Verification code ya Mungu? Ndio code ambayo Muhammad aliitumia kuthibitisha kwamba Mungu alimtuma Malaika Gabrieli kwake au Verification code ya nini hasa?
Ndugu Quran ni muujiza wa karne. Tofauti na mitume wengine walitumia muujiza ile sawa na wakati wao. Mfano wakati wa mabii MUSA na Yesu waliamini ktk uchawi. Mtume wetu Muhammad hakuletwa ktk karne ya walioamini ktk uchawi, laa kaletwa ktk karne ya sayansi na teknolijia. Ambapo number ndizo zinazoleta fact.
Verification code ni numba maalumu ktk hesabu. Na hesabu ndio lugha peka yake ambayo inaweza kutuwezesha dunia nzima tukawasiliana bila kujalisha utaifa wetu, ukabila wetu wala lugha tunazozungumza kwa sababu hesabu ndio ukweli unaothibutishika (provable facts)
SABABU ZA KUELEZEA HESABU NDANI YA QURAAN
1: Tunaeleza hesabu ndani ya quraan kwa kuthibitisha hifadhi ya quraan kwa maana kama ndani ya quraan hakuna kilichoongezeka wala kilichopungua hivyo kwa kutumia hesabu tunaweza kulithibitisha hili.
Hii inatufahamisha kwamba quraan yoote ni kama sentensi moja iliyobeba ujumbe mmoja kimaana na kimaandishi
Katika hili tunaweza kupata (balance perfection of words) uwiano uliotimia wa maneno yoote katika quraan
Hii ina maana kwamba kila kitu kiko mahali pake na hakuna kinachostahili kuongezwa wala kupunguzwa na kama itatokea kutaongezwa ama kupunguzwa chochote huu uwiano uliotimia wa kimahesabu katika quraan woote utaparaganyika.
Hii ina maana kama ile quraan iliyoshuka wakati wa mtume (sallah llahu alayhi wassalam) ndio quraan ambayo tuko nayo sisi leo hii.
Hivyo kwa wale ambao wataifuata quraan kikamilifu leo hii hawatakuwa na tafauti na wale waliokuwepo wakati wa mtume wetu (sallah llahu alayhi wassalam) sote tunapokea ujumbe mmoja kutoka kwa Allah.
2: verification code ndani ya quraan ni (intelectualy defence) ni hoja ya kiakili kwetu dhidi ya wapinzani wa quraan.
Leo tunashuhudia mashambulizi dhidi ya mtume wetu ( sallah llahu alayhi wassalam) uislam na quraan katika vyanzo mbali mbali vya habari, hivyo hesabu ndani ya quraan ni hoja nzito kwetu kwa wale wapinzani wa Uislam.
Uwiano wa kimahesabu katika quraan ni mwingi sana ni wa kushangaza na pia uko juu sana ya akili za kibinaadamu( muujiza).
Miaka 1400 iliyopita katika jangwa la arabuni ambapo hakukuwa na teknolojia yoyote ile hakuna ambae angeweze kutengeneza uwiano wa kimahesabu kama uliopo kwenye quraan.
Kama bado huiamini kwa ushahidi wa kisayansi Quran inakichallenge ktk
surah ya Baqarah 2:23
And if you are in doubt about what We have sent down upon Our Servant [Muhammad], then produce a surah the like thereof and call upon your witnesses other than Allah, if you should be truthful.
Ni ajabu mtu an a challenge kwa Nia ya ubishi ilhali hiyo Quran inamchallnge athibitishe hoja za kama kweli binadamu wa kawaida unaweza kuiandika basi tuandikie wewe aya moja. Sisi tutaitest kisayansi zaidi. Ukishinda hilo basi verify kama ukweli bibi lia ni kitabu toka kwa Mungu.
Karibu tena kama utahitaji ufahamu zaidi.