Marehemu Ayubu Kiguru: Shabiki mkubwa wa Sunderland football club miaka ya 1960

Marehemu Ayubu Kiguru: Shabiki mkubwa wa Sunderland football club miaka ya 1960

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
2016%2B-%2B1

Mchango wa kujenga club ya Sunderland Msimbazi Street katika miaka ya 1970

Majuzi hapa kulikuwa na Simba Day.
Nimekaa leo asubuhi na kuwaza vipi Simba ilikotokea.

Sijui kama Simba walifanya kisomo, yaani khitma ya kuwarehemu
viongozi, wachezaji na wapenzi wa club toka enzi za Sunderland.

Ikiwa walifanya kisomo naamini kabisa katika majina ambayo
yaliyotajwa moja litakuwa la Ayubu Kiguru.

Aliitwa Ayubu Kiguru kwa kuwa mguu wake mmoja ulikuwa na
athari.

Hii ilikuwa miaka ya 1960.

Mimi bado mtoto na nikipenda Sunderland na nikimjua Ayubu kwa
karibu sana na sababu ni kuwa Ayubu alikuwa na ubao wa biashara
Soko la Kariakoo na mjomba wangu Bwana Khamis Salum na yeye
alikuwa na ubao wake si mbali na ubao wa Ayubu Kiguru.

Ayubu alikuwa na sura jamil na alikuwa mweupe wa rangi.
Mungu alimjaalia Ayubu kipaji cha kuongea na kubishana.

Soko la Kariakoo enzi hizo lilikuwa moja ya vituo vya ushabiki wa mpira
Dar es Salaam.

Yanga na Sunderland walitawala soko na Yanga washabiki wao wengi
walikuwa na biashara ya kuuza samaki kiasi ikawa watani wao wakiwaita
Yanga, ''Wauza Samaki.''

Siku ya mechi ya Sunderland na Yanga moto ulikuwa unawaka sokoni pale
toka mapema asubuhi.

Ushabiki huo utaendelea kwa juma zima takriban baada ya mechi.

Sasa ikitokea kuwa Yanga imefungwa na Sunderland washabiki wa Yanga
walikuwa tabuni kwa juma zima pale sokoni wakipigwa makombora na
Ayubu Kiguru.

Ayubu alikuwa na uwezo wa yeye peke yake kuwanyamazisha Yanga wote
pale sokoni kwa maneno yake, kejeli na kebehi lakini katika namna ambayo
mtu hawezi kughadhibika bali ni kucheka tu.

Enzi zile za Ilala Stadium kelele za kuzomea zikizidi kutoka uoande wa Yanga
Ayubu atasimama kuwaelekea Yanga na atatoa maneno watu watacheka.

Yanga maneno yakiwaingia kisawasawa na sasa wamepwelewa hawana la
kusema basi watamwambia, ''Wewe Ayubu nani atakuweza bwana kiwete
wewe nyie mlojaaliwa na Allah ni mdomo tu.''

Ayubu alikuwa pia ni bingwa wa matusi.

Jibu litakalotoka litamaliza ubishi wote watu watatawanyika watamuacha
Ayubu anapanga nyanya zake huku amevaa jezi ya Hamisi Kilomoni.

Ilikuwa Sunderland ikishinda Ayubu anachukua kikombe anakujanacho
sokoni anakiweka mbele ya ubao wake watu wanapita wanatunza.

Ayubu alikuwa akitukana lakini si kutokana na hamaki wala hasad ya nafsi.

Ilikuwa ndiyo kusherehesha ushabiki wa Yanga na Sunderlaand wala mtu
haendi Msimbazi Polisi kushitaki kuwa katukanwa na Ayubu Kiguru.

