasa inaangazia operesheni mpya ya kuziongoza meli kupitia Mlango bahari wa Hormuz.
Kutoka kwangu.
Rubio anasema operation epiq fury imekwisha na wamebakiza hio project freedom ya kuzisindikiza meli zilizokwama gulf kupitia mlango bahari wa Hormuz, Trump anakuja kusema na hio project freedom wamesimama kwa muda 😂 😂 .
Tumeshasema hapa kwamba US inatafuta njia ya kujiondoa kwenye vita huku ikijaribu kulinda heshima yake na kudai kuwa imeshinda hii ni ili kuondoa fedheha na kulinda heshima.(face saving strategy)
Trump anatafuta njia kujiondoa kwenye mgogoro huu bila kuonekana kuwa wameshindwa au kudhalilika mbele ya wananchi wao au jumuiya ya kimataifa. Ndio maana alianzisha hii project ya kuitwa project freedom, na ingefanikiwa ungesikia huko truth social jinsi Trump angepiga domo na kujisifu. Lengo ni kubadilisha story kutoka kwenye kushindwa kwa vita kwenda kwenye mafanikio ya project freedom kuziokoa hizo meli zilizokwama Hormuz.
Maana ya kusema wana simamisha kwa muda hio project maana yake ni kushindwa, hizi ni strategies na mbinu za kidiplomasia, kiongozi kama Trump wa US hawezi kukiri kusema ameshindwa abadan.
Mbinu nyingine za kistratejia za kukimbia vita ni kutangaza ushindi na kuondoka ,Declaring Victory and Leaving.
Hii inaitwa save face strategy ni mbinu ya kidiplomasia ambapo kiongozi au nchi inatafuta suluhu inayowawezesha kujiondoa kwenye mgogoro bila kuonekana kuwa wameshindwa au kudhalilika mbele ya wananchi wao au jumuiya ya kimataifa. Ndicho US inafanya.
Baada ya Iran kukaza US imeona itulie.
Hili ni kama lile wakati wa Richard Nixon na vita ya Vietnam Kaskazini mwaka 1973, Nixon alijitoa kwenye vita pasipo kukiri ile vita imemshinda ndipo kukawepo na ile kauli mbiu yake peace with honor akidai makubaliano ya Paris ndio ilipelekea US kuondoa majeshi yake.
Soviet na Afghanistan mwaka 1989 na wao walijiondoa kwenye vita pasipo kukiri wameshindwa , Gorbachev alisisitiza kuwa kujiondoa kwenye vita ile ilikuwa ni matokeo ya makubaliano ya kidiplomasia ya Geneva badala ya kushindwa kijeshi.
UIngereza na Gallipoli mwaka 1915 kwenye vita ya kwanza ya dunia, Uingereza waliweza kubadilisha narrative kutoka kwenye kushindwa kwa vita kwenda kwenye mafanikio ya operesheni ya uokoaji.😂.
China na Vietnam mwaka 1979, baada ya kupambana kwa mwezi mmoja na China kuona mtu mzima anaweza kuaibika na ni vyema aepuke aibu zisizo na maana, walijitangazia ushindi na kuondoa majeshi huku wakidai wametoa kipigo heavy kwa Vietnam.
Kama unasoma posts za Trump huko truth social utagundua ninachozungumzia hapa, utasikia 'great progress', utasoma mengi yanayoonyesha US ni kama ipo vizuri.
Nataka niwaambie hizo zote ni face saving strategy na mara nyingi hizi mbinu znaposhindwa matokeo yake ni pamoja na kushuka hadhi kimataifa kitu ambacho tayari kinaonekana kwa US hivi sasa.