Marekani: Afisa wa polisi aliyefutwa kazi Derek Chauvin ashitakiwa kwa mauaji ya George Floyd. Mkewe ataka talaka

Marekani: Afisa wa polisi aliyefutwa kazi Derek Chauvin ashitakiwa kwa mauaji ya George Floyd. Mkewe ataka talaka

Huyo jamaa kaua kwa kukusudia. George alikuwa analalamika kabisa kuwa hawezi kupumua ndiyo kwanza jamaa anaongeza pressure! Raia wanamuambia utamuua jamaa hajali ndiyo kwanza anaongeza pressure! Hata baada ya George kukata moto jamaa hajaonyesha kushituka anaonekana yupo kawaida tu!

Halafu anashitakiwa kwa 3rd degree murder? Hii ndiyo Amerika. Mara nyingi raia wanalalamika polisi wanaua raia halafu hawachukuliwi hatua yoyote! Wana resign halafu mafao yao wanapata kama kawaida! Wengine wanahamishwa wanapelekwa jimbo jengine.

Polisi wa Amerika wametofautiana sehemu ndogo sana na wa-kibongo!
 
Hili jambo ni jepesi sana kulizungumza ila linapokuja mbele ya sheria ni gumu kuliko maelezo.

Kuna watu wameshangazwa na tukio la mtuhumiwa kufunguliwa mashitaka ya 3rd degree murder. Sijajua labda walitakaje?

Ndiyo maana nauliza.
Nahisi wengi wana jaji kuhusiana najamaa kupewa kesi yakuuwa bila kukusudia wakati jamaa kiuhalisia ama kiuno unahisi kabisa alikusudia kwa alivyofanya
 
Bongo siasa za chama tawala kandamizi! Amerika Ubaguzi, mbegu ya ubaguzi bado ipo! White people wengi sana wanawafanyia ubaguzi black. Shukrani kwa teknolojia ndiyo inayowaumbua wakionekana wanafanya hivyo vitendo. Halafu baadae wanakuja kwenye vyombo vya habari, mitandao ya kijamii kwa machozi yao feki na kuomba radhi.

Mbegu ya ubaguzi bado ipo Amerika. Ndiyo maana 2pac aliwaambia "Before we find world peace
We gotta find peace and end the war in the streets"
 
Nahisi wengi wana jaji kuhusiana najamaa kupewa kesi yakuuwa bila kukusudia wakati jamaa kiuhalisia ama kiuno unahisi kabisa alikusudia kwa alivyofanya
Kuhisi tu kuwa alikusudia si hoja mbele ya sheria. Kazi kubwa ni kuthibitisha mashitaka beyond reasonable doubt.
 
Huyo jamaa kaua kwa kukusudia. George alikuwa analalamika kabisa kuwa hawezi kupumua ndiyo kwanza jamaa anaongeza pressure! Raia wanamuambia utamuua jamaa hajali ndiyo kwanza anaongeza pressure! Hata baada ya George kukata moto jamaa hajaonyesha kushituka anaonekana yupo kawaida tu!

Halafu anashitakiwa kwa 3rd degree murder?! Hii ndiyo Amerika. Mara nyingi raia wanalalamika polisi wanaua raia halafu hawachukuliwi hatua yoyote! Wana resign halafu mafao yao wanapata kama kawaida! Wengine wanahamishwa wanapelekwa jimbo jengine.

Polisi wa Amerika wametofautiana sehemu ndogo sana na wa-kibongo!
Kuna tatizo gani kwa yeye kushitakiwa kwa 3rd degree murder kwa sasa? Isitoshe uchunguzi bado ungali ukiendelea na huenda makosa yakaongezeka.

Kumshitaki kwa 3rd degree murder kunaweka wepesi wa mashitaka kuthibitishwa mahakamani kutokana na tukio lenyewe tofauti na kama angeshitakiwa kwa 2nd degree ama 1st degree ambapo kutahitaji uwasilishaji wa ushahidi wa kutosheleza kuthibitisha mashitaka hayo, ushahidi ambao pengine bado uchunguzi haujauweka bayana.

Itakuwaje pale watakapomshitaki kwa 1st degree ama 2nd degree murder na ushahidi wa kutosheleza kumfunga ukakosekana? Kumbuka kuwa kushitakiwa ni jambo moja na kukutwa na hatia ni jambo jingine, kinachohitajika ni uthibitisho usio na shaka dhidi ya mtuhumiwa la sivyo mtuhumiwa anaweza kuachiwa huru.

3rd degree murder si mashitaka mepesi pia maana yanaweza kumuweka mtu ndani hadi miaka 25 kwa maana hiyo hili limefanyika kwa sasa kuhakikisha kuwa kivyovyote vile majibu ya uchunguzi yatakapopatikana bado kuna uwezekano wa jamaa kukaa ndani kwa muda mrefu tu.
 
Je, muuaji alikusudia?
Hadi mtu ashitakiwe kwa mayaji kwa 1st or 2nd degree order huyo mtu inabidi aseme ninaua kwa makusudi Nini? Maana naona Kama kwa Hilo Kama unasema ushahidi wa kumpata na hatia kwenye 1st au 2nd itakuwa mgumu Basi hakuna mtu anayeweza kushtakiwa kwa ngazi hizi hadi muuaji akiri au aandike statement kabisa ya Kanka ya kwenda kuua
 
Wanajitahid Nyeusi kuigeuza Nyeupe hahahahaha
Hadi mtu ashitakiwe kwa mayaji kwa 1st or 2nd degree order huyo mtu inabidi aseme ninaua kwa makusudi Nini? Maana naona Kama kwa Hilo Kama unasema ushahidi wa kumpata na hatia kwenye 1st au 2nd itakuwa mgumu Basi hakuna mtu anayeweza kushtakiwa kwa ngazi hizi hadi muuaji akiri au aandike statement kabisa ya Kanka ya kwenda kuua

Sent from my JSN-L21 using JamiiForums mobile app
 
Daudi Mwangosi aliuawa lkn yule kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda aliyeamuru mauaji alipandishwa cheo na kuhamishiwa makao makuu.

Wakati tunaona kibanzi kwenye jicho la wengine tusisahau kuona boriti kwenye jicho letu.

Polisi ni polisi tu na ndio maana wengi wao wakistaafu huadhirika sana kimaisha kwa sababu wengi wao wakiwa kwenye utumishi kazi yao kubwa ni kuwafanyia wenzao dhuluma. They're very hopeless indeed.
 
Yani inakuwaje kuua bila kukusudia ktk maxingira kama yale? Ndg yetu alijitetea na bado akatetewa lakini wauaji hawakusikia wakapiga pingu nakumuua!!! Inakuwaje kuua bila kukusudia?
 
Jukwa la kimataifa na uzi unazungumzia mauaji huko Marekani ila unakuta mtu anaingiza habari za mauaji ya polisi Tanzania, yani kama hajapenda kuzungumziwa hayo mauaji ya huko Marekani.

Sijui tuna matatizo gani wabongo!
 
Kule kwetu aliyemuua akwilini kesi imeends vise varsa
 
Mapolis wamerekani awajitambui wnafanana na sizonje Full brutality
 
Back
Top Bottom