ZOKqAPBmC8q1UbYrbXg59vBZeKzVpKf9Wu3ZBQKJRK8buK7jqXPlZbnYiXjFt74XQ95hda2vVKX8R6peFY-wpn-fcDMOHFgIl6E8IILuYKsSINjCYUQt9iTkttnzb96_Gz-kGjuTQyy2goQtOIFcx5H86rcRP7f1gI96PLk5FD3LudGalWSABrYM2TlVEf7v5sMXVRuyEFYPy8oKsHENjt-CvWIlXP7Yr8eGvaVgegBMHw7mlMwNYRqVdpzD0GSQr_lTQCEk2wSU7j_mxzJ5XcXBYDl31GPx2-CotchSWa5l2sBqVP18o-SRCZexCjWF4v_0ncn0zY0qyT-y3Io2XnxUvG194A9Mdr0BSKhb9XtlayuO5EqMA-0YlAqwkiWOXh3AJ6v4b8M9iPSAiNtIAO-Qj3gI9GcO59NapGKis4a395qK1xm_x4vOsICU4-o3dlqxzBii5aU9roRF6xMwac-dxeiD4spNY01V0JWdp8kLhoqk2aQHG_qArAKpKtmDnqJddC5fHD7flU8Z3q_UWDLGDJfQHe_lFEMbEcnkO_elbaKmiZ67UNQQ-hnMFANgHEpOqN8ySCSs11GQeubtFBzv7ehL7q8l=w596-h657-no

Ilikuwa ''ambition,'' yangu siku moja nivae jezi ya Sunderland lakini kipaji kilikuwa
kidogo nikaishia mchangani.

Rafiki yangu marehemu Jumanne Masimenti (Cosmopolitan FC, Simba na
National Team) siku moja tushakuwa wakubwa kanambia, ''Wee ungecheza
mpira gani bwana uko mazoezini sisi tunapiga danadana, wewe uko pembeni
ushavaa jezi unasoma kitabu. Mchezaji mpira gani anakwenda mazoezini na
vitabu?''

Matokeo ndiyo haya leo niko JF hapa nadarsisha historia.
 
hii ni kumbukumbu nzuri. sijui timu zetu kama zina utaratibu wa kuwaenzi washabiki wakubwa na wachezaji
 
hii ni kumbukumbu nzuri. sijui timu zetu kama zina utaratibu wa kuwaenzi washabiki wakubwa na wachezaji
Myaya...
Zamani kulikuwa kila mwaka hizi club zinafanya khitma ya
kuwarehemu waliotangulia mbele ya haki.

Siku hizi sijasikia.

Club iliyobaki na utaratibu huu ni Saigon peke yao ambao
kila mwaka wao husoma khitma na kufanya karamu watu
wakaalikwa pamoja na viongozi wa serikali.

Hii shughuli kila mwaka inazidi ukubwa na watu wengi sana
wanahudhuria:

AcA3LUTqtgLOHRvM7L47DtjoJg9_E4t2JWOOMwuJ5EuXdvSyXU2hUZfi6ka4OAbGx1TeBm6VrIVB9kmeTtTHhBJUo7X6nUEpu5jHIwjcnBnQEqMZvYVX6Lps2DhWSXEmGW_sjbT2rdvoFd731TBM2zq1nqwYMng59VXPHWCb5zpnxXWjTzEKhim4JvKYt0XN9UiS-uQkgYODMQiFZt8fBMBAPvZbtQikjt4CZR_dAJYtObdpypwbqhlvAQAHRj9KLRqTfPaBBCc9N_iPOPBWRub_9i9kZHkV4d_BxAQmq2lAQ8JR0FGmGCuYuct07Mq10nJZzF0nC0Rl3_mF2CMVV9ONckFc_DbHiPamH_IMFW_vmJSLxWwsE5FON10m-TJHF9l2FvhlcGIMjKhrmfN0Q7Xf4-MW-BE8e2je2U6NCGnFgEcvRNBPmyl_mJ0dh2WoNH12YG0PF4LX9yBlNxhBwl8V3bFDlV4ZAahWFpqzhEsg1rKZalJadwUWgD8U522rSGHrsdFWP1OX_czL3Je_LCyfr7N5FigZ-nuMeLcAUOhFxgtXXeEj5AizgD6vBcuFbQ1PrFPhdFk2vum_DGFMDGD9AasxeK9Z=w876-h657-no

Aliyekuwa Makamo wa Rais Ghalib Bilal katika khitma ya Saigon 2010

2HyQQKyBfjl6iV9knEG3G8mY1ZYw-kDcLcvOdIsKbXw2L1EpksUSutWDbFaHNljQPvGl1j2ZXIZxIs5SKSaRee3llTqDuZrib2N1ehl8xkkJdodinlKzDFjn2vR8GFBBfLSV80rjqfZdjZBIKoJu7-sl1O-iWy5jxMgV9_Z_WsTbTrbfrjsVO-8K7_spkc66EQ_5TW4Hewdv_HrbcS0KrZgnTAphB-w3W6KwJsBaBSE4D7z0xG5PaPPTu1Q8tqdzrx55ergM3uPzEuKOnqqZh-bigqj26sJNoUZOJN9CwNu4IYO9wsv-Huy-m79NSJT9fOfmlyNg1B5Ap5_VnWABY-r3_vA96mXpX5M6uwzqV-4Qngh200t3CZEaSFrDUijnjhcjUnYqSMyFgwvPw1lcQoKJ11mJ-AWBpMVnMJvd6edXH3cSGyL1ltfYF4eUAUehQ-xVjgORRtHEX1f51ROObXqiFvwm4jUgRm_YQOsSP97uIdw2RyfrB8pprg1Hs7BK4fnPa4BE6qjCWoILTZQrAS5CEW-OF_9mNQ-arF-G8n_EJEgIL0Ubo3K5Xc6DKclg6cNYxSGNS13ZUWUqaD2Ql8XKpTBwFuEG=w876-h657-no

Sheikh Rocket

Zm6moXuc7xOvVLqtJUO3RSqVEkOxoZ2vxR30rRwmDsCYAUHC1lcwN1-f0pEScDo91d8vhjtl2gZv65AYSJYyHb_j1NfqPNn6xr70aoYK1hMPybtnGovmvvcEJM5CkeQTHM4oy1AqruSjuIPuxxx1DnRhp6tDMcrNHqlZ6U3RSi0sFAbTwKq31DwZ01ALOnulpX9bTT9qSLw7e8bua16jSQqVYVKYM5mWu9SC5EKgq_6vU7yK53B3QWyXUeKtEJVUcWqIFFcdTGr2QUxD8kgAT0Q74L6YlATVbxS7UxiCMy0UCCk5moaAw9GUQ0TUiDt43mPfzSgaDdkxqCvW-18Jelg-34XS_GSbrZH9Re7qekN2XAg2xkvEXNeFKkVIMxO2WMICXU3OzVVwNkL1OslnxXVvWL9yZqji40SLLicBGriKkYN6S59CRumhs6yhyP5Df9Bd47VXDwdm5vcDKwWEkmsqKxeLzKcdBOiKGwtAGt3VEs8Z9aZwrOqz-Mh5W92Q60DNRPycY6xAYKR_SY3u2nU5Zy8cSC-snHV2ObFlOIxZt9s_oWSnLZCRmVWrI7vPHHCUA0qR0xDON7tzSIYtYWLuOEinhP54=w876-h657-no

Marehemu Athmani Kilambo aliyekuwa mchezaji wa Yanga na Timu ya Taifa miaka ya 1960 - 1970

V_sMAJswn7REGIzfvDX-rNKneH231yguCE9i-YbklbDIjae4i3bvERTXXsXAfSZrNbcHBg7rjkBs1QJf6HmAxMJMLdDlVgqtJXaomy0to_QNh4S_cWzj_jbnIHsEbU3wp_iNPQhW4oJTl1jNcT3S8YVrb63rlXc8v2r3cP-5wB4tQRhzHwzAe7ha9ZWtRXdrrBvlqe_vl28y4jE5VD9jhEw8CxJzCNa1nKg267YqdMFPFF6weJOmLhYIvCQadQrdrY_bJebcCoMykI0CgKK60XMzPva0K5ts8d_nVJ6UZ1jEqf0dxBxT4Qc5Ix2OBBBZvndtVf1qANzswocqKOMgF_DBer75vX531xFRamv8y3t4qfAwEd84Qypdiy6q3jcGtrJTfIRk1cqfFrHjxrNTzmX39vyjRDqeScRUbDnCN22pC5Tq7krVPM0luTy0UgjDF5Ex8LlzspXpGv1PfWsvo12B9VgIbO4Y_9dTRL1Jmz9tkXaAU5rZztbmXpMn6XzSV6IJaDW87Cycab7LF6xxyKG5eNCnuMLdVEd6bD9OMdstrlCfVN9DhIkONvAWqXcm23SSKS3V19y8Sc5ONgHrbHu2k1nBuI_n=w876-h657-no

Marehemu Mohamed Mwita aliyekuwa Mhandisi wa Ndege za Serikali
 
Myaya...
Zamani kulikuwa kila mwaka hizi club zinafanya khitma ya
kuwarehemu waliotangulia mbele ya haki.

Siku hizi sijasikia.
pengine wingi wa mchanganyiko wa wanachama wenye imani tofauti,ikaonekana ni busara either kufutilia mbali ama kuwakumbuka na kuwaenzi kwa namna nyingine.
 
pengine wingi wa mchanganyiko wa wanachama wenye imani tofauti,ikaonekana ni busara either kufutilia mbali ama kuwakumbuka na kuwaenzi kwa namna nyingine.
Tyta,
Kwani wingi unadhuru kitu gani ikiwa hao ''wengi,'' wamekuja
wamepokelewa na kuwakuta watu na mila na maadili yao?
 
Tyta,
Kwani wingi unadhuru kitu gani ikiwa hao ''wengi,'' wamekuja
wamepokelewa na kuwakuta watu na mila na maadili yao?
mila na maadili ''vinaweza'' kubadilika kuendana na wakati,mahitaji,umuhimu,lengo na hata mtazamo,na hasa ukizingatia tunahusisha ''Klabu'' ya Michezo na si asasi/taasisi ya Kiroho.
 
2016%2B-%2B1

Mchango wa kujenga club ya Sunderland Msimbazi Street katika miaka ya 1970

Majuzi hapa kulikuwa na Simba Day.
Nimekaa leo asubuhi na kuwaza vipi Simba ilikotokea.

Sijui kama Simba walifanya kisomo, yaani khitma ya kuwarehemu
viongozi, wachezaji na wapenzi wa club toka enzi za Sunderland.

Ikiwa walifanya kisomo naamini kabisa katika majina ambayo
yaliyotajwa moja litakuwa la Ayubu Kiguru.

Aliitwa Ayubu Kiguru kwa kuwa mguu wake mmoja ulikuwa na
athari.

Hii ilikuwa miaka ya 1960.

Mimi bado mtoto na nikipenda Sunderland na nikimjua Ayubu kwa
karibu sana na sababu ni kuwa Ayubu alikuwa na ubao wa biashara
Soko la Kariakoo na mjomba wangu Bwana Khamis Salum na yeye
alikuwa na ubao wake si mbali na ubao wa Ayubu Kiguru.

Ayubu alikuwa na sura jamil na alikuwa mweupe wa rangi.
Mungu alimjaalia Ayubu kipaji cha kuongea na kubishana.

Soko la Kariakoo enzi hizo lilikuwa moja ya vituo vya ushabiki wa mpira
Dar es Salaam.

Yanga na Sunderland walitawala soko na Yanga washabiki wao wengi
walikuwa na biashara ya kuuza samaki kiasi ikawa watani wao wakiwaita
Yanga, ''Wauza Samaki.''

Siku ya mechi ya Sunderland na Yanga moto ulikuwa unawaka sokoni pale
toka mapema asubuhi.

Ushabiki huo utaendelea kwa juma zima takriban baada ya mechi.

Sasa ikitokea kuwa Yanga imefungwa na Sunderland washabiki wa Yanga
walikuwa tabuni kwa juma zima pale sokoni wakipigwa makombora na
Ayubu Kiguru.

Ayubu alikuwa na uwezo wa yeye peke yake kuwanyamazisha Yanga wote
pale sokoni kwa maneno yake, kejeli na kebehi lakini katika namna ambayo
mtu hawezi kughadhibika bali ni kucheka tu.

Enzi zile za Ilala Stadium kelele za kuzomea zikizidi kutoka uoande wa Yanga
Ayubu atasimama kuwaelekea Yanga na atatoa maneno watu watacheka.

Yanga maneno yakiwaingia kisawasawa na sasa wamepwelewa hawana la
kusema basi watamwambia, ''Wewe Ayubu nani atakuweza bwana kiwete
wewe nyie mlojaaliwa na Allah ni mdomo tu.''

Ayubu alikuwa pia ni bingwa wa matusi.

Jibu litakalotoka litamaliza ubishi wote watu watatawanyika watamuacha
Ayubu anapanga nyanya zake huku amevaa jezi ya Hamisi Kilomoni.

Ilikuwa Sunderland ikishinda Ayubu anachukua kikombe anakujanacho
sokoni anakiweka mbele ya ubao wake watu wanapita wanatunza.

Ayubu alikuwa akitukana lakini si kutokana na hamaki wala hasad ya nafsi.

Ilikuwa ndiyo kusherehesha ushabiki wa Yanga na Sunderlaand wala mtu
haendi Msimbazi Polisi kushitaki kuwa katukanwa na Ayubu Kiguru.

ZOKqAPBmC8q1UbYrbXg59vBZeKzVpKf9Wu3ZBQKJRK8buK7jqXPlZbnYiXjFt74XQ95hda2vVKX8R6peFY-wpn-fcDMOHFgIl6E8IILuYKsSINjCYUQt9iTkttnzb96_Gz-kGjuTQyy2goQtOIFcx5H86rcRP7f1gI96PLk5FD3LudGalWSABrYM2TlVEf7v5sMXVRuyEFYPy8oKsHENjt-CvWIlXP7Yr8eGvaVgegBMHw7mlMwNYRqVdpzD0GSQr_lTQCEk2wSU7j_mxzJ5XcXBYDl31GPx2-CotchSWa5l2sBqVP18o-SRCZexCjWF4v_0ncn0zY0qyT-y3Io2XnxUvG194A9Mdr0BSKhb9XtlayuO5EqMA-0YlAqwkiWOXh3AJ6v4b8M9iPSAiNtIAO-Qj3gI9GcO59NapGKis4a395qK1xm_x4vOsICU4-o3dlqxzBii5aU9roRF6xMwac-dxeiD4spNY01V0JWdp8kLhoqk2aQHG_qArAKpKtmDnqJddC5fHD7flU8Z3q_UWDLGDJfQHe_lFEMbEcnkO_elbaKmiZ67UNQQ-hnMFANgHEpOqN8ySCSs11GQeubtFBzv7ehL7q8l=w596-h657-no

Ilikuwa ''ambition,'' yangu siku moja nivae jezi ya Sunderland lakini kipaji kilikuwa
kidogo nikaishia mchangani.

Rafiki yangu marehemu Jumanne Masimenti (Cosmopolitan FC, Simba na
National Team) siku moja tushakuwa wakubwa kanambia, ''Wee ungecheza
mpira gani bwana uko mazoezini sisi tunapiga danadana, wewe uko pembeni
ushavaa jezi unasoma kitabu. Mchezaji mpira gani anakwenda mazoezini na
vitabu?''

Matokeo ndiyo haya leo niko JF hapa nadarsisha historia.
syd
Umenikumbusha mbali sana na kariakoo yetu ilee
 
pengine wingi wa mchanganyiko wa wanachama wenye imani tofauti,ikaonekana ni busara either kufutilia mbali ama kuwakumbuka na kuwaenzi kwa namna nyingine.
Imani mbalimbali siyo sababu ya kuacha kuwakumbuka waliotangulia-hii ni mila na tamaduni yetu na haizuii kwenye visomo hivyo watu wenye imani tofauti kuhudhuria.
 
Imani mbalimbali siyo sababu ya kuacha kuwakumbuka waliotangulia-hii ni mila na tamaduni yetu na haizuii kwenye visomo hivyo watu wenye imani tofauti kuhudhuria.
Umenisoma na kunielewa vizuri lakini?
 
me ni mnazi wa YANGA ila historia na maneno yako yamenikosha ni vema kuwakumbuka waliotangulia kwa wema wao
hata wewe pindi ukitangulia mbele ya haki hakika tutakukumbuka kwa nyuzi zako nzuri za historia
ni kawaida watu wataona umuhimu wako pindi utakapokuwa haupo tena katika uso wa dunia 7bu ni wachache wenye umri wako na wenye kuijua historia ya jiji la DAR ES SALAAM kwa undani ambao wapo mtandaoni kutuhabarisha yaliyopita miaka mingi kama wewe
MWENYEZI MUNGU Akufanyie umri mrefu zaidi wenye afya tele
 
Ina maana hizo timu zilikuwa hazina wachezaji na viongozi wa deen nyingine zaidi ya islam? Wakina william mwaijibe, Rafael Paul na wengine nao hawaitaji kusomewa misa?

Achana na hayo mambo kaka Mohamed Said timu zimepanuka na zina watu wa kila deen, kwa nini iwe kisomo tu? Mbona huulizii misa?
 
Hivi vilabu viwili vilijengwa na masikini wa pesa ila matajiri wa mioyo ya mafanikio visomo vyao vidogo maskini ila mahaba ndo yamefanya tumezikuta ila kuziendeleza ndio shida pamoja na elimu na uwezo bado hatujapata watu wenye nia thabiti ya kuziona zina songa mbele na kukidhi viwango vya kimataifa.
 
Ina maana hizo timu zilikuwa hazina wachezaji na viongozi wa deen nyingine zaidi ya islam? Wakina william mwaijibe, Rafael Paul na wengine nao hawaitaji kusomewa misa?

Achana na hayo mambo kaka Mohamed Said timu zimepanuka na zina watu wa kila deen, kwa nini iwe kisomo tu? Mbona huulizii misa?
Kituko,
Nilichosema mimi ni kuwa wakifanya khitma na sasa hawafanyi.

Ikiwa mambo yamebadilika hapana neno mimi nimeeleza tu
historia ya Sunderland kama ilivyokuwa.

Ingekuwa Sunderland walikuwa wanasoma misa ningelisema.
 
me ni mnazi wa YANGA ila historia na maneno yako yamenikosha ni vema kuwakumbuka waliotangulia kwa wema wao
hata wewe pindi ukitangulia mbele ya haki hakika tutakukumbuka kwa nyuzi zako nzuri za historia
ni kawaida watu wataona umuhimu wako pindi utakapokuwa haupo tena katika uso wa dunia 7bu ni wachache wenye umri wako na wenye kuijua historia ya jiji la DAR ES SALAAM kwa undani ambao wapo mtandaoni kutuhabarisha yaliyopita miaka mingi kama wewe
MWENYEZI MUNGU Akufanyie umri mrefu zaidi wenye afya tele
Mzimu...
Amin kwa sote.

Bahati niliyokuwanayo mimi ni kuwa nilizaliwa hapa Dar es Salaam
kwa hiyo haya yote nimeyaona kwa macho yangu mwenyewe.

Na mimi napenda kuieleza Dar es Salaam kama ninavyoijua.
 
Kituko,
Nilichosema mimi ni kuwa wakifanya khitma na sasa hawafanyi.

Ikiwa mambo yamebadilika hapana neno mimi nimeeleza tu
historia ya Sunderland kama ilivyokuwa.

Ingekuwa Sunderland walikuwa wanasoma misa ningelisema.
Ni sawia tu Mzee wetu! Kama tunayemkumbuka alikuwa mkristo basi ifanywe misa! Na kama ni mwislam basi afanyiwe kisomo kulingana na imani yake alipokuwa hai!! Just kuwakumbuka na kuwaombea kheri! Asante mzee.
 
syd
Umenikumbusha mbali sana na kariakoo yetu ilee
Abunwasi,
Siku zimekwenda.

Kwenye maziko ya Abdulrahman Lukongo nilikutana na Hamisi
Kibunzi
nikamweleza mazungumzo niliyokuwanayo na marehemu
Athmani Kilambo kuhusu yeye na Arthur Mambeta, Yusuf Salum
na wengineo.

Nikamwambia kuwa Yanga wakiwahusudu sana baadhi ya wachezaji
wa Sunderland na akinitajia majina.

Kilambo anasema, ''Unajua kulikuwa na watoto kule Sunderland wana
mpira mzuri sana kama Kibunzi na Arthur Mambeta na Mzee Mangara
akiwataka awalete Yanga kuongeza nguvu ulinzi na ushambuliaji...''

Kilambo anasema kuwa Mzee Mangara anatuuliza, ''Mimi nikamwambia
kuwa hawa watoto akina Kibunzi na Arthur hata tukiwaleta Yanga
hawataweza kucheza mpira huku wana mapenzi makubwa sana na
Abidjan.''

Siku zile jina lingine la Sunderland ilikuwa ''Abidjan,'' na sijui lilitokana
na nini.

Kibunzi alikuwa hana habari hizi hata chembe.

Akacheka akanambia, ''Kilambo kasema kweli sisi tusingeweza kucheza
Yanga tukipenda sana Sunderland.''

Kilambo alikuwa mzungumzaji wangu mkubwa na akijua mie siipendi
Yanga sasa yeye ikawa kila siku kuniweka roho juu.

Mechi ya Yanga na Simba Zanzibar mwanzoni 1970s, Yanga walitokea
Nigeria, basi kanifata ofisini kunitisha ananiambia, ''Tumekufanyieni
fitna kubwa Zanzibar mnachukiwa kama Hizbu.''

Kweli Zanzibar tukafungwa Yanga wakachukua kikombe.

Kilambo alikuwa muungwana akiingiliana na wachezaji wa Simba vizuri
sana na akipenda sana kumtania Emmanuel Mbele ambae akipenda
kumwita, ''Fullup.''

m0AkTF7F_x7v3uUz2l23EpBUg-NuCixyFrth0Tb9uYA0crQq3KNKaXelEjFoRNlxHFUONs3932iil-jrro7ThdOFtCK4OJbIxeXITF01HigMjTKPcqpoNxAKuN0l192NamsWUTlv296Ip3oMJIexF0KtwXqD13xbZJPRayjMmnY4taN7X1TJ1DlLZiA5mzLXazFBLJAFseuk1P146pLPgvutcKSIT52ouzgr1BRO8FoAiEXBvuMUsSsojbL1zUNC0CZ7EtVwopylKgWKd3uPNGlk_zmL7Kt7N-2ZfZ37ltzp3OkmehLJGSUUBDC9bMcUVXAzaEf_Rkw-y_8lvWuaCeiQ7O8Igu9JksHFZ2RI6dHYce9X4yWhVwsdODcaOZTwo4wiSeCS5jgdbtppZtWMXn7TOyTQQ1VhZcRFkoPrFHXPFsuEGpBYONvF5kk4WVJsi3wYgcb8sTsv2608j8TLTonSeZSfD32Fehp36W0amrSqgS80S2BUncyiMsC379ii_fNZVYGfswq0h8bG5P1CV-62yKv9xQGueOrOuwR4Ezl_dhY-KLBKMNPSxeFR5B2XzcieroR0MEAm5G4eV-_4eT_iKhj-aXF6=w876-h657-no

Waliosimama wa tatu kulia ni Athmani Kilambo, wa tano Abdulrahman Lukongo
timu ya East African Cargo Handling Services

Akijua mapenzi yangu ya mpira na alikuwa akinipa habari nyingi sana za
Yanga hadi uchawi wa kuloga mechi.

Siku za mwisho za maisha yake tukiswali pamoja msikiti wa Manyema na
akija akiniona hataingia ndani msikitini sharti kwanza aje anisalimie.

XGLv9aiIr6aRQxikp3KyYIemtMOzk4wiDYGsKgXZBPoBx4Lvnzjjj_6InCUxJztppvycitZbf2umdl3cwi2otJcRzl1hJLtu2xQ35G7TMOJFipVN3pKHhDroX68OGm3xwzGTyzR48CCGtpXeLcHyfZupQA59VUMTLmMaLGN_WbQboAzLy5hnvKjcxJgV6VL2gjat8eMsUBQy4aWaQcr_TaIhlumWzuirk9mnF5is52gCmRQ9zTHG8wjGPtBh98lVmZZf5iENiVLXjZztr5jBpEZp4Kwyr4XQU0hbb5B7C82D0nC99pQ_NpTtkbA-4qDlRw4uqBc9gnWofHNj3G8zq0XE4D29dOi9NimCBpBKelwss7pmrnLQsIoRyV04AI6E-oFCUf8ccuinwK38CKaLdNYZh8Mwx0WGGpbyl2jPyud94FeGevOVNw9MU_dPPvz6L93r1--UQJ9Gph7MGwMzre6RCDSVtZgZeWZ0S3pBw5xUILlU--LPdlxkCRii1dPHd0lr2eqFspgNUmM3cEGqSPzuPlUlmbJkW5j6bBrUHBA_NXeCJnkk1GBgZPreFpevwVR-iuE1Mt9EOFMMUSxO7duU-LsuljQ=w330-h220-no

Athmani Kilambo (Yanga) kushoto na Abuu (Cosmo)
kulia kwenye khitma Saigon.

cVvBeW3-lqa-Sd7MqUlDplfoUmWunLyb39y1HpawtAKj8pHw3WNTEvxKiA7ZuHrnEkYeEVbWdPmM7h8Rw-gNsWNRmTRpYU6speUv4RGaooeiDXtbuOocZ1LWjosiMRYnLYZn62Eh4pJLSJdr3B-xiMLsnnAhuVOAjrd7BgX6SseyklnKhX3y-VDeD0bTO4oM195dRkI1PIYApi75HUH9ngf-TaMlPe6CTf5NgWy3ESnwxwdaOJQFLhwLbSUph0eYR8UF1p4RuUjCzvy263-LMhD5ZyM850psRTbRLcEK_Qd4JFf0XTuF2ltLiUh3ROOadG7SBQNaXkaGEE_QtEnYx60z1GmE8kgaYqUHd8-teqAL4ck2RYet6xe-JM-72LAQzKWdJdOmIiVZdLUx4TNID7BtQaBN1umspcDn31bgc5eithBOHlhhDB6HdfYPEqK302gmwfDeq97AzPSuUDF4OwAdTGBLK-LvH-ZGkwTCNrmu1klTT_PPyFsnR8F_PF7ox0SEsPIAlXli5sMmBurAIgCYX5iAJTbzEiDvvXBu1njpIhTcUvrMcgJYYwT_BJ8Ypp0zmI7fg1U9BwmAnUiTedwbQw9XMog=w986-h657-no

Kushoto wa kwanza mbele ni Hamisi Kibunzi, nyuma kulia wa kwanza Arthur Mambeta
anaemfuatia ni Emmanuel Mbele na wa sita ni Yusuf Salum.
 
Back
Top Bottom